matatizo ya kuingiza siasa kwenye mambo ya msingi

paul vicent

Member
Jul 13, 2012
44
4
kuna wakati nilisema watu wengi walio kwenye nyanja za siasa wamekua kikwazo kikubwa cha maendeleo.Nasema haya kwa sababu katika pitapita zangu huku mkoa Morogoro katika kijiji cha Ruaha nilikutana na baadhi ya wananchi wakilalamika kuhusu uchaguzi wa kijiji chao baada ya kuwaondoa viongozi wao madarakani kutokana na ubadhilifu walioufanya.Kwa sababu hiyo vyama vyote vya siasa havina budi kushiriki'hapo ndio tatizo lilipoanzia kwani baada ya chama kilichokuwa kikitawala awali kugundua wenzao wana nafasi kubwa ya kushindi wakaanza kuleta vikwazo hata kufikia kutumia dola..Kitu hiki kimewafanya wana Ruaha kushindwa kufanya shughuli za maendeleo kwa kijiji chao.Kwani sasa suala hilo limechukua sura kisiasa hivyo kupelekea hata ukusanyaji wa ushuru kutofanyika hivyo pato la kijiji kushuka kwa asilimia kubwa .Pia miradi ya kijiji kukosa msimamizi .pia sekta za usalama wa raia kuingilia mambo ya siasa zimeleta chachu ya kutopatikana suruhu ya haraka maana kila litakalofanyika kwa sasa linaonekana ni siasa.haya ndiyo matatizo ya kuingiza siasa kwenye mambo ya msingi.
 

Attachments

  • Africa_Flag_Map_by_lg_studio.png
    Africa_Flag_Map_by_lg_studio.png
    43.4 KB · Views: 57
Back
Top Bottom