Matatizo ya kuchubuka na kupata vidonda kwenye ulimi ni zika?

Bwiree

Senior Member
Nov 12, 2016
164
103
Wapendwa wana jukwaa naombeni kujua huu ni ugonjwa gani, unasababishwa na nini na matibabu yake nini? Maana hapa mtaani kwetu unasumbua watu wengi hasa vijana wakike na wakiume ..... Tusaidieni tupone.... Asanteni
7230761dd0f5a222a17bf15f6d861de5.jpg

IMG_20170118_121941.jpg
 
Attachments

  • IMG_20170118_121941.jpg
    IMG_20170118_121941.jpg
    4 KB · Views: 394
Hiyo kitu huwa inamsumbua sana binti yangu...huwa inakuja na kupotea yenyewe...nimewaona madaktari kadhaa bila mafanikio...ila kwa Mara ya Mwisho Dr niliyekutana naye aliniambia eti hyo kitu haina tiba ndo hvo eti mnakuja na kuisha yenyewe... Kuna dawa fulani nikishapewa ni multivitamins ukitumia inaisha faster ila ukiacha hali inarudi pale pale.

Kwa sasa ana muda kama miezi sita hv sijaona hyo hali...nilisumbuka sana mwanzoni yaani mpaka nimezoea.
 
Wapendwa wana jukwaa naombeni kujua huu ni ugonjwa gani, unasababishwa na nini na matibabu yake nini? Maana hapa mtaani kwetu unasumbua watu wengi hasa vijana wakike na wakiume ..... Tusaidieni tupone.... Asanteni
7230761dd0f5a222a17bf15f6d861de5.jpg

View attachment 461221

ULIMI NA UWEZO WAKE WA KUONESHA MAGONJWA

Bila shaka umewahi kwenda hospitali kuonana na daktari na ukajikuta ukiambiwa utoe ulimi nje ili daktari aangalie ulimi wako.

Wengine wetu tunafahamu kuwa ulimi matumizi yake ni kutusaidia katika kutambua ladha, kusaidia katika kuunda maneno wakati wa kuzungumza.

Hata hivyo, madaktari wanaeleza kuwa unaweza kufahamu maradhi anayougua mtu kwa kuangalia ulimi wake tu, kutokana na kiungo hicho kuwa na uwezo wa kuonesha dalili za iwapo mtu ana homa, kikohozi, kisonono, kichwa, tumbo, kisonono na maradhi yanayohusiana na HIV pamoja na kufeli kwa ogani za mwili.

Ulimi wenye afya kwa kawaida unatakiwa uwe msafi, wenye rangi ya pinki na wenye vitonetone ambavyo ndivyo hutumika kubainisha ladha mbalimbali.

Hata hivyo kwa kawaida ulimi wenye rangi nyekundu au mweupe ni dalili ya kuwa na maradhi kama fangasi. Kadhalika ulimi uliovimba ni dalili kubwa ya mtu kuwa na mzio.

Pia ulimi ni mojawapo ya kipimo kinachoweza kuonesha iwapo kinga ya mwili imeshuka. Yote hayo ni kutokana na kiungo hiki kuwa na uhusiano mkubwa na mwili wa binadamu na ogani za ndani ya mwili.

Kwa mfano, anasema ulimi kuwa na weupe mithili ya maziwa ya mgando ni dalili ya fangasi na maradhi ya kinywa mengine yanayohusiana na zinaa.

Wataalamu wa afya wanasema ulimi wenye rangi nyeusi au usio na rangi ni dalili kubwa kuwa mtu huyo ametumia kwa muda mrefu dawa za antibayotiki au ongezeko la fangasi kwa mtu anayeishi na Virusi vya Ukimwi.

Ili kutumia ulimi kama kipimo, vitu vifuatavyo huangaliwa ikiwa ni pamoja na rangi yake, umbile, yaliyomo kwenye ulimi, unyevu wake, ukubwa na ulaini wake.

Pamoja na hayo,ulimi ni kigezo tosha cha kujua iwapo mtu anaugua magonjwa ya zinaa, kama ulimi una mistari mirefu hiyo ni dalili ya magonjwa ya zinaa.

Ukiwa na Shida yoyote ile
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Doctor.MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
ULIMI NA UWEZO WAKE WAKUONESHA MAGONJWA

Asante doctor sasa kwatatizo langu tatizo linaweza kuwa nini? Na matibabu yake nini? Nisaidie kama ivyo iona picha
 
Ulimi na nyama ya ulimi. maradhi na chanzo cha maradhi ya kinywa. kinga na tiba ya maradhi mbalimbali kupitia ulimi.
kinyama kidogo kikisalimika siku hiyo mwili wote umesalimika.
Ulimi una mambo makubwa sana.
 
Back
Top Bottom