Matatizo tumeishayapatia ufumbuz au na sisi ni sehemu ya matatizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo tumeishayapatia ufumbuz au na sisi ni sehemu ya matatizo?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by CHASHA FARMING, Mar 14, 2012.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  GREAT THINKER VIPI HAYA MATATIZO TUMEISHA YAPATIA UFUMBUZI? AU NA SISI NI SEHEMU YA MATATIZO?

  Hili jukwa limekuwa na Watu wanatoa michango mbalimbali na watu wanakuja na Aidea zilizo enda shule na kuna watu ambao kupitia jamii forum wameisha anza miradi yao na wengine wako kwenye PROCESS.
  -KUNA MATATIZO MENGI SANA YANAYO KABIRI SECTA NYINGI SANA HAPA TANZANIA NA BAADHI YA SEKITA HIZO NI

  1. Kilimo
  - Hapa kuna matatizo mengi sana kama vile

  a. Upatikanaji wa pembejeo

  b. Elimu bora ya kilimo

  3. Mitaji ya kuwekeza kwenye kilimo

  4. Masoko ya mazao ya kilimo

  5. Uongezaji wa thamani wa mazao yetu/kusindika  A. UPATIKANAJI WA PEMBEJEO

  Hili ni tatizo kubwa sana na wakulima wengi wanashindwa kumudu au kupa pembejeo za kilimo kama vile, mbolea, madawa, matrecta, vifaa vya kuvunia na kuhifadhia mazao na kadhalika

  - Serikali imekuwa inaiimba sana kuhusu hili, na mpaka sasa hakuna suluhisho lilio patikana make kuna matrekta still yanauzwa bei kubwa sana na mbo;ea ndo usiseme kabisa, na nchi yetu ni ya wakulima

  SWALI KWA GREAT
  1. Je ni wangapi sisi tumegenerate aidea ya kutatua Taizo hili la pembejeo hasa, mbolea na matrekata. pamoja na madawa ya kilimo?

  2. Je tumeisha pata suluhisho la angalau kupunguza haya matatizo? au na sisi ni sehemu ya kulaumu Serikali kwamba ifanye hivyo?

  B. ELIMU YA KILIMO BORA

  Hili nalo ni Tatizo kubwa sana na kuna Vyuo vya kutoa elimu ya Kilimo Bora ila ni wachache wanao weza pata elimu na lazima uwe na pesa za kutosha kuweza kupata elimu hii, na kwa walio vijijini ni shida zaidi,

  SWALI
  1. Je tumeisha kuja na wazo la kutatua tatizo hili ka Elimu ya Kilimo cha biashara?

  2. Au na sisi tumejiunga kulalamikia serikali kwamba hakuna Elimu ya kutosha kuhusu kilimo Bora?

  C. MITAJI YA KUWEKEZA KWENYE KILIMO
  Hili laweza kuwa Tatizo kuu kabisa, watu wengi tunashindwa kulima kwa sababu ya mitaji, huko vijijini watu wanamashamba ekari na ekeari lakini wanashindwa kulima kwa sababu ya kukosa mitaji ya kuwekeza huko.

  - Benki zetu nd tusha piga kelele hadi tukachoka, Serikali mpaka leo na kesho haina majibu ya wpai watu wapate mitaji ya kuwekeza kwenye kilimo

  - Hata mitaji ikipatikana nina uhakika haitatoshereza kwani watanzania wanao hitaji mikopo ya kilimo ni wengi sana

  SWALI HAPA

  1. Je tumeisha kuja na mbinu mbadala kama wasomi wa Nchi hii kumaliza kutatua Tatizo la Mitaji ya Kilimo hapa Tanzania?

  2. Kuna walio kuja na wazo hilo?atujuze basi wamefikia wapi,

  3. Au na sisi ni sehemu ya kuto jua nini kifanyike? Na sisi tuko kundi la kusubiria siku isiyo julikana ambayo serikali italeta mikopo?

  D. MASOKO YA MAZAO YA KILIMO

  - Tumekuwa tukishuhudia mahindi, pamba, kahawa, Maharage, Ndizi, Vitunguu, Mchele, Matunda na kazalika vikikosa masoko na kuishia kuozea chini au mazo hayo yakiuzwa kwa hasara kubwa sana

  - Mahindi yamekuwa yakipelekwa Kenya na kenya wao wanasindika na kuza nchi za nje na hata kuuzia mashirika ya Misaada.

  - Na tumekuwa tukijisifu sana kwa kuuza mahindi kenya, inagawa ukweli ni kwamba pale hatufaidi choacote

  - Mazo ya biashara hayana masoko kabisa, tunabaki kuashumu kwamba ngoja tulime tu watakuja kununua, tumebakia kupeana noyo kwamba mwakani bei itakuwa nzuri bila hata kuwa na mikataba na hao wa nunuzi, je wakikataa kununua hayo mazao itakuwaje?

  - Matunda hayana masoko kabisa, kule Tanga machungwa hufikia kuuzwa ka mafungu, Kule Tabora maembe huishia kuozea kwenye miti, Ndizi kule Bukoba, Mbeya na Arusha na Kilimanjaro ni hivyo hivyo.

  - Mpaka sasa hakuna masoko ya uhakika zaidi ya wahun wano kuja mitaani na kuwaibia wakulima kwa kununua kwa bei ya chini kabisa,

  - Na hata kama wapo si wauhakika ni wanao kuja leo na kesho wanapotea,

  - Serikali bado inaendeleza Sarakasi zake tu, hakuna suluhisho la hili zaidi ya kuwepo Bodi za Mazao kama Pamba, Hizi Bodi hupanga bei kana kwamba wao ndo walikuwa wanalima sasa wanajua ghalama alizotumia mkulima

  SWALI

  1. Je mpaka sasa kuna tulio kuja na suluhisho la haya matatizo makubwa kabisa ya masoko?

  2. Tusha kuja na mawazo ya kutatua matatizo ya masoko ya kilimo

  3. Au na sisi ni miongoni mwa tusio jua tutauza wapi ila tunapeana moyo tu kwamba wanunuzi watapatikana?

  E. KUONGEZA THAMANI/KUSINDIKA

  - Asilimia 60 ya matatizo ya kilmo chetu yanaweza malizwa na hapa kwenye kusindika

  1, Masoko hakuna kwa sababu hatusindiki mazo yetu

  2. Tunashindwa kulima kisasa kwa sababu hatujui tuuze wapi mazo yetu na tusha kata tamaa ya kulima ila tungekuwa tunasindika ingekuwa simple sana

  - Hapa ndo shida kuu ya Kilimo cha Watanzania ilipo


  a. ,MAHINDI- Hapa tunategemea viwanda visivyo pungua 4 visindike mazo ya mahindi, wakati nchi ambzao hazina mashamba mengi kama sisi kuna viwanda vya kutosha
  - Hapa ni lazima mahindi yaoze kule Songea kwa sababu hatuna viwanda vya kusindika na kuongeza thamani.

  - Tunawauzia wakenya wasindike mahindi na warudi kutuuzia, unga na pumba

  - Kuna kampuni moja huku Arusha ni ya kutoka kenya wanauza Pumba za ngombe na kuku na ukijaribu
  kuchunguza walinunua mahindi hukuhuku kwetu na kuyasindika na kuridi kutuuzia pumba kwa bei ghali

  - Sisi tunaona sifa sana kuuza malighafi nje ya nchi theni inarudishwa kama bidhaa tena kwa bei ya juu sana

  b. Matunda
  - Hapa hatuongezi thamani na badala yake kule Tanga Fuso zinatoka kenya zinaingia shambani zinachuma na kupeleka kenya kusindika theni wanakuja kutuuzi juice tena ile freshi inauzwa mbali sana sisi tunauziwa frever tu

  Huwa tunafurahi sana kuuza matunda kwenye fuso, hapa kipimo si mizani tena kipimo ni FUSO MPAKA IJAE
  KWA KIFUPI TUNAPOTEZA PESA NYINGI SANA KWA KUUZA MALIGHAFI NJE WAKUU, NA NCHI KAMA CHINA IMEPIGA HATUA SI KWA KUUZA MALIGHAFI BALI BIDHAA

  MASWALI HAPA
  1; Je tumeisha kuja na mawazo ya kumaliza kabisa hili tatizo?

  2. Tumeisha anzisha viwanda vya kusindika ili tuwakomboe watanzania wengi wanao lima na hata kuwapa ajira wengine?

  3. Au na sisi hatujui tufanyeje na badala yake tunajiandaa kuuza mahindi kenya pamoja na machungwa kweny fuso?

  4. Tunasubiria serikali itujengee viwanda vya kusindika mazao? Je kuna mwenye taarifa ni lini wataanza kejenga?

  WAKUU KWA KIFUPI NI KWAMBA KWA KWELI TUNACHEZA SANA NA BILA MAPINDUZI TUTAKUWA NA SISI NI SEHEMU YAMATATIZO YA WAKULIMA WENGI SANA.

  HUWA NAPITIA SANA FORUM ZA WAJASIRIMALI ZA NCHI NYINGI SANA KAMA INDIA, PHILIPINE, MALASIA, INDONESI, NIGERIA, GHANA,SOUTH AFRICA NA KAZALIKA, HAWA JAMAA MAWAZO YAO SI YA MCHEZO KABISA WAKO SIRIAZI 100%

  SISI HUKU HATUKO SIRIAZI KABISA UTANI NA MIZAHA NI MINGI SANA, WATU TUNAKUJA NA AIDEA AMBAZO KWA KWELI HAZIWEZI KULIKOMBOA TAIFA BALI KUMKOMBOA MTU MMOJA TU,

  TUNAHITAJI MAPINDUZI MAKUBWA NA NI BORA TUKAANZA SISI KUFANYA MAPINDUZI MAKUBWA NA YANAYO ONEKANA KWA MACHO NA SI MAPUNDUZI YA POROJO WAKUU

  TUSIWE SEHEMU YA KULALAMIKA KWA SABABU VIJANA WA NCHI ZINGINE WALISHA ONA HATA WAKILIA HAITASAIDIA KITU BALI NI WAO KUINGIA NA KUFAITI KIVYAO, SERIKALI INAMAMBO MENGI SANA WAKUU,
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Ndugu, mapinduzi gani unayoyaongelea? Au, nawe unacheza?

  ...Kimsingi, sisi hatuwezi kuwa sehemu ya matatizo ya wakulima. Humu watu hubadilishana mawazo, kutoa maoni na ushauri, na wengine hukalia utani, masihara, uzushi, n.k. Hiki si chombo cha kutatua matatizo ya wakulima, au, kwa maana hiyo Watanzania. Vyombo hivyo vipo, na natumai unavifahamu. Nakukumbusha -pengine umesahau- hii ni jukwaa ya maoni na kubadilishana mawazo.
  ...Pata muda upitie vizuri hapa, nadhani utagundua kuwa kuna mawazo ambayo si ya mchezo na wako watu "siriazi" 120%.
  ...Hujapitia hizo "aidea" vizuri. Pata muda, soma kwenye baraza la siasa na lile la uchumi. Na kama kuna mapungufu changia kuboresha maoni hayo.

  ...Halafu, usisahau kwamba hii nchi haina utamaduni wa kusaka na kutumia professional advice. Bila kusahau waamuzi wengi hawashughuliki kusoma taarifa za wataalamu kwa kina, ili wafanye maamuzi sahihi. All the best!
  ...Mapinduzi yapi unayoongelea? Kwa mtu aliyepita hapa na kugundua kuwa hakuna la maana, bali porojo, ulitakiwa kuwa very articulated with what you are talking about.
  ...Vijana wasilalamike? Wakifaiti kivyao watajumuisha na mambo gani katika mchakato huo wa kufaiti kivyao? Kama hamna umeme unafaiti vipi kivyako, nawe hauna uwezo wa kununua generator, achilia mbali mafuta? Yule wa Tunisia alifaiti kivyake na kuuza matunda. What happened to him? Unataka wafaiti kihivyo?. Usiwe na wasi, wahenga walisema...."ngoma ikilia sana, hatimae......."
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  1. Hili si jukwaa la maoni pekee, ni sehemu ya kuja na mbunu mbadala, kwa hiyo mwisho wa haya maoni ni nini?

  Je ni nani anayafanyia kazi unayo ita maoni? Ni serikali?

  2. Mkuu sijasema hakuna mawazo mazuri yapo tena kuloko hata vyuoni, Tatizo ni kwamba yamefanyiwa kazi kaisi gani? je tukifanya tathimini yetu tutapata changes?

  - Kwa hiyo wewe tuambie unaye taka afanyie kazi haya ni nani au tubakie kwenye theory pekee?

  3. Hizo adivice inatakiwa nani azifanyie kazi? kwani serikali inafanya biashara? Serikali ndo unataka ikuambie ujenge kiwanda?
  - Ili ufungue miradi ni mpaka serikali ihamasishe?
  - Je nchi kama Chi zingine wanafanyaje? serikali zao ndo zinaenda kuwaambia waanzishe miradi?

  4. Porojo unazifahamu wewe na usikute naongea na Mfanyakazi ambae yeye vitu kama hivi unaona ni porojo wewe subiria mwisho wa mwezi,

  Kwa hiyo unaona tusha fanya mapinduzi kwenye kilimo? kwenye ufugaji? kwenye utalii?

  5.Hata hivyo hawatakiwi kufaiti wote ni lazima wajasirimali wachache wapatikane na wengine tubakie wafanya kazi wao, na wale tunao lia lia sana ndo tutakao ajiriwa, niko huku Arusha kuna Vijana wakenya wanaingia kila kukicha na kuanzisha kapmpuni zao moja kwa moja wakitikoa vyuoni na si kwamba wamekopeshwa na Serikali yao ila ni wao wenyewe wamepambana, Ok sisi basi tufanye hivi tuendelee lulalamika halafu waje wakenya wafungue kampuni zao huku tuwafanyie kazi

  TUTALALAMIKA SANA NA SIKU SERIKALI ITAKAPO SIKIA KILIO CHETU HAKUTAKUWA NA MUDA TENA MKUU, WEWE IMAGINE TUKAE TUSUBIRI SERIKALI ILEKEBISHE SERA ZAKE MY BE MIAKA 10 IJAYO TUKIWA TUMEKAA TU?

  - NI LAZIMA TUPAMABNE KWENYE HIZI HIZI POLICY MBAYA TULIZO NAZO HATA NCHI ZENYE VITA STILL WANAFANYA BIASHARA PAMOJA NA USALAMA KUWA HAFIFU

  - WEWE HAIKUUMI WANAVYO KUJA WAHINDI KUTOKA INDIA NA KUANZA CIHINI NA MWISHO WA SIKU WANAKUJA KUTUAJIRI? JE WAKENYA WANAO WEKEZA KWA KAZI KWETU? TENA WENGINE VIJANA WALIOMALIZA CHUO TU NA HAWANA MITAJI MIKUBWA.
   
 4. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Binafsi nakupongeza sana kuongelea hili. Jana na leo nimekuwa kwenye mku5 ambapo Mh Maghembe ni mwenyekiti...kikao cha watendaji, but kikao kinahusisha wakuu wa mikoa, wakurungezi halmashauri, watafiti na maafisa ngazi ya taifa na maafisa ugani. Kwa bahati mbaya kabisa, kikao kimejikita kujadili changamoto kwenye uzalishaji, mbegu, umwagiliaji masoko.Lakini suala la ajabu hakuna watu wa makampuni binafsi ambao ndo washiriki wakubwa. Ningependa kuchangia mjadala huu kwa ufasaha sometimes kesho au kesho kutwa kwa kuwa ninajua wakati huo nitakuwa na mda wa kutosha. Lakini itoshe kusema kuwa kilimo hakiwezi kufanikiwa endapo tunadhani serikali pekee ndo yenye jukumu la kuendeleza kilimo na kukiwezesha kuchangia kuondoa umasikini. Mfano mzuri ni wakulima wa korosho mwaka huu hawana soko...simply because makampuni yamegoma kununua korosho kutokana na utaratibu mbaya wa minada na vibari. Wakulima Lindi na Mtwara wanajiuliza nani wamwuzie korosho? Tar 1March 2012 Mh Kikwete alimwambia waziri Maghembe kufuta vibari kwa makampuni ambayo hajakubali kununua korosho, lakini wakati huo huo serikali haijadili mchango wake kudidimiza kilimo. Itoshe kusema kuwa mazingira mazuri huwavutia wafanyabiashara (wadogo na wakubwa) na hivyo kuongeza ajira, na kilimo ni sekta muhimu katika hilo, lazima mazingira mazuri ya kisera na kiutawala (governance) yawekwe ili kilimo kifanikiwe
   
 5. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Utajifunza, tena taratibu na utaelewa vizuri tu, mambo yanavyoenda. Labda nikuulize wewe unayejua kuhusu mapinduzi -maana, swali lako linaonyesha unayajua- kwa undani. Nani analeta mapinduzi kwenye kilimo, ufugaji na utalii?. Kwa ufahamu wako, unafikiri kuna nchi inayoweza kuwa na mapinduzi katika kilimo bila mkono wa serikali?. Unafahamu ni kiasi gani nchi za Ulaya na Marekani zinatoa kama ruzuku kwenye sekta hizo kwao?. Je, unafahamu kwanini Doha Round is a waste of time, especially to developing countries?
  ...Umeshawahi kukaa chini, wewe na macharlie wenzako, mkajiuliza hao Wakenya kwanini wanafungua kampuni zao, na kama wanafanikiwa. Mmejiuliza wao wana ujuzi upi na wanatoa huduma kwa nani? Je ni biashara zenye uhusiano na Wakenya wenzao au ni zile zinazohusika na bidhaa toka Kenya?
  ...Mkao huo ni upi? ule wa kupiga stori na kupata ganja au? kama ni huo, miaka 10 itawakutia jela au hapo hapo.
  ...Kijana, nani kakwambia hapa watu hawafanyi biashara au kuzalisha mali? Hao Wakenya uliowataja? Na umewasahau Wachina pia, tena hawa ndio tusipoangalia, waitainunua Tanzania yote. Unafahamu hilo?
  ...Acha ubaguzi usio na maana wala msingi. Unafahamu kuwa Wahindi wapo nchi hii kabla hata ya kuzaliwa kwa wazazi wetu, mimi na wewe. Kwa ufupi ni raia. Halafu, hao wote wanaokuja huku, hawaji kupata hasara. Wanakuja tengeneza pesa.

  ...Unafahamu makampuni ya Kenya yametoa ajira kwa vijana wangapi wa Kitanzania? Labda, tutaje KCB, Equity Bank Na Uchumi kwa kuanzia.

  ...Acha kulalamika, tulia, fikiria na chukua hatua.
   
 6. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Bube, hicho kikao ni cha ndani au cha wadau wote?. Maana, usikute inabidi mjipange kama serikali, kabla hamjashirikisha watu binafsi kama wakulima, vyama vya ushirika, makampuni ya madawa na mbegu, wanunuzi wa mazao, n.k.
  ...Ni kweli kabisa, serikali pekee haiwezi kuleta maendeleo kwenye kilimo. Na hii yetu, imekuwa inarudisha nyuma maendeleo ya kilimo bila kujua, hasa pale inapoingilia nguvu na utaratibu wa soko, ili kufurahisha wakulima au walaji.
  ...Tunategemea walipofanya hivyo walikuwa na soko mbadala la korosho hizo. Kama hali si hiyo, basi ni kiama kwa wakulima huko.
  ...Haiwezi kujikosoa, kwani hakuna utaratibu huo Afrika.
  ...Na hapa ndipo serikali inabidi kushika hatamu, kwa kushirikiana na wadau.
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu makampuni ya ununuzi ndo moja ya watu wanao didimiza kilimo huku Tanzania na ndo maana nasema ni lazima tuje na mbinu mbadala za kuweza kumaliza hili Tatizo, hatuwezi endelea kuwategemea wanunuzi ambao wanakuja na bei zao

  - Vyama vya ushirika ndo vinaongoza kwa kudidimiza kilimo na bado si suluhisho kabisa kwani ndo wameua kilimo na hatuwezi endelea kutegemea vyama vya ushirika, make viko kisiasa sana, na wakati wake ulisha pita

   
 8. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu, topic hii ni pana sana, nadhani kila changamoto uliyoizungumzia inahitaji thread yake ili ijadiliwe kwa mapana yake na wadau kwa ufasaha zaidi. Kiujumla nionavyo mimi, matatizo mengi tulianza kuyapatia ufumbuzi halafu tukapotea njia kutokana na mifumo ya kuletewa tuliyo amua kuimbatia, (either kwa kujua au bila kujua). Na hapa naomba niazime maneno ya Jenerali Ulimwengu anapozungumzia falsafa inayomtaka mama kuku awaache vifaranga wake watembee wanavyotaka ili kuwapa nguvu na uzoefu wa kujitegemea kwani hii ni falsafa inayohubiriwa na Mwewe.

  Hebu fikiria wakati sisi tunahubiriwa kuwa Serikali zetu ijitoe kwenye Biashara na kubinafsisha state owned enterprise, hao hao wanatuhuburia (Mwewe) Serikali zao zinakuwa na hisa kwenye makampuni makubwa (na mengine operation zao zipo Tanzania kwa sasa)Sasa naomba turudi kwenye topic na kwa ridhaa yako nitaanza na mifano iliyokaa katika mfumo wa maswali1. Hebu tuchukulie mfano wa Zao la Katani, hivi hatukuwa na soko lake hapo awali? Hivi soko lake la ndani (vile viwanda) vilikuwa vinanunua asilimia ngapi ya Katani tuliyokuwa tunalima? Je hali ya wakulima wa katani ilikuwaje kipindi cha nyuma, ukilinganisha na sasa? Najua umezungumzia na pembejeo. Hebu nikumbushe machine tools pale Kilimanjaro walikuwa wanajihusisha na nini? na leo hali ikoje? Hivi unajua kuwa walikuja wageni kutoka Asia kujifunza Tanzania juu ya zao hili. Leo hii wakati Zitto anataka kulizungumzia hili kupitia HOJA yake Binafsi, Bunge letu halioni umuhimu!

  2. Au labda tuache hili zao la katani, twende kwenye pamba. (Mmh huku ndio kubaya zaidi, kwani ukifika tu Dar es Salaam eneo la Urafiki utaona namna majengo ya iliyokuwa kiwanda cha urafiki yanavyotoa machozi). Ruzuku ilikuwepo, maafisa ugani, pembejeo, masoko (viwanda), na bado tulianza kutengeneza nyuzi badala ya kuuza pamba ghafi? leo hali ikoje?

  Kwa kweli hata sisi ni sehemu ya tatizo kwani wengi wetu tumekaa tukitegemea serikali itatufanyia kila kitu. Na wengi wetu tumeridhika na matendo haya ya Serikali ndio maana tunairudisha madarakani katika kila uchaguzi. Kiujumla kila mmoja wetu anawajibu wake wa kutimiza, lakini serikali yetu ina wajibu mpana zaidi hasa ikizingatiwa kuwa wao ndio waliotupoteza njia. Ni vyema wakati tunaishauri au kuishinikiza serikali kurudi katika njia sahihi (au wakati tunasubiri kuipumzisha), na sisi tutimize majukumu yetu especialy yale yaliyo katika uwezo wetu kwani serikali zetu haziwezi zikatufanyia kila kitu.

  Ukiniuliza mimi, ni njia ipi iliyo sahihi nitakuambia Guided Economy & Guided Democracy, na ndipo tulipopotea kama Taifa kwa kukumbatia sera za WB, WTO & IMF ambazo mpaka leo bado hazijatukomboa
   
 9. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,507
  Likes Received: 6,008
  Trophy Points: 280
  mkuu chasha umeongea kitu kizuri,ila naogopa hata kuchangia sababu mawazo yangu mengine ni ushauri kwa hii serikali kiziwi hivyo naweza kuonekana bado nalalamika anyway nianze hivi.
  1. kuhusu elimu ya kilimo naona TBC huwa wanavipindi vya kilimo japo huwa na doubt kama wanamaanisha, pia nashangaa nchi ya wakulima haina gazeti linalo husu kilimo! ningeona waanzishe gazeti la kilimo walau once per week, information zilizoandikwa zinaeffect kuliko za tv na redio
  2.kuhusu mitaji ya kilimo naona watu mnaweza mkajikusanya kwenye vikundi vya watu wenye mitaji kama watu 2,3,4, 10 hadi 100 na mkachanga labda laki tano na kuendelea na mkatafuta mradi ambao ni feasible kwa hela yenu cha muhimu muwe na sheria zinazoeleweka na watu wasiegemee sana kwenye mradi kama source ya mapato especially siku za mwanzo
  3.kuhusu masoko naona ndani soko ni dogo sana ukilinganisha na potential tuliyonayo kwenye sekta ya kilimo, hapa tatizo wapanga sera, tukianza na kilimo cha mazao ya chakula, serikali imeweka vikwazo ku export haya mazao hivyo wakulima kuuza ndani kwa bei ndogo kitu ambacho kinawakatisha tamaa watu kulima hasa wale wenye mitaji mikubwa kwa mtindo huo uzalishaji wa chakula unapungua na badala ya kuzuia njaa tutajikuta tunaleta njaa, cha kufanyika ni kumuacha mkulima auze atakako hilo linaweza kumuongezea kipato hata akaweza kusindika, wengi watavutiwa kulima, pia wawekezaji wa ndani watavutika kufungua viwanda vya kusindika kwa sababu ya upana wa soko jamaa wanasema tuwe bread basket but they dont mean
  NOTE: ku work hard kunahusisha kuthink hard, tukiwork hard tutawaajiri watu kama DAR si LAMU! jina lenyewe linaonyesha mtu mwenye mawazo hasi
   
 10. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu safi sana nimependa sana hii,

  1 kwenye mitaji, ni kweli kabisa si kwamba Tatizo letu ni mitaji no tatizo ni kwamba kila mtu anataka aonekane anafanya biashara yeye kama yeye, kuna wakenya fulani huku arusha wana kampuni yao ya IT na nilijaribu kuongea nao walipata wapi mtaji wakaniambia walijiunga watano na wakaunganisha nguvu ndo wamefungua kampuni ya IT,

  Huko Bongo ni Tofauti kabisa kila mtu anataka awe na Basi lake, kila mtu anataka awe na min supermarket yake na kwa ushindani uliopo na unaokuja tutakuja kufunga biashara tupende tusipende

  - Inawezekana kabisa kuunganisha nguvu tatizo ni kwamba kila mtu anataka aonekane kwa ndugu zake na marafiki zake kwamba anafanya biashara yeye kama yeye


  2. Yapu kwa kweli we need kuunganisha nguvu kwa kila nyanja, Bila kuunganisha nguvu tutabakia kulaumu serikali milele, ok tutalaumu serikali, je Siku ikisikia kilio chetu labuda baada ya miaka 9 ndo tuanze kazi? tutaweza kushindana kweli?

  Ni bora tukaanza kwa mazingira haya haya magumu ili yatakapo boreshwa yatukute na si tusubirie yaboreshwe
   
 11. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu, hoja yako ni nzuri but ngoja nikuchallenge kidogo kwa kufuata mfumo wa namba kama ulivyotumia
  1. Hoja ya kuwa na Gazeti la Kilimo. Hii ni hoja nzuri lakin wewe unavyoizungumzia, ni kama ni wajibu wa serikali kufanya hivyo. Kwani private sector kama wewe na mimi hatuwezi kuichukua hii kama business Opportunity na kuifanyia kazi? Hasa ikizingatiwa kuwa Tayari Serikali imeshaonyea nia kubwa zaidi ya kuwa na Benki ya Kilimo

  2. Hoja ya kuunganisha nguvu, ninaikubali na ninaiunga mkono pia, (ukifuatilia post alizoanzisha malila kipindi fulani zilikuwa zinahamasisha wadau waungane nae ili wakaanzishe miradi ya kilimo na ufugaji na ninadhani amefanikiwa kwa hilo).

  Lakini kabla sijaenda mbali zaidi, naomba niulize swali. Hivi model hii ya kuunganisha nguvu haikuwahi kutumika kipindi cha nyuma? (Rejea, Vyama vya ushirika). Je ni kitu gani kiliua vyama hivi? Mbona tulikuwa na vyama vya ushirika vyenye nguvu na sasa vimekufa. Nauliza haya, ili watu wajue tulijikwa wapi na kuchukua hatua muafaka kwani bila ya hivyo hata hizi juhudi tulizonazo za kuanzisha SACCOS zitapotelea gizani kwa kiwango kikubwa
   
 12. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kikao hili inaelekea kilikuwa cha ndani. ila sasa hata kuelezea ndani nashindwa. Kuna wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi halmashauri kama nilivyoeleza hapo kwanza. Kwa hiyo ningetegemea kuwa kilimo ambacho mchango wake kwa GDP umeshuka kutoka 50% to 24% (mwaka 2010) kingepewa mikakati jinsi gani kifufuliwe. Ni ukweli usiopingika kuwa 65% ya ajira inatoka kilimo, na vijijini ni 80%, vile vile zaidi ya 95% ya chakula huzalishwa hapa, na hususani wakulima wadogo ambao ni masikini. Kwa bahati mbaya umasikini kwetu Tz unasura ya vijijini. Hivyo basi, kuendeleza kilimo ni kuondoa umasikini na uhaba wa chakula ni kufikia malengo ya mkukuta na milenia. Bahati mbaya jitihada za kuleta mafanikio zimekuwa za kisiasa zaidi. Mfano, bajeti ya serikali ilikuwa Bil 52 mwaka 2000/2001-sawa na asilimia 2.95% ya bajeti ya taifa. Wakati awamu ya nne imeingia madarakani, Mh Kikwete alisema mwanzoni mwa mwezi huu (1-3-2012) wakati anapokea maandamano kuwa bajeti ilikuwa bil 233 fedha za kitz. Leo hii (2011/12) bajeti ni Bil 926 sawa na asilimia 6.9 ya bajeti nzima. Sasa, ukichukulia bajeti huwa haifizingatii mfumuko wa bei, kwa mwaka huu, real budget ni kama Bil 500. Kwa maana nyingine tunapewa matumaini na mh Mkullo kuwa bajeti imeongezeka, but in real sence hakuna kitu. Pili kama nilivyosema awali, ni ngumu kuleta mapinduzi bila kupindua AKILI za watendaji wakuu. Mfano leo unahamasisha uzalishaji, unatoa ruzuku pembejeo na zana za kilimo. Porduction (sio productivity) inaongezeka, lakini una-HISI kuwa kuna njaa kata, tarafa au wilaya fulani. Mtendaji mkuu anatoa AMRI - ubabe fulani hivi kuwa TANGU LEO HAKUNA KUUZA MAHINDI AU MCHELE NJE YA NCHI! Ebhoo! Jiulize huyo anajua mimi mzalishaji nimekopa kiasi gani benki na kuna loan repayment schedule nimekubaliana na benki kwa kuangalia wakati wa mavuno? Haya kazuia, anamwambia mtu wa Grain Reserve kuja kununua badala ya private buyers. Kwa kuwa mtu wa grain reserve anakuwa ni mmoja ana-monopolise soko, thus anakupatia bei anayodhani inafaa...hakupi bei ya soko! Give me peace bandugu. MKULIMA ANANYONHYWA KUPITIA MATAMSHI KAMA HAYA! Sasa endapo wakulima wangejipanga vizuri, bila shaka wangedai fidia

  Kwa upande mwingine, sina hakika kama iwapo tunazuia uuzaji nje, huwa vibari vya kuingiza unga/mahindi toka nje huwa vinazuiwa. Kuna uwezekano havizuiwi. So, what happens, mazao yaliozalishwa na wakulima wetu, ambao tumeapa kulinda maslahi yao yanaozea majumbani wakati mazao toka nje yanaingizwa tena kwa msamaha wa kodi.
  Hebu tuangalie gharama nyingine kwa mkulima ya utunzaji. Kuna takwimu kuwa post harvest losses zina-range between 25 (nafaka) -70% matunda/mbogamboga. Kwa mkulima ambaye amelazimishwa (YES AMELAZIMISHWA) kutunza mazao nyumbani kwake inampatia hasara kwa kuingia gharama ya utunzaji (storage costs) na madawa na hata nafasi na udhia nyumbani.
  Wakati huo tunahubiri ujasiriamali katika ku-transform kilimo? How??? Ni vema ziwepo zijitahaza za maksudi kwa serikali kusimimamia taratibu na kuacha maslahi binafsi. Mh Kikwete kwenye hotuba yake tar1 March 2012 alisema hata wanapozuia usafirishaji vyakula nje, watendaji fulani ndo wanaonufaika kwa kuenda kinyume na taratibu. Swali la msingi hapa ni je.... Ni jukumu langu kuhakikisha kuwa jirani yangu anachakula cha kutosha? La HASHA! Ni jukumu binafsi na pia jukumu la serikali! Na je ni sahihi serikali kunizuia kuuza mazao yangu kwa muda, mahali na wakati ninapotaka? JIBU ni la! Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya mkulima. Na kimsingi inakinzana na jitihada za serikali yenyewe kuleta mapinduzi.Mapinduzi lazima yawe outward looking

  Mwisho kwa sasa

  Lakini kuna weakness kubwa katika kusimamia sheria nchi hii, na hasa sheria za kumlinda mkulima. Sometimes kuna mgongono wa kimaslahi ndani ya watendaji. Mkuu wa mkoa fulani nilimtembelea mwaka fulani kwenye crisis ya ununuzi wa korosho. Alikuwa amekasirishwa sana na mchakato mbovu wa ununuzi pamoja na kiburi cha makampuni ya wanunuzi. Alisema 'amepokea maelekezo toka kwa waziri kuwa akubaliane na makampuni ya wanunuzi wa korosho kwa bei wanayotaka wao'. Nakumbuka tulimwuliza wewe umemjibu nini? Akasema amemwambia yeye si mkulima wa korosho, suala la bei ni wakulima wenyewe waridhie,vinginevyo watendaji wa serikali ndo wawauzie hao makampuni korosho zao walizolima mashambani mwao! Kwa ufupi ni kwamba Kilimo chetu kiko-highly politicised! Laiti wakulima wangeamuka wangeidai fidia serikali kwa baadhi ya mambo ambao nadhani hayaendi vizuri.
  Mimi ni mkulima wa nanasi na machungwa. Wakati wa msimu huwa nauzia shambani au naleta mjini. Bei ni tofauti. Lakini najiuliza kama Azam angenipa mkopo wa kuzalisha nanasi/machungwa tani kadhaa na kwa ubora kadhaa kwa wakati fulani, kisha serikali ikaniambia nisiuze mananasi hayo kwa Azam sijui inaweza kuwaje! Hii inaweza kusababisha mtu kujinyonga hivi hivi

  Mwisho mwisho kabisa. Suala la Korosho nimeambiwa baadhi ya viongozi hasa Tandahimba wanakatiwa mazao yao shambani simply because wakulima wanahisi kuwa wamechangia kutopatikana wanunuzi. Wanunuzi wenyewe hawafunguki kuweka wazi kwa nini hawanunui. Bahati mbaya sana, wanunuzi wengi wa korosho ni wahindi/wana-asili ya India. LAKINI tujiulize IINDIA NI WALAJI WAKUBWA WA KOROSHO DUNIA HII? Jibu ni hapa! SO why bank on Indians (hii kauri yaweza kuonekana ni ya kibaguzi but I do not mean it) while you know they are not final consumers? Mwuliza Mh Mpya mwenyekiti wa bodi ya Korosho (Anna) hata yule aliyepita (Kitwana) bodi zimefanya nini kutafuta real markets badala ya kutegemea hawa wachuuzi/watu wa kati? Kwa nini viwanda 11 vya kubangua korosho vilivyo binafisishwa hadi leo zaidi ya nusu havifanyi kazi? Why can we add value to our korosho, create employment and secure the market? Kwa nini tulenge ulaya wakati tunajua hata tungelenga makampuni ya ndege za Afrika tungeuza korosho kiasi kizuri tuu? Inatia uchungu. Nitarudi kesho kutwa!
   
 13. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Elimu ya TV na magazetini haiwezi kufanikiwa sana, labda kama ni kuhusu masoko. Mabwana shamba wawe na mashamba yao ya mfano...kauri ambao Mh Pindi amekuwa anaitoa mara kwa mara, but no follow up! Hii nchi ni maagizojuu ya agizo but no time to assess and evaluate implementation ya hayo maagizo!

  Uzoefu wangu unaonesha watu wazima wanajifunza kwa haraka wakifanya na hasa jambo lenyewe kama liko-connected with tangible gains - they have no time to waste. Vijana wanaomaliza vyuo wangekuwa ndio chachu ya kuleta maendelelo endapo wangejengewa mazingira mazuri - kisera, kimiundo mbinu na upantikanaji wa huduma za kifedha na ushauri wa kitaalam!

  Juzi Mh Maghembe alisema kwa nini maafisa kilimo/mabwana shamba wanafungua maduka badala ya mashamba? Ikanikumbusha mtu mwingine mwaka 2009 alisema -lecturers wengi wamefungua guest houses badala ya hata shule za nursury ambazo zinaelekea kwenye taaluma zao. Naomba kuishia hapa!
   
 14. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280


  1. KUHUSU ELIMU, Elimu ya kilimo bora si jukumu la serikali mkuu, kwani hata nchi za jirani kama kenya hii kitu inafanywa na private company, na ni jukumu letu sisi kuchukua nafasi hii kuprovide elimu ya kilimo,
  Je ni wangapi wamejaribu kuanzisha elimu hii wakashindwa? ni vikwazo vipi walipata?

  2. Hapo kwenye red, mkuu napingana na wewe kabisa kwamba ni mpaka serikali ituwezeshe, fikilia vijana wanamaliza pale SUA na elimu yao ya mifugo, hawa vijana wanashindwa nini kukaa chini na kuja na aidea ya hata kufungua kampuni yao ya kutoa ushauri wa elimu ya mifugo? je ni mpaka wasubiri serikali?

  Haya mambo ya kusubiri serikali iboreshe mazingira tutakuja kukuta mwana si wetu, wakati vijana wakenya wanafulika huku TZ kudill na oportunity zilizopo sisi tunasubiria serikali iboreshe mazingira.

  JE SERIKALI ISIPO TUTAFANYAJE? TUTABAKIA KUWA WATAZAMAJI? TUTAENDA KWA VIJANA WENZETU WA KENYA NA KWINGINEKO WATUAJIRI?

  3. KWENYE GREEN

  1. Hili si Tatizo la malecture, au ma afisa kilimo, ni tatizo la Watanzania wengi sana, WATANZANIA WENGI SANA WANAPENDA
  - BIASHARA ZISIZO UMIZA KICHWA
  - BIASHARA ZA KULETA FAIDA SIKU HIYO HIYO
  - HAWAPENDI MIRADI MIKUBWA NA YENYE KU GENARATE PROFIT BAADA YA MIAKA HATA MITANO
  2. Watanzania tunapenda sana Biashara za uchuuzi, na nazani Tanzania ni miongozi mwa nchi ambazo biashara ya Uchuuzi iko juuu sana
  - Hatupendi Project kubwa, Na watanzania hawako tiyali kuwekeza kwenye miradi ambayo inatoa faida baada ya miaka hata 6,

   
 15. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280

  MKUU NIMEPENDA MAELEZO YAKO NA NI MAZURI SANA,

  1. Mkuu suluhisho la haya yote ni sisi wenyewe kuwa na Viwanda vya kusindika nafaka, si dhani kama serikali inazuia kuuza mahindi ndani ya nchi. KWA NINI TUSIWE NA VIWANDA VIDOGO VYA KUSINDIKA MAHINDI THENI TUNAUZA UNGA KENYA? MAKE UNGA UNARUHUSIWA KUUZWA NJE,

  Mimi sioni Tatizo hapa, ila ni sisi wenyewe watanzania tunapenda BIASHARA RAHISI NA ZISIZO TUMIA AKILI NYINGI, NA NI ULEMAVU WA AKILI HUU,
  - KUNUNUA MAHINDI ARUSHA NA KUPELEKA KENYA HAIHITAJI UJUZI WA AINA YOYOTE ILA KUFUNGUA KIWANDA CHA KUSINDIKA INAHITAJI AKILI SANA, NA HAPA NDO TATIZO LILIPO.

  LAZIMA SISI HUMU TUANZE NA SMAA INDUSTRY ZA KUSINDIKA NAFAKA THEN TUUZE PRODUCR ANA SI RAW MATERIO

  2. SWALA LA EXPORT BUN LIPO NCHI NYINGI SANA MKUU, HATA BAADHI YA NCHI ZA ASI KAMA THAILAND, VEITINAM, CHINA NA ZINGINE WAMEPUNGUZA KU EXPORT CHAKULA NJE ILI KUZUIA UPUNGUFU NDANI YA NCHI ZAO

  3. HAPO KWENYE NANASI
  KILIMO CHA MKATABA NDO SULUHISHO LINGINE MKUU, HIZI KAMPUNI ZA HUKU ARUSHA ZINAZO LIMA MBEGU ZA MAUA ZINATUMIA SANA KILIMO CHA MKATABA,
  NA HATA WAO WANAPO UZA NJE NI KWA MKATABA

  WEWE IMAGINE UNAINGIA SHAMBANI KULIMA HUJUI UTAMUUZIA NANI NA UNAISHIA KUAMBIWA KWAMBA KUNA WANUNUZI WATAKUJA, NA HATA WAKIJA THEN WAKALINGA KUNUNUA HUWEZI WASHITAKI POPOTE MAKE HAWAJAKUTUMA ULIME

  MIMI SIONI KAMA KUWALAUMU WANUNUZI NI HAKI KWA SABABU HAKUNA MKULIMA ALIE INGIA NAO MKATABA WA KULIMA KOROSHO AU PAMBA,

  LAKINI KUNGEKUWA NA KILIMO CHA MKATABA, AMBACHO KINAKUWA NA MAKUBALIANO YA KIMANDISHI KATI YA MNUNUZI NA MKULIMA NA HAPA MNUNUZI ASIPO ONEKANA UTAMSHITAKI KISHERIA NA ATAKULIPA

  HUKU BONGO TUNALIMA TUKIAMINI KWAMBA WATANUNUA TU, HIKI NI KILIMO CHA KABLA YA MAPINDUZI YA KILIMO HUKO ULAYA, NA NDO MAANA WANUNUZI WANA KIBURI KWA SABABU WANAJUA FIKA WAKULIMA HAWAWEZI KUWAFANYA CHOCHOTE MAKE HAWAJAWATUMA KIMAANDISHI KWAMBA WALIME

  SIASA ZIMEKUWA NYINGI SANA ANASIMAMA MKUU WA WILAYA ANAWAAMBIA LIMENI ALZETI KUNA SOKO ZURI SANA, SOKO ZURI KIVIPI? TUMEINGIA NAO CONTRACT NA WAKATUHAKIKISHIA KIMAANDISHI KWAMBA WATANUNUA ALIZETI?

  HUKU TUNADAGANGANYANA, BILA CONTACT FARMING HAKUNA KILIMO, HII YA KUSEMA KUNA SOKO ZURI ULAYA, MAREKANI NA KWINGINEKO NI UONGO MTUPU, BILA KUONGEA NAO KIMAANDISHI USIDANGANYIKE, UATALIMA HALAFU UTAISHIA KULIA BURE
   
 16. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  MKUU KWENYE GREEN.

  1. Kumbuka kwamba hivi vyama vya ushirika na kilimo cha ushirika kilikuwepo kisheria na ilikuwa ni lazima ujiunge na ushirika na si hiyali, enzi za chama kimoja

  Na ushirika ulikuwa na watu zaidi ya buku, sasa kwa mazingira ya sasa hatuhitaji ushirika tunahitaji kuunganisha nguvu kufungua makapuni, make bila kuunganisha nguvu hatutaweza kushindana na makampuni ya Makaburu au wahindi na wachina
   
 17. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  1.Naunga mkono hoja, kwani hili si lazima liwe jukumu la serikali. Lakini swali la kujiuliza ni wangapi wanaweza kuchukua hii initiative na wakaifanyia kazi? (including you) Je kibiashara ni viable? Na hata kama sio viable, je magazine hii haiwezi kuwa funded na Sponsors pamoja na advertisers? (i mean non profit publication). Kuna Jarida moja la The Agriculturalist huko Texas (Texas Tech University) lilianzishwa na wanafunzi tu. Vipi kuhusu sisi?

  2. Hapo kwenye namba 2, ninakubaliana nawe kwa sehemu fulani, lakin bado mchango wa Serikali unahitajika katika uwezeshaji.. Labda nitoe mfano, back in 2004, serikali ilikuja na mpango wa urasimishaji biashara na rasilimali. Mpango huu ulikuwa ni mwanga mpya kwa Watanzania wengi hasa linapokuja suala la kuhuisha DEAD CAPITAL kama mashamba ili yawasaidie katika kujikwamua. Sasani miaka Takribani nane, na bado ukienda kijijini mifumo rafiki bado haijawekwa, na wananchi bado wanashindwa kurasimisha mashamba yao. Sasa hebu niambie hatma ya huyu Mwanakijiji (tena aliyekosa elimu)
  Najua hata suala hili linaweza likafanywa na Private Sector, but gharama yake ni kubwa sana hivyo kupelekea watanzania wengi kushindwa kumudu.

  Je Serikali isipofanya tufanyaje?
  1. Kwanza kuna umuhimu wa kutumia forum zilizopo ili kuishauri?kuishinikiza serikali kwani ni wajibu wake, na tunalipa kodi ili itimize wajibu huo.
  2. Wakati tunaishauri serikali ni vyema nasi kwa vikundi au kila mmoja kwa nafasi yake akatimiza wajibu wake, kwani mambo mengine yapo ndani ya uwezo wetu.

  Nionavyo mimi, changamoto kubwa kwa nchi hizi zinazoendelea kama Tanzania ni upungufu wa Social Entrepreneurs, Innovators na uhaba wa R&D. Hata wale innovators wadogo wadogo waliopo hawaendelezwi na kuthaminiwa, hivyo ubunifu wao unapote bure. Yaan ni mpaka wazungu tena waje watusaidie?

  Natamani wanabodi wangesoma Kitabu hiki "THE BOY WHO HARNESSED THE WIND" by William Kamkwamba & B. Mealer.
  Kijana huyu alitokea katika familia yenye maisha duni sana huko Malawi, lakini aliweza kutengeneza mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia vyuma chakavu, na miti (na kutengeneza windmill). Ukweli ni kwamba hata shule hakuweza kumaliza kutokana na ukosefu wa ADA, lakini akiwa na miaka 14 tu, aliweza kuleta umeme kwenye familia yao na kijiji chao. Sisi wengine huku tumekaa tukilalamika tu pamoja na elimu tulizonazo, wakati kuna watu wanaleta mabadiliko. Hata wale wachache wanaoleta mabadiliko tunashindwa kuwatambua na kuwathamini
   
 18. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Naomba nijikite hapo kwenye red kwanza
  Kwani Public Companies zinakuwa na Shareholders wangapi?
  Mbona NICOL walikusanya mitaji kwa mfumo wa Kampuni na dado wanahisa wake wanalalamika kuwa hawaoni faida ya mitaji yao? Na huu ni mwaka wa nne sasa
   
 19. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  SIKUTAKA KURUDI HAPA KWA SASA, lakini nimelazimika


  Katika context (muktadha) wa Tanzania kwenye siasa na maendeleo vipo pamoja. Hivyo huwezi kusema kujengewa mazingira, hasa kwa kilimo you will need something. Mfano, endapo unahitaji mkopo say unawekeza kwenye samaki wa kufuga utahitaji ardhi, unless you got tittle dead au hata CCRO - customary certificate of right of occupancy. This is a process hasa kwa mtu mmoja mmoja. Serikali inapaswa kuwekeza kufanya upimaji wa ardhi - itoe certificate kwa vijiji viwe na land registry ndo viweze kutoa CCROs. Hili litamwezesha mtu kutumia ardhi kama collateral - hapa pia ina maana ni jukumu la serikali kuhakikishia mabenki kuwa ardhi hata ile ya vijijini inaweza kutumika kama collateral! Huu ndo uwezeshwaji wa serikali nilio-maanisha. Pia endapo mtu unafunga samaki utahitaji huduma za vyumba baridi/cold roooms! Hii haiwezekani kama hakuna umeme! Huu ni uwezeshaji pia wa serikali.

  Kimsingi tunaongea kuleta mapinduzi ya kifikra kutoka kilimo cha kujikimu kuja kwenye kilimo cha biashara. Sasa graduate hata kama anaanza mwenyewe, ni lazima yawepo mazingira bora yanayohamasisha kuwekeza

  Likewise mfanya biashara hana mkataba na mlimaji, lakini anaweza kushawishika kuingia biashara kama mazingira ni bora. Nijuavyo mimi kilimo cha mkataba sio mwarubaini -panacea ya matatizo ya soko na ubora wa mazao. Katika mfumo wa sasa zipo avenues nyingi sana za kufanya biashara, but sisi tumeendelea kuangalia njia moja! Wakati mwingine natamani niache kazi nijikite kabisa kwenye kilimo -mazao au mifuko (amid challenge ya upatikanaji wa maji na malisho).

  La mwisho, kuna Enterpreneur (nadhani- sikumbuki nani humu) ameongea kuhusu export ban (sio bun). Jambo hapa muhimu kujua ni kwamba we are not totally against it, BUT should not be done by violating farmers and or traders' right! What do I mean here? Serikali iki-impose ban iwe tayari kununua kwa bei ya soko tena pasipo usumbufu. FINITO! Wale ambao wanaimpose ban, lazima wanakuwa na mechanism za kuuza. Mkutano wa wiki hii hapa Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alilalamika SANA kuhusu unsold consignment ya mahindi - over 600 tonnes!Waziri akakataa kuwa kiasi hicho hakipo. Alipoulizwa mtu wa Grain reserve hakuwa na takwimu! Sasa ban zinazoenda bila enough data unategemea nini
  Mchana mwema

   
 20. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  1. Mkuu kwenye jarida la kutoa elimu ni sahihi, na si jarida pekee, kuna vitu ingi sana kama semina, mikutano, mashindano fulani fulani ya kushindinasha wakulima wetu na kazalika
  Ni kweli ni jukumu langu, lako na la wengine kuchua hatua mkuu, ni kweli serikali inatakiwa ihusike sasa je ni lini tunajua watabadili sera ziwe nzuri?

  2. Ni kweli kabisa kwamba urasimishaji huu umekwama sasa je tufanyeje? tusubiri mpaka hapo utakapo fanikiwa? je sisi wenyewe hatuna njia mbadala?

  3. Ni kweli public company zina share holder wengi sana na kwa kesi ya NICOL kuna shida, na ndo maana nasema mitaji tuanze kuunganisha sisi tunao fahamiana kwanza
  HAPA TANZANIA HATA WANAFAMILIA HAWATAKI KUUNGANISHA MITAJI ILA WANASHINDANA WAO KWA WAO KITU AMBACHO KWA WAZUNGU HAKIPO, SI AJABU KWA BONGO KUKUTA MTU NA DADA YAKE AU KAKA YAKE WANASHINDANA KIBIASHARA BADALA YA KUUNGANISHA NGUVU NA KUTENGENEZA INVESTMENT KUBWA

  Tunatatizo la kila mtu kutaka aonekane kwenye jamii kwamba ni mjanja sana na ana pesa sana na biashara ni yake, na ndo maana TANZANIA TUNAPENDA SANA BIASHARA ZA INDIVIDUAL NA si za kuunganisha mitaji.

  Haya hata huko kenya yapo ila wale wakenya kwa sasa hawalalamiki tena bali kwa sasa wanachukua hatua kivyao vyoa tu sasa sisi tukisubiria serikali itakula kwetu
   
Loading...