Matapeli wanapoingia Jeshini kufanya uhalifu, wakapigwa doso (drill) raia msihemke

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
442
1,000
Kijana aliyekamata Dar es Salaam Ni jirani yetu. Taarifa za ndugu zinasema alikamatwa kwa kujifanya afisa usalama Takukuru. Kwa stori walizopewa na jamaa zake baada ya video kuonekana mitandaoni ni kuwa. Jana alipata abiria ampelekea uhamiaji kupata huduma ya passport. Akiwa njia kama kawaida ya tax driver akaongea na yule abiria kumdodosa kisha alipojua abiria ana shida gani akamwambia atamsaidia kwa maelezo kwamba atamlipa kiasi flani ili pasipoti itoke haraka.

Huyo abiria inaonekana ni mtu anajitambua au ana fedha kulingana na umbali aliokodi tax.

Huyu Alex akakajaza fomu za Uhamiaji. Baadaye inasemekana akaendesha gari hadi getini la Uhamiaji na kueleza kwamba anatoka TAKUKURU hivyo akafunguliwa geti na kupaki gari ndani akimwacha abiria wake aingie kivyake. Wanadai watoto wa mjini hii Ni moja ya mbinu kubwa inayotumika kuwatapeli watu, kwamba ukiingia ndani ya geti la serikali unamjengea confidence yule unayetaka kumtapeli.

Kwa ujasiri wa ajabu ndugu na jamaa zake wanaeleza kwamba akusimama kokote bali alikwenda moja kwa moja kwa afisa mmoja mkubwa akaingia ndani ya ofisi yake nakujitambulisha kuwa yeye ni afisa wa TAKUKURU na anaomba mke wake asaidiwe kupata pasipoti. Wakati huo yule abiria yupo nje. Huyo afisa inadaiwa alikubali kumsaidia nakuelekeza apewe huduma. Wakati wanaendelea na huduma baadhi ya maafisa walibaini nyendo zisizo za kawaida wakatamani kuhojiana naye na hii inaelezwa nikutokana na dharau yake kwa maafisa hao wadogo huku akilazimisha mteja wake ahudumiwe nje ya utaratibu.

Wakati wanamhoji yule abiria inasemekana waligusia suala la taarifa mme yule mteja akatoa taarifa tofauti na alizowapa awali Bw. Alex.

Maafisa walipobaini kwamba yule siyo mke wa yule aliyedai ni mtumishi wakatamani kujua ukweli. Alex akachomoka mbio akitaka kutoroka jamaa wakapita naye nakumkamata kisha wakakurupushana naye kijeshijeshi alipoona hali tete ndo akasema yeye ni tapeli si afisa wa Takukuru. Kwa hiyo baada yakula kichapo inaonekana alipewa dhamana ila madreva tax wenzake wanasema gari wameiona Uhamiaji bado kitu ambacho kinaonyesha wapo wanafanya uchunguzi.

Lakini pia tunaomfahamu tunajua zipo nyendo zisizo za kawaida ndani yake, status yake na stori zake Ni tofauti. Haya maisha wameyaiga serikalini hukohuko basda ya wasiojulikana kuwa wengi na vishoka nao wamepata pakuwajambisha Hadi Askari.

Haya mambo yapo sana kila kona kwa sababu watu wasiojulikana wamejivika userikali na wanaweza kufanya lolote. Ukiona raia ana nguvu yakwenda kwenye ofisi za polisi au jeshi akiwa na gari akajitambulisha Hadi afunguliwe geti jua huyo ni mbobezi na tayari ameshawaumiza watu wengi kwa mbinu Kama hizi.

Haya yote ni matokeo ya hofu iliyojengwa na serikali iliyopita kuwafanya hata hao wenye dola wenyewe washindwe kuhojiana wenyewe kwa wenyewe. Huu mtandao ndio tuliokuwa tunasikia watu wanasema flani katapeliwa kwa jina la JK au hata JPM na kesho utasikia wanatumia jina la familia ya Mama Samia kujipatia fedha au hata kuumiza watu.

Lakini pia anayafanya haya kijana ambaye miaka michache iliyopita huku kijijini alikuwa anatuma picha kwa baadhi ya vijana wanaomfahamu akionyesha yupo na shangingi la serikali anaendesha. Je hayo magari ya serikali alikuwa anapewa na Nani? Alikuwa mwajiriwa au alikuwa anatumia mbinu hizo hizo kuwatapeli madereva wa serikali magari na kupiga nayo picha kisha kuwatumia jamaa zake?

Huyu ndugu yetu ametufedheesha sana na hii ndiyo ilinifanya nikaleta hoja kuwa wazazi tufuatilie nyendo za watoto wetu. Mtoto unajua siyo mwajiriwa wa serikali anakuja nyumbani au unamwona kijiweni na gari lenye adhi ya waziri unashindwa kushtuka?

Lakini yapo maswali najiuliza
Ameshawatapeli wangapi?
Amewapatia pasipoti na huduma nyingine watu wangapi?
Gari alizokuwa anapiga nazo picha au marafiki zake wanamkuta nazo alikabidhiwa na Nani?

Abiria wangapi wamewashirikisha madreva tax taarifa zao za Siri nakupelekea wakatekwa au kutengenezewa zengwe la uhalifu?
Hawa wanaojiita watu wa haki mitandaoni mnataka kuwatetea watu wa aina hii kesho wapeleke walipuaji kwenye ofisi zetu za umma ndugu zetu wauwawe kwa tamaa zao zisizozingatia maslahi ya umma?

Ninyi viongozi na Watumishi wa Umma kwanini msijiwekee utaratibu wakutambuana kwa vitambulisho?

Mimi nilipomwona huyu kijana niliwaza kwa sense ya JKT ya miaka hiyo, nikajiuliza waalifu wanawezaje kujipenyeza kwenye majeshi kutapeli bila kubainika?

Yupo ndugu yangu Ni mstaafu wa jeshi namjua, alitapeliwa pensheni yote kwa mbinu Kama hizi na alipata presha akafariki. Haya matapeli tusiyape haki za binadamu Wala haki gani wanapokamatwa kwenye majeshi yetu lazima wabebeshwe dunia wakasimulie na wenzao ili majeshi yetu yawe salama. Tuache siasa this is serious na Waziri wa Mambo ya Ndani toka adharani ukemee huu utapeli na uhalifu unovikaribia vyombo vyako.

Niwapongeze sana waliotukamatia huyu wakora anatufanya tuonekane matapeli mjini. Video imetoa fundisho kwa watu wengi kwamba wasicheze na dola. Natamani kuirudia rudia maana nakumbuka JKT enzi nabebeshwa dunia

PIA, SOMA=>Sheria inawaruhusu Vyombo vya Dola kuwatendea hivi Watuhumiwa?
 

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
11,719
2,000
Nimeiona clip ukiacha mambo ya haki za binadamu wale maofisa ninawapongeza sana yule kijeshi tunasema katolewa DEMO ili wengine wawe na hofu juu ya kupenyeza janja janja zao kwenye ofisi za umma na kwingineko. Ila nimesikitishwa kwa taarifa kuwa maofisa walioshiriki kuwa wameandikishwa maelezo kwa maelekezo ya katibu mkuu, kuwa wamemuadhibu kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,283
2,000
Nimeiona clip ukiacha mambo ya haki za binadamu wale maofisa ninawapongeza sana yule kijeshi tunasema katolewa DEMO ili wengine wawe na hofu juu ya kupenyeza janja janja zao kwenye ofisi za umma na kwingineko.Ila nimesikitishwa kwa taarifa kuwa maofisa walioshiriki kuwa wameandikishwa maelezo kwa maelekezo ya katibu mkuu,kuwa wamemuadhibu kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Sawa wamechukua hatua za awali kumdhibiti mhalifu hayo mengine acha yafuate.... huyo mhalifu ukiona kajiamini hivyo nao wameshughulika nae jua keshawasumbua kitambo... 40 zimetimia sasa wamwangalie vema nyuma yake lazima kuna mtu...
 

Reykijaviki

JF-Expert Member
Aug 25, 2020
388
1,000
Nimeiona clip ukiacha mambo ya haki za binadamu wale maofisa ninawapongeza sana yule kijeshi tunasema katolewa DEMO ili wengine wawe na hofu juu ya kupenyeza janja janja zao kwenye ofisi za umma na kwingineko.Ila nimesikitishwa kwa taarifa kuwa maofisa walioshiriki kuwa wameandikishwa maelezo kwa maelekezo ya katibu mkuu,kuwa wamemuadhibu kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Katibu Mkuu kakurupuka, angewapongeza wale maafisa kwa kazi nzuri ya kumbaini tapeli na kumpa kichapo. Binafsi sioni shida ya ile clip.
 

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
410
1,000
Nimeiona clip ukiacha mambo ya haki za binadamu wale maofisa ninawapongeza sana yule kijeshi tunasema katolewa DEMO ili wengine wawe na hofu juu ya kupenyeza janja janja zao kwenye ofisi za umma na kwingineko.Ila nimesikitishwa kwa taarifa kuwa maofisa walioshiriki kuwa wameandikishwa maelezo kwa maelekezo ya katibu mkuu,kuwa wamemuadhibu kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

Acha umbea waki CDM, toka lini Askari akachuliwa hatua kwa kupambana na waarifu? Usifundishe serikali kazi wanajua namna yakupambana, naona Wambura naye matv kibao. Waalifu wapigwe tu nchi itulie tufanye majukumu yetu.

Limtu limenenepeana kwa fedha za dhulma Hadi linakwenda kuwadindia Askari.....Kwanza angepigwa tu. Ukiangalia ile clip uone hata akitoa machozi maana yake Yale ameyazoea na wangemvua nguo ungekuta lazima ana sugu zakupondwa huko anakofanyia ualify wake......

Wanambembeleza........nilitamani niwepo ningetupa hata jiwe. Mimi namshangaa mtu anamwonea huruma jambaz wakati kila siku mlalamika wamezidi....yaani watu wamekua sugu. Duniani kote hakuna mtu anathubutu kwenda kufanya ualifu Jeshini kwa sababu kule hakuna haki na wakiweka haki wakati Wana maghala ya silaha Basi watakuja waalifu kuchukua silaha wanavyotaka wakiamini hata wakikamatwa watabembelezwa Kama mnavyotaka then watapelekwa mahakamani nakupewa dhamana wakakae uraiani. Huu ujinga wafanye uraiani siyo kwenye vyombo vya usalama na wakikosea wakaweka haki za binadamu kwa waalifu wanaingia kwenye vituo vya polisi, Magereza au jeshi tutaona tutakavyovamiwa. Principle ndogo tu za dunia hakuna haki za binadamu wapigwe tu wajitambue
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
165,163
2,000
Video ninayo ila ni ndefu sana dakika 15 kamili
Baada ya kukamatwa na kukiri utapeli akaambiwa akabidhi vitu vyake vya thamani.. Akakabidhi sh 65,500 akavua mkanda soksi na viatu.

Kisha akaambiwa alale chini, akamwagiwa maji mwili mzima na kuambiwa abingilike kwenye parking ya uhamiaji.. Kichekesho na huruma ni pale alipobadilishiwa zoezi aruke kichura na baadae pushup nusura afe kwa kuhema (ana kitambi)
Kuna kufedheheka duniani lakini ya jamaa hatakaa asahau.
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
7,896
2,000
Video ninayo ila ni ndefu sana dakika 15 kamili
Baada ya kukamatwa na kukiri utapeli akaambiwa akabidhi vitu vyake vya thamani.. Akakabidhi sh 65,500 akavua mkanda soksi na viatu
Kisha akaanbiwa alale chini, akamwagiwa maji mwili mzima na kuambiwa abingilike kwenye parking ya uhamiaji.. Kichekesho na huruma ni pale alipobadilishiwa zoezi aruke kichura na baadae pushup nusura afe kwa kuhema (ana kitambi)
Kuna kufedheheka duniani lakini ya jamaa hatakaa asahau
Akirudia atakuwa na roho ngumu huyo!
 

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
7,692
2,000
Sijawahi kumtapeli mtu na magari nimeeendesha zamani sana, siku hizi ni Bajaj tu sitaki tabu. Nikishika gari ni muda wa Kwenda, kurudi bajaj itanihusu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom