Matatizo haya yatakwisha lini jamani? Umasikini?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
Begger.jpg

A street beggar shaves her child along Bibi Titi Street at Upanga in Dar es Salaam yesterday. (Photo: Selemani Mpochi)
 
Begger.jpg

A street beggar shaves her child along Bibi Titi Street at Upanga in Dar es Salaam yesterday. (Photo: Selemani Mpochi)

14. Haki ya kuwa hai
Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

na zaidi ya hiyo ibara ya 9 ya katiba iko wazi:

Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha–

(a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;



(i) kwamba matumizi ya utajiri wa
Taifa yanatilia mkazo maendeleo
ya wananchi na hasa zaidi
yanaelekezwa kwenye jitihada
ya kuondosha umaskini, ujinga
na maradhi;


(j) kwamba shughuli za uchumi
haziendeshwi kwa njia
zinazoweza kusababisha
ulimbikizaji wa mali au njia
kuu za uchumi katika mamlaka
ya watu wachache binafsi;


Hivyo basi jibu ni kuwa tukifuata na kuzingatia katiba matatizo yatakwisha.
 
Wananchi wenyewe tuna nafasi kubwa ya kubadili hali ya maisha yetu kwakuwachagua viongozi ambao sio manyangau.
 
Hii mbona wengine wameshageuza kazi, tunavyowahi kazini na wao wanawahi kutuwahi.
 
Wananchi wenyewe tuna nafasi kubwa ya kubadili hali ya maisha yetu kwakuwachagua viongozi ambao sio manyangau.
Ni kweli kabisa hakuna mgawanyo mzuri wa rasilimali za nchi, zaidi wanaofaidika ni viongozi manyang'au.
 
Mie nikiangalia vitu vingine hujiuliza kama serikali yetu ipo hai na yatenda haki kweli au boro twende tuuu. wenzetu USA wana fight for Health Care Insurance, Kenya wana fight katiba ibadirishwe hapa kwetu siju ndio ivyo kila kukichA siasa chafu na kujisifia kwingiii sana ambako hakuna maendeleo yoyote wafanyakazi wakipanga kugoma serikali ya piga mkwala sasa sijui serikali yetu yataka kuongoza watu wa aina gani sijui
 
Umaskini utakwisha tukipata mtu kama kagame sio hawa wasio jua njaa inaumaje
 
Back
Top Bottom