Matatani kwa kuuza vipodozi vya kuongeza Makalio na Matiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatani kwa kuuza vipodozi vya kuongeza Makalio na Matiti

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Aug 19, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mojawapo ya madawa ya kuongeza makalio na hips Saturday, August 15, 2009 3:10 PM
  WANAWAKE wawili wanashikiliwa na polisi kwa kudaiwa kujihusisha na uuzaji wa vipodozi vya kuongeza maumbile huko maeneo ya Kariakoo jijini Dar. Watuhumiwa hao majina yao hayakupatikana mapema kwa sababu za kiupelelezi walikamatwa katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam wakiuza vipodozi hivyo kwa siri.

  Watuhumiwa hao walidaiwa kujihusisha na kuuza vipodozi vinavyosababisha kuongeza maumbile ya akina mama maeneo ya makalio na matiti ambavyo vinapigwa marufuku na Serikali visitumike nchini.

  Hivyo ilidaiwa kuwa wafanyabiashara hao walikuwa wanatoa vipodozi hivyo nchini China kwa lengo la kuwauzia akina dada wenye malengo ya kuongeza makalio na matiti vikiwemo na vipodozi vya kubana maumbile sehemu nyeti kwa akina dada kurudisha bikira.

  Vipodozi hivyo viligundulika hivi karibuni vikitumika na wakinadada wengi na serikali kupiga marufuku uingizaji na uuzaji wa vipodozi hivyo nchini.

  Serikali ilipiga marufuku uingizaji wa vipodozi hivyo na wafanyabiashara wa vipodozi hivyo wanaendelea kuuza kwa njia ya siri madukani.

  Hivyo Mamlaka ya Chakula na Dawa wapo kwenye operesheni endelevu na kuzunguka maeneo ya jiji kuwakamata wanaoendelea kuuza vipodozi hivyo na kuwachukulia hatua za kisheria.

  Awali serikali ilikataza uingizaji wa vipodozi hivyo na kupiga marufuku kutumia vipodozi hivyo kwa kuwa utafiti uliofanyika uligundua kuwa vipodozi hivyo vina madhara kwa watumiaji na kumsababishia mtumiaji wa vipodozi hivyo baadae kuathirika na magonjwa ya kansa.

  Wafanyabishara hao walifkishwa katika kituo cha Msimbazi Polisi huku upelelezi wa kina ukiendelea.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2817774&&Cat=1
   
 2. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dah! hao akina dada wanataka wenzao warudhike zaidi nini?.
   
Loading...