Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

gilldenu

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
2,914
3,002
Wakuu kwema.

Mambo ya online business kuna page Instagram wanauza iPhone, nikachati na muuzaji anauza simu used kutoka UK nilitaka iPhone 7+ wao wanauza 450,000 nikawaomba wakanipunguzia mpka 430,000 ijumaa ya tarehe 22 nikawatumia pesa kwa tigo pesa wakala.

Mwenyewe anadai duka lipo Zanzibar simu ukisha order inakuja na boat ya mchana kwa maelezo yake. Nilivotuma hiyo pesa aka confirm kwamba kapokea akiniahidi kwamba atanipa namba ya mtu anaefanya delivery huku Dar ndio maongezi yakaishia hapo.

Kila nkimwambia anitumie hiyo namba kimya na kaniblock jamani naombeni msaada nataka niende police je kuna utaratibu gani huko kwa kesi za kutapeliwa mtandaoni?

Naombeni muongozo karibuni.

======
UPDATE:

NOTE: Matapeli hawa hawaruhusu comments kwenye pages zao na wanafanya promotion ya contents zao (Sponsored) katika m

Hizi hapa ni baadhi ya akaunti zinazofanya utapeli Instagram

5D6F27F2-48CD-4B26-AFE8-159887B5BAA3.jpeg

E27E0046-7453-4DDD-84DF-3E750919377E.jpeg

4CAF5547-1A3D-4DF6-A1CD-1B117D4D75D8.jpeg
 
Pole mkuu, kwa ushauri tuu...
Ukishaona Mtu anauza bidhaa hasa electronics Anadai ana Duka na ni nje ya Dar halafu haanzi kwa kutaja exact location Anajinadi kusema popote tunakutumia, Anza kutumia akili yako vizurii....

Wanatumia trick ya nje ya dar hasa zanzibar maana wanajua Ni ngumu kuifuata,
Na anajua wateja wengi wapo Dar, au Ana ndugu Dar, hivyo akikuambia yupo Dar ni simple tuu utahitaji kumuona au kutuma mtu.

Hapo ataanza uswahili..
Huyo ni tapeli, hauzi simu na Asilimia kubwa wapo hapa hapa Dar...

Ila vitu vingine ni kujiongeza tuu, sasa kweli mtu anakuambia Anauza simu, yupo Manyara, Tabora, Iringa(kupatana wamejaa hawa) Ukiangalia Mazingira ni bonge ya Duka, Bei nayo hata ya China haioni ndani....

Kweli kweli kwelii mtanzania mwenzangu Duka la Simu bei chee tena iphones na Macbook za maana likose kote kwa kukaa likae Mara na sumbawanga?

Anyway labda...

Pia hii habari ya mjini ya sasa ya free delivery ndio inawaumiza watu..
Ni nzuri ila kiafrica wengi wana mlengo wao mwingine..

Binafsi hata kama hamna utapeli, sio mpenzi wa biashara za free delivery hasa zile ambazo zinahitaji ukaguzi, bora hizi za kimataifa za kuagiza nje, ila bongo uaminifu bado sana.

Raha ya biashara uone bidhaa, ukague, ulidhike, ulipe uchukue..
Sio ulipe, uletewe, ulazimike kuchukua.

Kama INAWEZEKANA nenda dukani kabisa, kule utakutana na option nyingi, quality tofauti tofauti uchague mwenyewe,
lakini pia kwa usalama na uhakika wa pa kumpata muuzaji endapo itakulazimu baadae...
Tuwe makini, kupunguza Majuto.

Kama una starting point nzuri mfano ushahidi mzuri, mtu wa kukusimamia hili, Ufahamu wa taarifa zake zozote, n.k Basi fungua kesi Msake...
Ila kinyume na hapo utapoteza zaidi, na jinsi utakapo pata shida kumsaka, Ndio uta refusha mda wa Machungu na hasara zaidi.

HAKIKISHA HILI HALITINGISHI IMMUNE YAKO.
 
Wakuu kwema..

Mambo ya online business kuna page Instagram wanauza iPhone, nikachati na muuzaji anauza simu used kutoka UK nilitaka iPhone 7+ wao wanauza 450,000 nikawaomba wakanipunguzia mpka 430,000 ijumaa ya tarehe 22 nikawatumia pesa kwa tigo pesa wakala ...mwenyewe anadai duka lipo Zanzibar simu ukisha order inakuja na boat ya mchana kwa maelezo yake.... Nilivotuma hiyo pesa aka confirm kwamba kapokea akiniahidi kwamba atanipa mamba ya mtu anaefanya delivery huku Dar ndo maongezi yakaishia hapo...kila nkimwambia anitumie hiyo namba kimya na kaniblock jamani naombeni msaada nataka niende police je kuna utaratibu gani huko kwa kesi za kutapeliwa mtandaoni....?? Naombeni muongozo karibuni
Anua tanga.. Pangusa vumbi chapa lapa... Biashara imeisha iyo.. Huko police hutapata msaada wa maana zaidi ya kutolewa upepo zaidi...

Jr
 
Jamaa awa wa Instagram ni matepeli hivyo hivyo na mimi nilitapeliwa 270K TZS nilikuwa nataka kununua laptop wakaniambia nitume pesa nusu kwanza nikatuma laki mbili na nusu.

Nilivyo tuma wakaniambia awawezi kutuma uwo mzigo kwa agent wao eti kwasababu ya corona wana avoid social distancing kwaiyo ni hatari kwa agent wao wakanitaka nimalizie kiasi cha pesa kilicho baki ndyo waitume mimi nikagoma. Then wakani block.

Nimesha potezea coz ni mda sasa lakini siyo mbaya coz nimejifunza kitu. Biashara mtandaoni imejaa utapeli jiahari
 
Pole Mkuu sema ungeanza kuuliza huku Ijumaa hiyo ungepata majibu sema usitume fedha kwa njia hizo mpaka ujiridhishe na usalama wa pesa zako kwanza na pia hizo used nunua ukiiiona maana hata angetuma mbovu bado ungepata hasara.

Na pia ukiwa hela ndogo Kama zangu nunua simu mpya unayoiona jina lolote usiwasikilize wapiga mbiu wa iPhone muda wake ukifika utanunua popote bila hata kuagiza...
 
Jamaa awa wa Instagram ni matepeli hivyo hivyo na mimi nilitapeliwa 270K TZS nilikuwa nataka kununua laptop wakaniambia nitume pesa nusu kwanza nikatuma laki mbili na nusu. Nilivyo tuma wakaniambia awawezi kutuma uwo mzigo kwa agent wao eti kwasababu ya corona wana avoid social distancing kwaiyo ni hatari kwa agent wao wakanitaka nimalizie kiasi cha pesa kilicho baki ndyo waitume mimi nikagoma. Then wakani block. Nimesha potezea coz ni mda sasa lakini siyo mbaya coz nimejifunza kitu. Biashara mtandaoni imejaa utapeli jiahari
Hiviii unaanzaje kuingia king kirahisi hivii????
 
Wakuu kwema..

Mambo ya online business kuna page Instagram wanauza iPhone, nikachati na muuzaji anauza simu used kutoka UK nilitaka iPhone 7+ wao wanauza 450,000 nikawaomba wakanipunguzia mpka 430,000 ijumaa ya tarehe 22 nikawatumia pesa kwa tigo pesa wakala ...mwenyewe anadai duka lipo Zanzibar simu ukisha order inakuja na boat ya mchana kwa maelezo yake.... Nilivotuma hiyo pesa aka confirm kwamba kapokea akiniahidi kwamba atanipa mamba ya mtu anaefanya delivery huku Dar ndo maongezi yakaishia hapo...kila nkimwambia anitumie hiyo namba kimya na kaniblock jamani naombeni msaada nataka niende police je kuna utaratibu gani huko kwa kesi za kutapeliwa mtandaoni....?? Naombeni muongozo karibuni

Muzammil electronics
 
I phone 7plus kwa 450k umewahi ona wapi hyo bei mzee? Hata kama imetumika nje. Ndo ujifunze uache kupenda vya RAHISI kuwa makini next time Mjuba
 
Back
Top Bottom