Matatizo ya automatic gearbox

teac kapex

JF-Expert Member
Jan 23, 2011
470
136
Mimi nina gari lenye auto gear box, lakini lasumbua sana sijui tatizo nini, mara ya kwanza nilipoiweka baada ya kuiondoa ile iliyokuwepo ilikua inabadilisha gia bila shida kwa sasa ina kama km 700 imegoma kbadili gia kama mwanzo hasa inapokuwa imepoa, ninapoanza kuondoka hunilazimu kwenda na gia moja kwa umbali kama mita 800 hivi ndo inabadili na ikfanikiwa kubadili haisumbui kwa namba 3 na kuendelea ss tatizo litakuwa ni nini?
 
Au ni mimi ndo nitakuwa sijakuelewa. Gari yako ni automatic lakini hapa nadhani unaongelea manual. Au automatic nayo ya gear 1,2,3...? Pole sana na tatizo hilo mkuu, waone mafundi, watakusaidia vizuri japo itategemea uko wapi!
 
Angalia level ya transimition fluid (gear box oil). Normailly ikishuka ni tatizo na ikizidi pia ni tatizo

Tafuta fundi mzuri anayejua kupima kiwango kinachotakiwa, in most cases hata mafundi walio wengi wa uswahilini hawajui hii kitu sawasawa.

Pia kuwa makini na aina ya fluid unayotumia, nyingine (most of cheap prices) ni fake hazifanyi kazi ipasavyo au unaweza kuta mmeweka fluid ambayo si ATF

Mimi nimepitia matatizo mengi ya aina hiyo mpaka sasa nimekua mtaalam
 
Au ni mimi ndo nitakuwa sijakuelewa. Gari yako ni automatic lakini hapa nadhani unaongelea manual. Au automatic nayo ya gear 1,2,3...? Pole sana na tatizo hilo mkuu, waone mafundi, watakusaidia vizuri japo itategemea uko wapi!

inategemea na aina ya gari....european nyingi zina P R 1 2 3 4 D....ukiweka 4 gear zinabadilika automatic hadi 4,ukiweka 3 zinaishia 3 etc....ukiweka D zinakwenda hadi 6 kutegemea na gari yako ina gear ngapi.....pia kuna gari zina option ya semi automatic-mistakenely called manual.....kama umeona kwenye gear lever alama za + na - unaweza kushift up and down manually by puhshing the gear lever up or down
 
Mimi nina gari lenye auto gear box, lakini lasumbua sana sijui tatizo nini, mara ya kwanza nilipoiweka baada ya kuiondoa ile iliyokuwepo ilikua inabadilisha gia bila shida kwa sasa ina kama km 700 imegoma kbadili gia kama mwanzo hasa inapokuwa imepoa, ninapoanza kuondoka hunilazimu kwenda na gia moja kwa umbali kama mita 800 hivi ndo inabadili na ikfanikiwa kubadili haisumbui kwa namba 3 na kuendelea ss tatizo litakuwa ni nini?
Nina gari mark2, tatizo kwenye kuondoka, ukisha weka D,inakuchukua kama dk 3 hivi ndininaanza kumove hasa asubuhi au ukipaki muda mrefu,ila ukitoka tu ina changanya vizuri nini tatizo?
 
Pamoja

Mleta mada ili usaidike vizuri...taja kampuni ya gari mfano Toyota, Model mfano IST, mwaka mfano 2004....hapo utasaidika kirahisi..

Lakini swala lingine isijekuta gearbox ni CVT wewe ukaweka ATF za uswahilini......hapo utacheza sana..
 
Mimi nina gari lenye auto gear box, lakini lasumbua sana sijui tatizo nini, mara ya kwanza nilipoiweka baada ya kuiondoa ile iliyokuwepo ilikua inabadilisha gia bila shida kwa sasa ina kama km 700 imegoma kbadili gia kama mwanzo hasa inapokuwa imepoa, ninapoanza kuondoka hunilazimu kwenda na gia moja kwa umbali kama mita 800 hivi ndo inabadili na ikfanikiwa kubadili haisumbui kwa namba 3 na kuendelea ss tatizo litakuwa ni nini?
Umeme hauko sawa kwenye gari yako. Kuna kitu kimoja kinaitwa "Control Box" hiki kifaa kipo kama kibox flani kinachoendesha mifumo ya umeme wa gari hasa Giabox.. hata mimi niliwah kuwa na ttz hilo kwenye Aice yangu nikabadili gearbox 2 na zote zipo nyumbani kwangu.. ila baadae nilihisi kwamb ni umeme, Nikapeleka wakatengeneza wakapima umeme wote kwenye gari, pamj na hy control box ikaonekana ina hitilafu ilipopona gari iliendelea kupiga kazi kama kawaida na sasa ina km 300,000 na.
 
Mkuu we nenda kwa fundi afungue sampo ya gearbox asafishe strainer aisafishe, shida unaisahau kabisa.
 
Nina gari mark2, tatizo kwenye kuondoka, ukisha weka D,inakuchukua kama dk 3 hivi ndininaanza kumove hasa asubuhi au ukipaki muda mrefu,ila ukitoka tu ina changanya vizuri nini tatizo?
Badili Hydrolic ya gearbox na pia safisha strainer
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom