Matangazo ya waganga wa kienyeji ktk magazeti ya udaku kuhusu mapenzi, nguvu za kiume na mali

Changamoto2015

JF-Expert Member
Oct 1, 2012
773
313
Inaashiria baadhi ya wasomaji wa haya magazeti ni wateja wazuri wa hawa wataalamu wa tiba asilia.

Matangazo yanayoshika chati ni pamoja na;
1) Kuongeza nguvu za kiume
2) Kuleta mvuto wa mapenzi
3) Kumrudisha mchumba (hapa nadhani ni kwa penzi lililochuja)
4) Kupata mali au kurudisha mali iliyopotea

Hawa wataalamu wa tiba asili wasingeendelea kutangaza kwa muda mrefu kupitia magazeti haya kama response sio nzuri kutoka kwa wateja wao.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, hlf hayo matangazo yapo pia kwenye miti na nyumba za watu Dsm sanasana.
 
Ndo maana TZ inaongoza kwa imani za kishirikina....haya matangazo mabovu ndo yanapotosha jamii
 
Inaashiria baadhi ya wasomaji wa haya magazeti ni wateja wazuri wa hawa wataalamu wa tiba asilia.

Matangazo yanayoshika chati ni pamoja na;
1) Kuongeza nguvu za kiume
2) Kuleta mvuto wa mapenzi
3) Kumrudisha mchumba (hapa nadhani ni kwa penzi lililochuja)
4) Kupata mali au kurudisha mali iliyopotea

Hawa wataalamu wa tiba asili wasingeendelea kutangaza kwa muda mrefu kupitia magazeti haya kama response sio nzuri kutoka kwa wateja wao.

Kuna moja nimeiona stand ya Daladala-KUFAULU BILA KUSOMA:)
 
haha tunaonekana hatujui kama kuna Mungu muweza wa vyote na Imani zetu ni potofu ndio maana labda.
 
Kwa sasa wanatumia sim za watu kuwatumia ujumbe wa kushawishi kama hivi
IMG_20171206_072904_640.jpg
 
Nimekuwa nikipata ujumbe kama huu kwa mfululizo sasa! Wanakopata namba zangu hata sijui!
 
Umeshasema magazet ya Udaku. Hata wanaonunua ni wale wale wapenda Umbea, majungu, fitina. Halafu tangazo bei ipo chini labda buku 5. Wajaribu the guardian, nipashe, citizen na mwananchi.
 
Back
Top Bottom