Matarajio wa wanaCCM juu ya uwezo wa JK ktk kusimamia mchakato wa KATIBA yako wapi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matarajio wa wanaCCM juu ya uwezo wa JK ktk kusimamia mchakato wa KATIBA yako wapi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by meddie, Nov 23, 2011.

 1. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu watz na wanasisiem embu turudi nyuma kidogo na kufanya tathimini juu ya uwezo binafsi wa JK kama kiongozi mkuu tunayetarajia kusimamia mchakato wa kuandika KATIBA yetu. (Hapa leo naomba kusema mapema kwamba tunachoangalia/hoji si uhalali wa JK bali uwezo binafsi wa JK) Hasa tukijua kwamba swala la KATIBA ni swala kubwa linalohitaji usimamizi mzuri na busara za kutosha. Tukumbuke swala la KATIBA ni zito na inabaki kuwa dira yakutuongoza ktk kujenga/kuleta ustawi mzuri wa kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa muda mrefu!

  Sasa wote tunamfahamu vizuri kiutendaji ndugu yetu JK, kwa kumuona akipita na king'ola, kumsikiliza nk. Hivyo tunaweza kuongea/kutathimini juu ya uwezo binafsi alionao kiutendaji, kiusimamizi na kama kiongozi then tuone kama anaweza kuchukua jukumu la katiba! Tuangalie yafuatayo:
  • Natumai wote tunakumbuka akisema hajui kwa nini Tz ni masikini........je anaweza kuwasimamia chombo(KATIBA) ambayo tunataka isimamie rasilimali zetu na baadae tuondokane na unasikini?
  • Ametuahidi mambo mengi ya hapo kwa hapo na yasiyo ya hapo kwa hapo.....lakini tujiulize ameweza kutimiza mangapi ilitujue tukimpa swala hili zito la katiba ataweza kusimamia vizuri
  • Yeye na watu wake (mawazili wake) ameshindwa kutatua swala la umeme pamoja na kutuahidi kwamba itakuwa historia lkn bodo mgao mpaka kesho
  • Yeye kama kiongozi mkuu wa chama "CCM" ameshindwa kuvua magamba ambayoa walisema ni ndani ya siku 90. Lkn hadi leo kashindwa...sasa je tumtwika swala katiba taweza kweli? (nauliza tu!)
  • Swala la Richmond je ameweza kulitatua?
  • Swala la mafisadi je ameweza kulitatua?
  • Swala la uchumi je anayomikakati yeyote anagalau ya kuokoa shilingi yetu inayodidimia kila iitwapo leo. Juzi nilisikia akiongea na wazee juu ya hali ya uchumi lkn aliwaeleza kwamba hata mataifa mengine hali ni hiyo hiyo...so what?
  • nk
   
Loading...