Matarajio katika bunge la kumi (10)

wishega

Member
Sep 6, 2010
7
0
Ni matumaini yangu wote tumekuwa mashuhuda wa mabadiliko makubwa ya kisiasa na demokrasia miongoni mwa watanzania kwa kufanya maamuzi sahihi hasa katika nafasi za Ubunge. Tumeweza kuona sura mpya za vijana wengi wakishinda nafasi za Ubunge.

Ninachotarajia ni kuwa sasa tutakuwa na bunge makini,mahihiri na lenye viwango vikubwa vya ubora wa kufanya maamuzi yenye manufaa kwa watanzania wengi na si wachache, ukizingatia kuwa sura zote zinzoingia ni sura zenye nia ya dhati ya kuikomboa nchi yetu ya Tanzania toka katika ufisadi hivyo sitegemei kuona maamuzi yasiyo na masilahi kwa Taifa yakipita bungeni.

Aidha,vijana hawa ni viajana wenye uwezo wa kujenga hoja,kuchanganguwa mambo na pia kuwakilisha mawazo ya wanaowawakilisha na ya watanzania kwa ujumla kwa ustadi wa pekee. Zitto,Lissu,Mnyika,Kafulila,Wenje,Selasini, Mbowe na wengine wengi ni watu mahili sana.

Hivyo kilichobaki sasa ni kupata Spika makini na si Spika gohigohi napenda pia kutoficha hisia zangu kwa kusema Samuel Sitta anafaa kuwa Spika wa Bunge lijalo kwani anaweza.

Vijana katimizeni matarajio ya watanzania waliowachagua.

By Wishega,Mboyi
 
Back
Top Bottom