Matapeli kutumia utambulisho wa vyombo vya dola kunathibitisha udhaifu wa vyombo au mazoea yamezidi?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Sabaya aliwahi kutumia kitambulisho Cha TISS akabainika ila kesi yake ikafutwa akateuliwa kuwa DC

Shinyanga amekamatwa Mwalimu mwenye kitambulisho Cha JWTZ pamoja na official documents za chombo hiki nyeti akituhumiwa kufanya utapeli.

Uhamiaji tumeona hivi karibuni wakitoa adhabu huku wakimtaka mtuhumiwa kujua Serikali ipo macho baada ya mtuhumiwa kuingia kwa wadosi wa ofisi hiyo nakuwatisha ni Afisa wa TAKUKURU.

Polisi Dar walimkamata raia mmoja aliyekuwa anatumia uniform za polisi kutapeli na kujipati fedha kwa wananchi.

Watu hawa wote nikizisoma sheria za nchi haziwatambui kama wahaini badala yake sheria zinazowabana ni laini kiasi kwamba hata hukumu zao zinawavutia kujinoa zaidi.

Je, kwanini watu Hawa wamejijengea hii confidence ya kialifu wakati zamani tulikuwa tunaviogopa na kuvihofia vyombo vyetu?

Lakini kwanini tunawatetea sana Hawa watu hatuoni tunawapa nguvu na kuwafanya wasiviheshimu vyombo vyetu? Huu usugu unaotengenezwa unatokana na msukumo wa kisiasa au wakuu wa vyombo wamepoteza wivu na vyombo hivi?
 
Hii ilitokana na mazoea ya kutishana ambayo wanayo wenyewe watumishi wa vyombo hivyo vya ulinzi na usalama hasa katika awamu iliyopita ambapo vilishamiri sana

Watumishi wa vyombo hivi baadhi yao wanajifanya wababe na kuvunja sheria katika utekelezaji wa majukumu yao na kama wakitakiwa kufuata sheria wanaweza hata kuumiza watu kwa vipigo au kwa silaha na wasiwajibishwe na mamlaka zao za utumishi

Matokeo yake hilo limeonekana kama ndio utamaduni na taratibu zao za kazi kiasi kwamba hata wale watu wenye nia ovu hutumia mbinu hizo wakijua kwamba ukifanya hivyo itajulikana wewe ama ni mjeshi, au polisi, au mslama au mtakukuru. Na wakati mwingine hufanikiwa kutimiza uhalifu wao

Rai yangu ni kwamba, watumishi wa vyombo vya dola wahakikishe wanajenga tabia na utamaduni wa kufuata sheria, kanuni na taratibu zao za kazi ili iwe rahisi kuwatambua na kuwatofautisha na wahalifu wenye nia ovu
 
Back
Top Bottom