Matatizo ya kiakili

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,392
33,263
Matatizo ya akili husababisha tofauti jinsi mtu anavyo fikiria na kufanya mambo Fulani kulingana na uwezo wake wa kawaida.

Pata habari kuhusu jinsi chanzo na dalili.Angalia cha kutizama, jinsi ya kujikinga, na matibabu yake

Alzheimer's/Dementia


Alzheimer’s ni nini?
Ni mojawapo ya hali zinazo sababisha usahaulifu na kuchanganyikiwa. Huwashika sanasana wazee. Huwa wasahaulifu na mara nyingi huchanganyikiwa. Hali hii hutendeka wakati ambapo seli (cells) kwenye sehemu fulani za ubongo hufa.

Kinachosababisha hali hii hakijulikani hata hivyo, kuwa na hali hii huweza kusababishwa na ugonjwa wa Parkinson's, homa, ama hawili wa mtu unaposhindwa kukatiliana na dawa fulani. Dalili za Alzheimer’s ni sawa na usahaulifu na kuchanganyikiwa lakini ni muhimu daktari wako akufanyie uchunguzi tofauti iwapo wewe ama mtu unayemjali ana huu ugonjwa.

Ni zipi baadhi ya dalili zake?

 • Kupoteza kumbukizi kwa muda kwa kurudiaerudia swali moja mara kadhaa.
 • Shida katika kukumbuka maneno rahisi kama vile kusema “Kile kitu ninachotumia kuandikia” badala ya kusema “kalamu”
 • Kutotaka kufanya vitu ambayo kwa kawaida huwa unafurahia kurifanya.
 • Kufanya uamuzi usio stahili kama vile kuweka moto wa juu sana, kutembea muuani kukinyesha badala ya kujikinga kwa kutumia mwavuli, kusahau kula ama hata kumpatia mtu usiyemjua pesa nyingi, bila sababu yoyote.
 • Mabadiliko makubwa sana ya kitabia ya kuwa na hasira na huzuni.
 • Kuchanganyikiwa kutambua watu wa kitambo na wa kisasa.

Unatibuje hali hii?
Hapana matibabu ya ugonjwa huu. Hata hivyo ni muhimu uweke akili yako katika afya nzuri na changamfu. Tafuta utambue namna ya kufanya hivyo.
Iwapo wewe au mtu unayefahamu anaonyesha dalili zifuatazo pata ushauri wa daktari mara moja. Atakusaidia kutambua kinachousababisha.

Iwapo hali ya kimatibabu inasababisha hali hii, badilisha madawa na utumie yale ya vitamini. Ama kunywa vinywaji vingi ili hali hii isikidhoofishe. Iwapo hali ya Alzheimers inasababisha kusahau na kuchanganyikiwa, kuna aina ya dawa zinazoneza kupunguza hali hii.
 
Dhiki iletwayo na mshtuko


Ni hali ya kiakili inayotokana na kuishi maisha ya kuhatarisha nafsi ya mtu kama wanajeshi, matatizo ya kimazingira mashambulizi ya kiajali ya wahalifu ajali kubwa dhuluma za kijamii kwa mfano kupigwa na kunajisiwa.

Watu walio na shida hii huwa na ndoto za kutisha wanapokumbuka waliopitia wana shida za kupata usingizi wao hujihisi pweke na huoba kuwa wametengwa. Hali hii unaweza kudumu kwa muda mrefu kiasi kwamba itaathiri shughuli za maisha yake ya kila siku.

Ni nini baadhi ya dalili?


 • Epukana na hali ambapo utakumbuka mabaya yaliyotendeka kama mahali na vitu
 • Kumbukizi na mazingaombwe
 • Kuwa na hisia za kujulaumu hasa baada ya kueponea ajali au mkasa, hasa iwapo ni mtu mwingine aliyesababisha
 • Woga mwingi
 • Kutotuhe na kupata shida katika kuzingatia jambo
 • Kuhisi bubu kama vile hakuna lolote linalokujalisha ama kujiona hufai.
 • Kutofurahia shughuli ambazo hapo awali ulizifurahia
 • Kufikiria kila wakati kuhusu kilichotokea
 • Kumwa na kichwa, tumbo na kuona kizunguzungu
 • Kuzungumza kuhusu kujitia kitanzi au hata kujiumiza mwenyewe

Unatibuje hali hii?
Ugonjwa huu huweza kumshika mtu wa umri woyote hata watoto. Dalili huanza kwa muda miezi 3. Mtu huwa na usumbufu unaohusu kitendo alichotendewa. Wakati mwingine hakuna chochote ambacho hutendeka hadi miaka ya baadaye. Watu wengine hupona baada ya matibabu ya miezi sita huku wengine wakiumia kwa muda mrefu zaidi. Anayeugua, huhitaji nasaha bora madaktari au watoa nasaha wanaaza kukutafutia muhudumu wa kukusaidia. Iwapo anayeugua anafikiria kuhusu kujiua, daktari mara moja.
 
Hali ya Upweke


Ni hali inayoathiri namna mtu anavyofikiria kuhisi na hata anayotenda matendo yake. Mtu aliyeathiriwa na hali hii huwa na shida ya kutambua mambo ya kufikileko tu na yale ya maisha halisi. Huenda hata wasiitike wakiituwa na wana shida kusema namna wanavyohisi katika hafla za kufangamana.

Hali hii si nafsi moja au nyingi. Watu wengi wakiwa na hali hii huwa si wabaya wa kujiumiza au kuuwuza wengine. Haisababishwi hali aliyoipitia katika utoto, malezi mabaya na kukosa moyo wa kufanya mambo sababu haijajulikana haswa. Sababu inaweza kuwa ya kuuzithishwa katika familia, hali ya kizinaa na shida za kukosa kinga.
Kila mtu huwa na dalili zake za kipekee. Zinaweza kujitokeza polepole kwa muda wa miezi ama miaka ama hata itokee tu ghafula bila kutarajiwa. Ugonjwa huu huweza kuenda na kurudi.

Ni nini baadhi ya dalili zake?
Kusikia ama kuona vitu ambavyo haliko
Kuhisi kuwa unaangaliwa kila mara
Kuongea ama kusema vitu ambavyo havina maana. (Havieleweki)
Kutojishughulisha na mambo ambayo ni ya umuhimu sana
Kudidimia kimasomo au namna unavyofanya kazi
Kutojishughulisha na unadhifu au hata namana unavyofanana
Kutoonekana kabisa mahali ambapo watu wametengana
Maamuzi yasiyofaa, hasira, ama kuonyesha hisia za kuogopa wale unaowapenda
Kushindwa kulala au kizingatia kufanya jambo
Tabia zisizokubalika au za kiajabuajabu
Kushikilia sana dini au mambo yaliyokia kawaida
Imani ya uwongo kuhusu uwezo na nguvu zako au umuhimu wako
Imani kuwa mengine wanathibiti matendo yako

Unatibuje hali hii?
Wewe au mtu yeyote unayemjua aliye na dalili hizi kwa zaidi ya majuma mawili unaweza kupata msaada mara moja. Mpigie simu daktari, piga kwa hospitali ama kwenye kituo cha kutibu wenda wazimu matibabu ya mapema huashiria matokeo mazuri ya baadaye.

Hapana matinanu lakini mtu akipata tiba ibayostahili anaweza kuishi vizuri kama mtu wa kawaida. Hali hii hutibiwa kwa dawa na kufanyishwa mazoezi, pamoja kupewa nasaha bora, vijihusisha na vikundi vya kujisaidia na vituo vya kukusaidia pia.
 
Kukosa Utulivu


Hii ni hali ya mtoto kutotulia, kukosa makini au kufanya kitendo kimoja kwa fujo na vishindo.

Ni nini baadhi ya dalili?

Katika watoto

 • Husababisha makosa mengi yanayotokana na kutokuwa waangalifu

Shuleni na nyumbani.

 • Kutokuwa msikivu, mwangalifu ama hata kushindwa kufuata maagizo
 • Kutopanga shughuli vizuri
 • Kupoteza vitu kama vile madaftari vya kiada
 • Kuwa msahaulivu na kuzubazubaa kila mara (kuotea)
 • Kukosa kutulia kitini
 • Kushindwa kunyamaza
 • Kushindwa kusubiri zamu yako yake kutenda kitu

Watu wazima

 • Kuzuiliwa kuzingatia kitu kwa urahisi
 • Kukosa mpangilio
 • Usahaulifu
 • Kuahirisha kufanya mambo
 • Kuchelewa kila mara
 • Kulegea kila mara
 • Kuwa na majonzi na masikitiko
 • Kutojiona bora
 • Kuwa na mabadiliko ya hisia ya haraka haraka
 • Shida za kikazi kushindwa kumudu kazini
 • Kukosa utulivu
 • Kutumia minadarali ama kuwa na uraibu wa kitu.
 • Kuwa na shida za uhusiano
Unatibuje hali hii?
Watoto wengi na hata watu wazima wana hizi dalili na hivyo haimaanishi kuwa wana ADHD. Ni daktari tu anayeweza kuhakikisha akishafanya uchunguzi wa kina. Watoto walio na hali hii, kwa kawaida huonyesha hizi dalili kabla hawajatimia umri wa miaka saba na shida hii huwa inadumu kwa zaidi ya miezi sita. Iwapo unadhani kuwa wewe au mtoto wako ana hali hii muone daktari.
 
Kuyongayonga kwa hisia za furaha na huzuni


Hii ni hali ya kuwa na furaha sana na baada ya dakika chache unabadilika na kuwa na huzuni sana. (Bipolar disorder)
Mtu anayeugua kutokana na hali hii anaweza kuonyesha hisia za furaha sana (very high mania) ama za huzuni sana (depression). Ukipata tiba inayofaa, unaweza kuzuia hali hii.

Ni nini baadhi ya dalili?


 • Kukataa kukiri kwamba unashida kiakili
 • Kuwa na furaha iliyokithiri mipaka
 • Kuwa na huzuni uliokithiri
 • Tabia zisizo za kawaida
 • Kukasirika haraka hata kama jambo ni dogo
 • Kushindwa kushikilia jambo na kulimaliza
 • Tabia za kuhatarisha maisha
 • Kuwa na wasiwasi pasi na kutulia
 • Kutumia mvinyo mwingi
 • Shida za kupata usingizi

Utatibuje hali hii?
Nenda kwa daktari wako ili akutume kwa daktari anayetibu walio na shida ya akili. Unaweza kupewa madawa, nasaha, kushiriki katika vikundi vya kukutia nguvu na kufanya mazoezi. Ni daktari wa akili pekee anayeweza kuchunguza na kutambua iwapo mtu ana huu ugonjwa kasha autibu vizuri.
 
Majonzi na huzuni


Majonzi na huzuni ni nini?
Ni ugonjwa unaohusisha mwili, kupanda na kishuka kwa hisia za hasira na mawazo. Ni hali ambayo huwezi kuiondosha mbali kwani unashindwa kujizuia na hizi hisia.

Hakuna sababu moja kunayosababisha majonzi na huzuni mwingi. Hali hii hurithishwa katika historia ya familia. Hata wale ambao hii hali haijawahi kuonekana katika familia zao hujikuta nayo, taabu na dhiki za kupambana na maisha, mpenzi ama ugonjwa mkali. Watu wengine, hata madaktari, hudhani kuwa ni hali inayokumba tu watu wazee pekee la hasha.

Dalili

 • Kuhuzunika kila mara na kujiona bure
 • Kukosa shughuli na tama katika vitendo ulivyokuwa umenipenda hapo awali
 • Kuhisi kuchukizwa hata kwa jambo dogo
 • Kulia sana
 • Kuona hufai na kujihukumu huku ukijihurumia
 • Kulala sana ama hata kutolala kabisa
 • Kula sana au hata kuishindwa kabisa kula.
 • Kupata shida katika kufanya maamuzi au kufuatilia jambo
 • Kuwa na fikira za kutaka kujitia kitanzi au kufa.
 • Kulewa na kutumia dawa za kulevya.
Unaijuaje?
Ukihisi mojawapo ya dalili hizi kwa zaidi ya majuma mawili, ni muhimu upate usaidizi na kitaalamu. Huzuni ba majonzi huweza kutokea iwapo mtu ana shida ya kiafya, hasa kuna ugonjwa wa Sukari mwilini, ugonjwa wa moyo, kupata kipigo. Matibabu yanaweza kusababisha huzuni na majonzi pia. Ugonjwa wa kiakili na matumizi ya mihadarati, kupata nasaha bora na matibabu husaidia.

Unatibuje?
Iwapo kemikali katika ubongo wako hazitoshani unaweza kupata majonzi na huzuni kwa watu wengine, matibabu husaidia kwa wengine, nasaha bora huwasaidia. Kupata matibabu pamoja na nasaha bora huweza kutibu. Iwapo dawa au nasaha haisaidii endelea kujaribu hadi pale ambapo utapata tiba kamili. Watu tu baada ya majuma machache.
 
Majonzi na huzuni baada ya kujifungua


Hii ni hali gani?
Baada ya kupata mtoto kina mama wengi huathirika. Mwili hupitia mabadiliko mengi ya kupanda na kushuka kwa kiwango cha homoni. Wao huhisi majonzi huzuni na hawapati usingizi wa kutosha. Ni hali ya kawaida kuogopa, kuona umeshindwa, kuwa na hisia za huzuni/furaha kwa siku chache baada ya kujifungua. Hata hivyo mama wengine huhisi vibaya sana baada ya kujifungua. Hali hii husababisha kuumia kwa majuma au miezi iwapo hatatibiwa mara moja.

Ni nini baadhi ya dalili zake?
Unahitaji kukaguliwa na daktari ndipo atambue iwapo una huzuni na majonzi ya baada ya kujifungua. Wewe au rafiki yako mnaweza kugundua dalili za kuashiria hali hii. Tajiriba ya kila mwanamke ni ya kipekee. Hivyo basi usijilinganishe na mtu mwingine.

 • Kukosa furaha, kujiona bure na kuhisi kuwa huwezi kufanikiwa katika jambo lolote.
 • Uchovu, kuhisi bure, kuhuzunika ama kuwa na kilio tele.
 • Kuchanganyikiwa na kuwa na wasiwasi.
 • Uwoga wa kumuumiza mtoto
 • Uwoga wa kuwa peke yako ama kwenda nje kutembea
 • Kukosa hamu ya kufanya mambo ya kawaida ya kushirikiana
 • Kukosa kulala au kulala sana
 • Kuishiwa na nguvu
 • Kushindwa kujitunza (kujinadhifisha)
 • Kushindwa kutafakali vizuri ama kufanya maamuzi
 • Kuyaepuka majukumu yako yote na kukataa kuyashughulikia
 • Kuwa na woga wa kukataliwa na mpenzi wako.
 • Fikra za kumuumiza mtoto au wewe mwenyewe.

Unautibuje?
Muite daktari wako mara moja tu unapoona hizi dalili na unapitia mapwito ya mabadiliko ya kimaisha kama vile talaka, kutengana, kazi mpya, kuhama ama kufiwa na mtu unayempenda sana. Muone daktari wako iwapo huoni nafuu baada ya majuma mawili au ukianza kuwa na mawazo ya kijitia kitanzi ama kumjeruhi mtoto wako. Daktari anaweza kukupa matibabu na akusaidie kupata mshauri yanayo kufaa.

Marafiki na jamaa pia wanaweza kuwa wa manufaa kwako. Unaweza kuhitaji mtu wa kukutunzia mtoto wako huku nawe ukiwa na muda wa kujitunza. Usiogope kuitisha msaada wa kutunziwa mtoto ama kupata mtu wa kukufanyia kazi za nyumbani kwa kupika, kufua na kununua chakula.
 
Simanzi

Sikitiko ni kujumulisha pamoja uchungu wa akili, hisia nzito na hali ya kuchanganyikiwa inayotokana na mtu kumpoteza jamaa muhimu sana kwake. Unaomboleza na kusikitikia hali ya kumpoteza huyo jamaa hadi unajisikitikia. Kumpoteza mpendwa ama jamaa ni mojawapo ya hali ngumu sana maishani kukabiliana nayo. Kakuna atakayokuambia namna ya kusikitika. Ni hali ya kibinafsi sana anayopitia mtu.

Ni baadhi ya dalili hizi

 • Kushtuka na kushindwa kuongea.
 • Ugumu wa mkazo kwenye kufua na kooni
 • Kupata shida unapopumua
 • Kukosa nguvu
 • Kushindwa kula ama kulala

Namna ya kutibu
Nenda ukamuone daktari. Anaweza kukutanisha ba vikundi vya kukuhimiza ba kukutia nguvu. Atakupa mwongozo na wosia na matibabu. Hapa pana hoja ya kukumbuka iwapo unaomboliza;

 • Ni vyema kulia, kupiga nduru, kukaa peke yako kwa muda, ama kupandwa na hasira. Ukiwa katika hali hii kwa zaidi ya mwezi mmoja, kuna uwezekano, kuwa umeshtuka na kuwa mdhoofu.
 • Mambo huja yakawa mazuri baadaye mwanzoni huenda yasionekana kuwa kweli. Kuendelea na maisha hakumanishi eti umsahau kabisa mpendwa wako inamaanisha tu kuwa unapona. Usijihukumu unaoanza tena kujenga maisha yao.
 • Jitunze. Hakikisha kuwa unakula na kupumzika vya kutosha. Gharamila upishi, malipo ya maji na stima kusafisha na kufua. Hukuchukua muda kwa mtu kuzoea kujifanyia mambo.
 • Zungumza kuhusu hasara iliuokupata marafiki na familia wanaweza kukusaidia usiogope kuongea na mtu wa mbali kidogo kuhusu namna unavyohisi.
 • Usitumie vileo na dawa kusikia vyema. Iwapo tayari unatunia ni muhimu utafute msaada wa kitaalamu. Haikosi huenda unaugua kutokana na majonzi na huzuni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom