Matani

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,329
23,874
Jamani nilipokuwa mdogo hii ndo ilikuwa hobby yangu maana kwa umbo langu dogo sikuweza kupigana ila ukinikosea kidogo..nitakupa neno utakaa kimya mwenyewe!
Najikumbushia tu...(usinichukie...)

Unataka matani..

Nyani Ngabu
, una bichwa kubwa mpaka shuleni ulikuwa unaitwa Headboy! twende twende..
Fidel80, wewe umekonda mpaka ukisimama kwenye ukuta unakaa kama crack...
Mzee Mwanakijiji demu wako amekonda mpaka akivaa t-shirt ya bluu anafanana na sim card ya tiGO..

Asprin
unamashavu kama mimba ya panya..

Na wewe TUKUTUKU uso kama shamba la matuta...

Unataka unataka..

Mwangalie kwanza, wewe Bigirita yaani wewe ni mbaya mpaka hutumia lotion inayoitwa 'why bother!'..teh teh..

Zak wewe ni mweusi mpaka ukirushiwa jiwe linarudi kuomba tochi...
Watu8 wewe ni mshamba hadi mara ya kwanza kupanda daladala ulianza kutandika vitambaa kwenye siti.


PS: On a light touch...
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri tunajaribu kuondoa stress za uchaguzi eeehh, haya bwana taratibu tu usijemtukana mkweo, naskia mpaka vidingi vimo humu JF!!! Sijajua JK na PINDA wanatumia nickname gani bt i think ni moja kati ya ulizotaja hapo juu, Makamba yeye anatumia nickname ya Malaria sugu au ZUBEDA
 
nafikiri tunajaribu kuondoa stress za uchaguzi eeehh, haya bwana taratibu tu usijemtukana mkweo, naskia mpaka vidingi vimo humu jf!!! Sijajua jk na pinda wanatumia nickname gani bt i think ni moja kati ya ulizotaja hapo juu, makamba yeye anatumia nickname ya malaria sugu au zubeda


sema hakyanani!
 
Elli acha kunivunja mbavu bana...so, wakuu wote wamo humu...
Kwanza nlikuwa na moja la malaria sugu wacha nimpe ndo nimuombe msamaha: Una kiuno kidogo mpaka ukijifunga belt ya kijani unakaa taxi za Ilala...

basi wacha niendelee na wewe:
Yaani wewe ni mjinga mpaka ulienda boarding sunday school!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu uzuri wa matani yasifanane na ukweli manake unaweza sababisha mengine humu.

Nilikuwa napita tu jamani................................

Hahah..hapo ndo ukweli ulipo lala..
Na wewe ndugu,
una bichwa kubwa mpaka ukipita town unapita ukifanya psss psss....
 
elli acha kunivunja mbavu bana...so, wakuu wote wamo humu...
Kwanza nlikuwa na moja la malaria sugu wacha nimpe ndo nimuombe msamaha: Una kiuno kidogo mpaka ukijifunga belt ya kijani unakaa taxi za ilala...

Basi wacha niendelee na wewe:
Yaani wewe ni mjinga mpaka ulienda boarding sunday school!
yote tisa kumi hilo hahaaaaaa haaaa haaaaaaaaataaaa uh huu chwaaah......
 

Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom