Matapeli wapo wengi ila babu wa LOLIONDO alitisha

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,288
2,000
ImageUploadedByJamiiForums1400756509.587219.jpg Ambilikile Mwasapile a.k.a Babu akiwa kazini...

Wakuu duniani kuna matapeli wengi sana hata hapa tanzania gazeti la jamhuri lilishawahi kutoa orodha ya matapeli
Na ilikuwa hivi Rashid Ntimizi (mtoto wa waziri wa zamami), familia ya Aurora, Roger David Mawelle, Tambwe Moses, Papa Msofe, John ChizumoNaftari Njoree (Mmasai), David Kazibwe na wengine wengi. Wanatapeli wazungu hadi Sh bilioni
Ila kuna tapeli wa kimataifa huwa watu wanamsahau si mwingine ni BABU wa loliondo Ambilikile Mwasapile
Huyu aliwatapeli watz wengi wakiwemo wanasiasa kama Lowassa,Kikwete,Mrema,mzee Ndesamburo,rais Zuma,Lukuvi,Wasira,na mimi mwenyewe na wengine mtawataja wanajamvi
Kwa maana hiyo ninadiriki kusema hamna tapeli africa mashariki alishawahi kutokea kama Babu wa loliondo kama yupo tuambiane
Nani alipona ukimwi?
Nani alipona kisukari?
Na magonjwa mengine nani alipona?
Kama kuna mtu anaushuuda wake au wa ndugu yake aliyepona aje hapa atueleze
HAMNA TAPELI A MASHARIKI KAMA BABU WA LOLIONDO
 

miku

Senior Member
Oct 24, 2011
149
225
Ili jambo lilitawaliwa na imani zaidi kuliko ujuzi na maarifa ya kibinadamu
 

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,288
2,000
Ili jambo lilitawaliwa na imani zaidi kuliko ujuzi na maarifa ya kibinadamu

Mkuu iwe imani au ujuzi lakini huyu babu stail aliyotumia kupiga watu kiboko
Hatuwezi kumsahau kirahisi rahisi
Leo nasikia anaishi kitajiri lakini dawa haina tena nguvu
Kina msofe watasubiri sana kwa mzee mwaki!
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,198
2,000
ni kutomtendea haki haki kwa kumuita tapeli, wengi wamepona kupitia yeye mimi nina ushuhuda wa ndugu zangu wanne kupona maradhi yao kupitia kikombe chake. matapeli wengi wameishia pabaya babu angekuwa tapeli leo ingekuwa tunaongea mengine BTW watu ndio walimtangaza yeye hakuwahi kujitangaza na malipo yake yalikuwa jero ambapo yeye alichukua mia 2 tu. mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni jamani
 

littleheaven

Member
Jan 9, 2014
34
70
Hao walopona hawakuwa wanaumwa au hawakupma bal walihc kuwa wanaumwa wakaenda kupata kikombe na kujinad wamepona km kwl walkuwa wanaumwa tuambie ugonjwa gan walokuwa wanaumwa! Achen polojo.
 

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,288
2,000
ni kutomtendea haki haki kwa kumuita tapeli, wengi wamepona kupitia yeye mimi nina ushuhuda wa ndugu zangu wanne kupona maradhi yao kupitia kikombe chake. matapeli wengi wameishia pabaya babu angekuwa tapeli leo ingekuwa tunaongea mengine BTW watu ndio walimtangaza yeye hakuwahi kujitangaza na malipo yake yalikuwa jero ambapo yeye alichukua mia 2 tu. mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni jamani

Hata mimi mshanajr nina ndugu wengi tu walienda kwa mzee mwaki ila wote maradhi yao yamerudi pale pale mkuu
Sasa nikikumbuka ule mfumuko wa watu siishi kusema babu alitisha hana mfano wake east africa tena ikiwezekana africa nzima
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom