Matapeli Waliofungua Benki Feki Waacha Watu Uganda Wakilia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matapeli Waliofungua Benki Feki Waacha Watu Uganda Wakilia

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Jul 25, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Thursday, July 23, 2009 8:39 PM
  Matapeli wamewaacha mamia ya wakazi wa mji wa Malaba nchini Uganda wakisaga meno baada ya kufungua benki feki na kuitangaza redioni na magazetini na kisha baada ya wiki mbili walitoweka na pesa zote za wateja waliojitokeza. Matapeli wamewaingiza mjini wakazi wa mji wa Malaba nchini Uganda uliopo kwenye mpaka wa Uganda na Kenya baada ya kufungua benki feki iliyoitwa 'Visa Finance Bank' na kisha kutoweka na pesa zote za wateja waliojiunga na benki hiyo.

  Polisi wa Uganda walisema kuwa matapeli hao walifungua benki hiyo wiki mbili zilizopita na waliitangaza redioni na kwenye magazeti wakiwaahidi watu mikopo ya haraka haraka bila masharti magumu.

  Zaidi ya wakazi 204 wa mji huo walijiandikisha kwenye benki hiyo na kulipia shilingi 25,000 za Uganda katika malipo mbali mbali ya kujisajili na benki hiyo. Watu wengine ambao idadi yao haikujulikana walihamishia pesa zao kwenye benki hiyo feki.

  Watu wengi walivutika na kujiunga na benki hiyo baada ya kusikia matangazo redioni na sehemu mbali mbali kuwa benki hiyo inatoa mikopo kwa watu wenye uwezo wa kulipa asilimia 25 ya mikopo yao.

  Matapeli hao baada ya kuona wamepata pesa walizoona zinawatosha walitoweka na kuwaachia ujumbe wateja wao uliosema " Samahani kazi zote za benki zimehamishiwa sehemu nyingine".

  Hadi wakati matapeli hao wanatoweka jumatatu usiku, wateja wa benki hiyo waliwekeza zaidi ya dola laki moja ( Takribani Tsh. Milioni 113) na hakuna mteja hata mmoja aliyefanikiwa kupata mkopo.

  Katika kuonyesha kali ya yote, matapeli hao walitumia cheki feki kununua chakula, kulipia pango la nyumba waliyofungua benki hiyo na pia walitumia cheki hizo feki katika kuitangaza benki hiyo redioni na sehemu zingine.

  Richard Ojore, mmiliki wa jengo ambalo matapeli hao walifungua benki yao alipewa cheki feki ya Shilingi Milioni 9.8 za Uganda kwaajili ya pango la benki hiyo kwa mwaka mzima.

  "Tulitia sahihi mkataba wa mwaka mzima na walinilipa cheki ya malipo ya mwaka mzima" alisema Ojore.

  "Nilipoenda benki nyingine na cheki hiyo ndipo nilipoambiwa kuwa cheki hiyo ilikuwa ni feki".

  "Niliporudi Malaba nilikuta wameishatoweka na kuacha ujumbe wa kuhamishwa kwa tawi hilo" alisema Ojore.

  Hoteli waliyokuwa wakikaa na kula matapeli hao iitwayo Port Spring Villa Hotel nayo ilipewa cheki feki ya Shilingi milioni 1 za Uganda.

  Radio ya Rock Mambo Radio nayo iliingizwa mjini kwa kupewa cheki feki ya Shilingi milioni 4.2 kwa kuitangaza benki hiyo kwa muda wiki mbili mfululizo.

  Baada ya habari za kufungwa na kutoweka kwa wamiliki wa benki hiyo kuzagaa, mamia ya wateja wa benki hiyo walijazana mbele ya ofisi ya benki hiyo wakiwa hawaamini kama ni kweli wameishaibiwa pesa zao.

  Wateja wengi wa benki hiyo walikuwa ni wakulima na wafanyabiashara ndogo ndogo wa maeneo ya mji wa Malaba na miji ya jirani.

  Matapeli hao walibeba na kuondoka na kila kitu chao na kuacha viti, feni na makasha ya kuhifadhia fedha ambayo yalikuwa tupu.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2602802&&Cat=2
   
 2. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #2
  Jul 25, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Duh kweli serikali za kiafika ni kiboko.Jamaa wanafunguaje bank kirahis rahisi hivyo?mhh DECI nyingine hiyo.poleni sana wathirika watukio hilo.
   
Loading...