Matangazo ya wizara afya hayafai

Tujikomboe Finance

JF-Expert Member
May 8, 2013
212
79
Kuna tangazo moja maarufu sana redioni limetolewa na wizara ya afya. Tangazo hilo linahusisha binti anamueleza mamaye kuwa ana uja uzito. Sikumbuki maneno yote lakini nitaandika maneno yenye walakini katika tangazo hilo.

Huyo binti anamueleza mama yake kuwa ANAHISI NI MJAMZITO. Hili ni jambo la upotoshaji kabisa, kwasababu binti alipaswa kumueleza mama yake kuwa AMEFANYA KIPIMO na ni mjamzito. Tangazo hili linalipinga (contradicts) tangazo jingine la wizara ya afya ambalo linahimiza kuwa TUSIHISI KUWA KILA HOMA NI MALARIA bali twenda hospital kufanya VIPIMO. Sasa iweje kwenye malaria, wizara inapromote kutumia VIPIMO, ila kwenye uja uzito wizara ina promote kutumia HISIA.

Tatizo jingine kwenye tangazo hilo ni ile tabia iliyozoeleka kwenye ndoa nyingi za siku hizi ambapo mama mkwe (mama wa wake) wamekuwa wakiingilia, na kuendesha ndoa za mabinti zao (NI TATIZO kubwa). Mama mkwe wengi wamekuwa tatizo kubwa kwenye ndoa nyingi, hawajawaachilia mabinti zao, wanataka waendelee kuwapa maagizo kwenye ndoa zao. Katika tangazo hili, baada ya binti kumueleza mama yake kuhusu huo ujauzito...........ndipo mama mkwe anapotoa maagizo kuwa ''MWAMBIE MUME WAKO'', angalia kwa makini hapa.....mama hajamuuliza bintiye kama ameshamwambia mume wake......... inaonyesha ana uhakika ndio maana anasema straight ''MWAMBIE MUME WAKO''........

Yaani mama mkwe anapewa taarifa kwanza kabla ya mume mhusika............Hii si sawa kwa tangazo ku promote tabia hii kwani ni mwiba kwa ndoa nyingi sana. Lakini hii pia inalipinga (contradicts), tangazo lao jingine ambalo lina himiza wanandoa kukaa pamoja kupanga juu ya uzazi. Tangazo linahimiza kupanga uzazi pamoja, ila matokeo ..... ''alezewe kwanza mama mkwe

Na ndio maana kwenye tangazo jingine la uzazi wa mpango, mama mkwe (baba wa mume) anakuja juu kuwashutumu wana ndoa kwanini hawataki kuzaa mtoto mwingine. Hii inaonekama kama tangazo lina promote wazazi kuingilia wana ndoa kwenye masuala ya uzazi. Ukisikiliza majibu ya wale wana ndoa kwenye lile tangazo hawaonyeshi kumueleza mama juu ya independence yao kama wanandoa kuamua juu ya uzazi wa mpango. Ilitakiwa yule mama aambiwe kwa maneno MAZITO kuwa sio wajibu wake kuwapangia wanandoa lini wapate watoto, maana ndio mazoea ya wazazi wengi kudhani wana haki ya kuwaamulia watoto wao lini wapate watoto......

Nadhani sija over understand
 
Back
Top Bottom