Matarajio na Matamanio ya Mabadiliko; Kazi hazifanyiki maofisini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matarajio na Matamanio ya Mabadiliko; Kazi hazifanyiki maofisini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Jan 25, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nadhani nitakuwa sawa kama nikisema kwamba Tanzania haijawahi kuwa na post election fever and enxiety ndefu kama hii ya wakati huu.

  Kadri hali ya siasa za Tz inavyozidi kuchacha, hali ya kiuchumi inavyozidi kuwa ngumu, serikali inavyoshindwa kuongoza, upinzani unavyozidi kuimarika, basi wananchi wengi wanazidi kuwa na shauku ya ni lini mabadiliko yatatokea.

  Wafanya kazi wa serikalini, mashirika ya umma na asasi zisizo za kiserikali, wote wanafuatilia siasa za nchi hii wakati huu kuliko vipindi vingine vyote awali katika nchi hii. Vyanzo vya habari vinatumika barabara, iwe magazeti, runinga, blogu, simu, au mijadala ya ana kwa ana. Tofauti na zama nyingine zote Tanzania, wakati huu, hakuna mwananchi asiyejua nchi iko kwenye tatizo gani. Most public servants are blogging against their government!!

  kwa sababu hiyo, utaona kwamba watz wengi sasa wana hamu ya kuona nini hatima ya haya mambo, ingawa haiko wazi hatima inayotarajiwa ni ipi ilimradi kila mtu anatarajia jambo fulani kubwa litokee. Kuna wanaoamini tunahitaji kufanya kama Tunisia, sasa hivi. Kuna wanatamani utokee muujiza viongozi wa juu wa serikali wabadilike ghafula. Kuna wanaotamani 2015 ifike kesho. Kuna wanatamani uchaguzi mkuu urudiwe leo! Kuna wanaoamini kwamba Bunge litakomesha hii hali, litaleta mabadiliko.

  La msingi ni kwamba, fikra za watz wengi ziko kwenye matarajio ya mabadiliko na wanatumia muda mwingi kufuatilia na kutamani kinachoendelea kuliko wanavyofikiri na kufanya kazi zao. Haina maana kwamba kazi hazifanyiki kabisa, lakini nadhani siyo kwa tija kama ambavyo hii hali isingekuwepo. Ni kama kusema watu wanalazimika tu kuamka asubuhi na kwenda kazini, hawajisikii. Muda mwingi kutwa wanafuatilia habari kwa njia mbalimbali.
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu heshima yako, ile issue ambayo unayo nimekuwa nikiitafuta bila mafanikio please naomba unipatie
   
 3. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  truely
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Correct.Umefanya diagnosis nzuri.
   
 5. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Yaani ni kweli kabisa,asubuhi nikifika ofisini kila mtu yupo busy na magazeti au mtandaoni akiperuzi habari mbalimbali
   
 6. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unafaa kuwa mganga wa kienyeji maana unayajua yaliyo moyoni mwa mgonjwa. Hakika bila kupata taarifa mpya huwa siwezi kula. Big up! Lakini lini mabadiliko yatatokea,nchi haina viongozi, CCM wenyewe kwa wenyewe wanalumbana. Matumaini ni kwa CDM tu. Lakini 2015 ni mbali, DOWANS itamwondoa JK, Amen
   
 7. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yani mi sina hamu,umeme shida maji shida foleni,kubanana kwenye daladala, hata nikiingia kazin nipo hoi,kazi haitamaniki hivi haya yataisha lini,kuishi kama vile si binadamu
   
 8. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesema mawazo yetu...
   
 9. s

  simanjiro Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  well said!...
   
 10. s

  simanjiro Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sitashangaa ukitoka waraka kutoka utumishi ukiwataka wakuu wote wa idara za serikali na mashirika ya Umma kuweka block kwenye server zao kuzuia access ya blogs na mitandao kama JAMIIFORUMS kwa wafanyakazi. NYIE SUBIRINI TU!
   
 11. V

  Vumbi Senior Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Siku zote jamii inapokuwa imezidiwa na matatizo ya kiuchumi haiwezi kufanya kazi kwa ufanisi. Kila mtu anafikiria ni kipi kifanyike ili aweze kuboresha maisha yake na familia yake japo bila kuwa na jibu sahihi kwani waliopewa dhamana ya kuiongoza inchi nao hawajui wafanye nini ili waweze kutatua matatizo hayo. Serikali ya TZ kwa sasa haina dira, hakuna kiongozi wa serikali mwenye uwezo wa kukueleza tanzania itakuwaje baada ya miaka mitano ijayo au malengo ya serikali ndani ya miaka mitano ni yapi na yatatekelezwa kivipi, viongozi wapo tu ilimradi siku imepita. Wananchi wameanza kuchoka au kuchoshwa na utendaji wa serikali hivyo muda mwingi wanasoma au wanatafuta habari ambazo zitawapa faraja ya mapinduzi ya matatizo yanayo wakabili. Kama hali hii ikiendelea kwa muda mrefu ni harisi sana wananchi kuiondoa serikali madarakani au utenadaji wa watumishi wa serikali kudorora kiasi ambacho uchumi unaweza kudidimia kabisa. Lazima viongozi wa serikali warudishe matumaini kwa watu kwa kuwawajibisha watenadaji wabovu na kuanza kufanya mapinduzi ya kiuchumi yatayofanya raia kuwa na imani na serikali.
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu?
   
 13. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Gurudumu, nimesoma nimerudia nikasoma tena! Nimeelewa! Hivi Poland ndio raisi na timu yake walikufa kwenye ajali ya ndege?

  Otherwise nimejichokea tu. Just came out from Kikao cha Kamati ya Elimu, Afya na Maji cha Halmashauri. Trust me, am sad, very sad! I have been feeling helpless since when it ended. Let me collect my thoughts!
   
 14. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndiyo ni Poland. Ndiyo naelewa exactly how you feel hasa madiwani, maji, elimu, na afya. Helpless is a much positive word!

  Na bado tunahubiri kwamba nchi yetu ni masikini?
   
 15. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Misri pamoja na kuongozwa kiimla, leo wameamua kufuata nyayo za Tunisia. Baada ya Algeria..wamesema yaliyoanza Tunisia ni REGIONAL MOVEMENT. Wamekusudia kuwawajibisha viongozi wadhalimu.
  Nadhani mkwere akiwa huko Davos umeupata ujumbe kupitia CNN/BBC
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hivi ni lini hao wafanyakazi wa serikali walianza kujituma na kufanyakazi kwa tija? ukawaona wanachacharika basi ujue kuna ulaji unapita vinginevyo kawaida ni kufika asubuhi kusaini mahudhurio, atatoka kwenda kunywa chai na haonekani tena.
  Ukimwona mtu anajituma huenda kuna vikao wanalipana posho!

  Kama tunafikiri vita kubwa ni kuondoa mafisadi kisha basi yanakwisha basi tunajidanganya. Kuna vita kubwa mbele ya kupambana na uzembe, ubabaishaji na UDOKOZI. Na vita hii itakuwa ngumu sana tusijeshangaa wakombozi wetu wa leo sisi wenyewe tukawageuka!
   
 17. l

  limited JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  pole ndugu yangu leo nimemfukuza kada wa ccm anapita ofisini kwangu anaomba mchango i was so pissed off
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Gurudumu, nchi yetu sio masikini. Masikini kwa sababu gani? Imekosa nini?

  Nilikuwa najiuliza kwenye kikao, kila mchangiaji alikuwa anelezea kuhusu elimu duni! Nikajiuliza; ni nani huyu tunayemwambia kuhusu elimu duni ambaye yeye haelewi na haoni? Kwani yeye hakereki? Yeye ndiye anahamisha walimu, yeye ndiye halipi mishahara, yeye ndie hawezeshi walimu kufundisha katika mazingira mazuri! Haoni! Hajali!

  Kwenye kata yangu, kuna shule haijanunua kitabu hata kimoja kwa mwaka mzima wa 2010! Hela ipo! Lakini anayetakiwa kusupply anadai uchaguzi ulimzuia!!

  Mara moja nikataka kuchukua hatua....awajibike! Duh! Mkataba kasaini na Kamati ya Shule! Kamati ya shule is NOT a legal entity! It has no powers to contract! Nilipoangalia zaidi, mkataba ni wa mwaka mmoja! Haukusema vitabu vitapelekwa lini! Unamalizika Feb 11 so he still is not late 'technically'!

  Nilipoongea na Afisa Elimu jibu lake 'mh we acha tu jamani, tuna matatizo mengi jamani'....sasa tatizo liko wapi? Hela zipo, mkataba mbovu! Ni uzembe au tatizo? Au uzembe ndio tatizo???

  Kama kamati ya afya tunaongelea afya kinga...usafi wa mazingira! Taarifa ni kwamba kaya elfu 21+ zimekaguliwa! Nikauliza masoko? Hospitali? Misikiti? Makanisa? Hakuna vyoo vya public vilivyotembelewa! Does it make sense???

  Lakini cha kushangaza na kukera ni choo cha halmashauri chenyewe! Ni kichafu na kinatia aibu!! Nikashindwa kujizuia! Inawezekanaje kuongelea vyoo vya wilaya nzima na usafi wakati hicho cha anayeoongea ni aibu!??? Hata hilo tunashindwa!

  Jibu rahisi, mh tutalifanyia kazi mapema!

  Tunashindwa kuweka mipango thabiti ya maendeleo. Elimu ya shule ya msingi tumeidharau. Hatuweki mkazo wa kutosha. Ni nini hii Gurudumu? Kuna haja gani ya kuhangaika na mabarabara na majengo mengine wakati elimu yetu ya msingi ni kituko? Eti naambiwa 'mh hatuna upungufu wa walimu....heri sisi ni mwalimu 1 kwa wanafunzi 45-50. Wengine ni 1 kwa 70..' kwa hiyo sio mbaya! Mwalimu ana vipindi 25 na ni mwalimu mkuu!! Aandae somo, afundishe, asahihishe na afanye kazi ya utawala!

  Tufike mahali tuache kila kitu. Kila kitu tuwekeze kwenye elimu ya msingi na sekondari tu!!

  Bado sijajikusanya mawazo yangu vizuri ila....

  Mapato ni 39+ billion.

  Mishahara ni 22+ billion

  Miradi ni 10+ billion

  Matumizi mengine ni 6+ billion

  Unategemea nini hapo?? Bado natafakari!!
   
 19. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hebu ngoja niende kule kijijini isokami nione kama na wao wanamuamko wenu?
  Je sisi ni representative ya majority ya wa TZ kweli au nikasehemu? Wote humu mnakazi au ajira zinazowafanya muweze kuafford internet communication. Ni asilimia ngapi ya waTanzania wako kama sisi?

  Semeni tu kwamba mabadiliko sio lazima yaletwe na watanzania wooooote, werevu wachache wanaweza. Lakini sio mseme a majority of Tanzanians want change.
   
 20. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa kijijini huko mwanza na unaona kwa macho watu wana matamanio ya ubora wa maisha ila hawajui yatakujaje.
  Wamemchagua diwani wa CUF pamoja na ghiliba za CCM kuwa ni chama cha waislam.

  Ajabu wanalipia sh100 kuingia kwenye banda waangalie taarifa ya habari kwenye tv.

  The country is groaning and yeaning for CHANGE.
  Nobody knows ni lini change itakuja
   
Loading...