Matatizo makuu matano ya sisi watanzania

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,917
wadau nawasalimu sana!!
mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa tuna madui watatu Wa kupigana nao
1.ujinga
2.maradhi na
3.umaskini..

kwa muda sasa tumeendelea kukariri hao maadui kwa miaka nenda rudi!! hata hivyo kwa uelewa wangu na uzoefu wangu katika nchi hii ikiwemo kutembea mikoa kadhaa mjini na vijijini nimeona niyataje matatizo makuu matano ambayo ndio hasa "kiini" cha Hapa tulipo Leo... pengine yapo mengi lakini kwangu mimi nimeona haya ndio haswa matatizo Yetu watanzania...
1.WOGA
hili ni tatizo kuu, tumekuwa maskini kwa sababu ya woga, tunashindwa kudai haki zetu nyingi kisa kuogopa kufanyiwa hiki au kile!! ndio maana operation ukuta ikafa kifo cha kawaida baada ya intimidation.

2.TUMEIELEWA VIBAYA SIASA
sidhani kama siasa hii inayofanyika nchini kwetu ni sawa na siasa za nchi nyingine! ni kama tuna aina Yetu ya siasa ama njia Yetu binafsi ya kufanya siasa!! mgonjwa yupo hospitali anahitaji dawa za shilingi elfu kumi 10,000) ili apone ...mwanasiasa anakuja na waandishi Wa habari kwa gharama ya shilingi elfu 50 kisha anatoa msaada Wa dawa Wa shilingi elfu mbili!! huu ni mfano Wa kwanza!!

mfano Wa pili...kuna sehemu inabidi ijengwe shule isaidie watu wote bila kujali vyama vyao...lakini kwakuwa anayefadhili ni Wa chama Fulani basi ama atazuiwa au itacheleweshwa kujengwa makusudi na watu wenye nguvu Wa chama kingine!!

mfano Wa mwisho,
Musa anatoa siri kuwa kijiji fulani kina tatizo la vyoo katika zahanati yao na tatizo hilo lipo kwa miaka kadhaa na thamani ya ujenzi Wa hivyo vyoo ni milioni 10 tu na habari hii ikatangazwa na vyombo vya habari sasa angalia kinachotokea..
a) Musa atakamatwa kwa uchochezi.
b) zitatumika milioni 30-40 kuficha ukweli kuhusu hicho kijiji!! narudia tena hii ni mifano tu!!

4.UNAFIKI
Tatizo lingine kubwa ni hili ingawa pia lipo sehemu nyingi lakini sisi linatuumiza zaidi...tumeona wakati Wa kampeni watu wanajaa, wanashangilia..lakini mwisho Wa siku wanaamua kufanya yao!! wabunge wanaomba kura vizuri lakini wakifika bungeni hawafanyi tena kwa ajili ya waliowatuma!!
rafiki zangu ukisikia mwanasiasa anasema "tuweke maslahi ya nchi mbele kwanza" kwa Hapa Tanzania basi jiongeze!!

5.UVIVU

hili pia ni tatizo kubwa linalotutafuna si kwamba hafufanyi kazi! tunafanya lakini si katika bidii!! kuanzia hata mafundi, wakulima, wafanyakazi n.k bado hatujafanya kazi kwa bidii na hiki ndio kinatutafuna maana tunabaki kuwa tegemezi na watumwa.

5.USAHAULIFU
Ni kweli binadamu wameumbiwa kusahau lakini sisi ni too much! yaani tunapigwa goli halafu ikipelekwa krosi moja tu tukapata kona tunasahau kabisa kuwa tumefungwa!! kuna watu wanalalamika maisha magumu, hakuna nyongeza za mishahara, sijui kodi, sijui hivi..lakini mtu akipewa kofia na tisheti na elfu mbili!! anasahau tabu zote alizopata miaka nenda rudi!! Hapa sitii neno!! na sitaki kufukua makaburi.
asanteni..
tubishane kwa hoja.
 
Mkuu namba 2 sio tanzania tu ni africa nzima,lakini number 5 nakubaliana nawewe.
 
Bhanaa kote umepita vizuri sana ila namba tano wajuvi wanasema umelenga bull
Mana saivi mtu anaweza aka kaa masaa manne na kuendelea kila siku kujadili nchi na Serikali.umbea umbea tuu.
Si magazeti si television kila kitu full ni ku promote matukio na Kiki za wasanii nakusahau jinsi gani ya kuzalisha kuku wakienyeji wengi na mayai.

Yani wengi tuna jifanya wazungu na ndomana tuna kuwa tegemezi kila siku.
 
wadau nawasalimu sana!!
mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa tuna madui watatu Wa kupigana nao
1.ujinga
2.maradhi na
3.umaskini..

5.USAHAULIFU

Kweli wasahaulifu. Tunashauriwa kila siku, kwamba kama nyuma tulilala mbele tusilale tena, lakini sie nyuma tulilala na mbele tutalala!

Sisi watu kweli?
 
UVIVU . ...ACHA KULALAMIKA KAMA WAISRAEL JANGWANI . ..ILIBIDI WAFIE HUKO MAANA HAWAKUTAKA KUBADILI MAWAZO YAO . ..MAANA RICH PERSON THINKS OF BEING RICH UNFORTUNATELY POOR PERSON THINKS OTHERWISE . ..YOU ARE WHAT YOU THINK . ...BADILIKENI ACHENI KULALAMIKA . ...DAH !
 
wadau nawasalimu sana!!
mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa tuna madui watatu Wa kupigana nao
1.ujinga
2.maradhi na
3.umaskini..

kwa muda sasa tumeendelea kukariri hao maadui kwa miaka nenda rudi!! hata hivyo kwa uelewa wangu na uzoefu wangu katika nchi hii ikiwemo kutembea mikoa kadhaa mjini na vijijini nimeona niyataje matatizo makuu matano ambayo ndio hasa "kiini" cha Hapa tulipo Leo... pengine yapo mengi lakini kwangu mimi nimeona haya ndio haswa matatizo Yetu watanzania...
1.WOGA
hili ni tatizo kuu, tumekuwa maskini kwa sababu ya woga, tunashindwa kudai haki zetu nyingi kisa kuogopa kufanyiwa hiki au kile!! ndio maana operation ukuta ikafa kifo cha kawaida baada ya intimidation.

2.TUMEIELEWA VIBAYA SIASA
sidhani kama siasa hii inayofanyika nchini kwetu ni sawa na siasa za nchi nyingine! ni kama tuna aina Yetu ya siasa ama njia Yetu binafsi ya kufanya siasa!! mgonjwa yupo hospitali anahitaji dawa za shilingi elfu kumi 10,000) ili apone ...mwanasiasa anakuja na waandishi Wa habari kwa gharama ya shilingi elfu 50 kisha anatoa msaada Wa dawa Wa shilingi elfu mbili!! huu ni mfano Wa kwanza!!

mfano Wa pili...kuna sehemu inabidi ijengwe shule isaidie watu wote bila kujali vyama vyao...lakini kwakuwa anayefadhili ni Wa chama Fulani basi ama atazuiwa au itacheleweshwa kujengwa makusudi na watu wenye nguvu Wa chama kingine!!

mfano Wa mwisho,
Musa anatoa siri kuwa kijiji fulani kina tatizo la vyoo katika zahanati yao na tatizo hilo lipo kwa miaka kadhaa na thamani ya ujenzi Wa hivyo vyoo ni milioni 10 tu na habari hii ikatangazwa na vyombo vya habari sasa angalia kinachotokea..
a) Musa atakamatwa kwa uchochezi.
b) zitatumika milioni 30-40 kuficha ukweli kuhusu hicho kijiji!! narudia tena hii ni mifano tu!!

4.UNAFIKI
Tatizo lingine kubwa ni hili ingawa pia lipo sehemu nyingi lakini sisi linatuumiza zaidi...tumeona wakati Wa kampeni watu wanajaa, wanashangilia..lakini mwisho Wa siku wanaamua kufanya yao!! wabunge wanaomba kura vizuri lakini wakifika bungeni hawafanyi tena kwa ajili ya waliowatuma!!
rafiki zangu ukisikia mwanasiasa anasema "tuweke maslahi ya nchi mbele kwanza" kwa Hapa Tanzania basi jiongeze!!

5.UVIVU

hili pia ni tatizo kubwa linalotutafuna si kwamba hafufanyi kazi! tunafanya lakini si katika bidii!! kuanzia hata mafundi, wakulima, wafanyakazi n.k bado hatujafanya kazi kwa bidii na hiki ndio kinatutafuna maana tunabaki kuwa tegemezi na watumwa.

5.USAHAULIFU
Ni kweli binadamu wameumbiwa kusahau lakini sisi ni too much! yaani tunapigwa goli halafu ikipelekwa krosi moja tu tukapata kona tunasahau kabisa kuwa tumefungwa!! kuna watu wanalalamika maisha magumu, hakuna nyongeza za mishahara, sijui kodi, sijui hivi..lakini mtu akipewa kofia na tisheti na elfu mbili!! anasahau tabu zote alizopata miaka nenda rudi!! Hapa sitii neno!! na sitaki kufukua makaburi.
asanteni..
tubishane kwa hoja.
Mi naona tatizo ni moja tu. Tumekosa 'rasilimali watu' ktk nafasi nyeti za nchi ambao ndio key players wa kutupa mwongozo mzuri ktk uchumi, siasa, jamii n.k
 
6.Roho mbaya
ROHO MBAYA:
Watanzania hatupendi kusikia mwenzako au jirani amefanikiwa, wapo tayari kutunga uongo, kukuroga, na kukushusha hapo juu ulipo ili muwe sawa au mambo yaharibike kabisa uishi kama shetani.
Mfano kama ni msanii,
*nyimbo zako hazichezwi
*kura za awards hatukupigii
*channel/promo za soko, connection na collabo hupewi.
*ukikosa shangwe, sapot na kuharibu kidogo, social media kuanzia Insta, Fb na Insta utapaona pachungu. Magazeti, redio, Tv na udaku watazungumza yaliyomo na yasiyokuwepo.
 
7. UAMINIFU

Watu wengi sio waaminifu,
Hili ni tatizo kubwa sana kuliko hata tunavyofikiria.
UONGO NA UTAPELI (UAMINIFU)
Kila kitu dili, mtu yupo tayari kuidanganya jamii na hata serikali kwa vyeti bandia au kukwepa kodi hata kwa nyaraka feki. Kumnyima mtu haki yake kwa taarifa za uongo au kutoa ushahidi wa uongo. Pia ukizubaa kidogo tu unakuta umeshatapeliwa na haki yako imepotea kwa sisi watanzania kukosa uaminifu.
 
Back
Top Bottom