Matangazo ya vifo: Mbwembwe Kibao!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,274
Sijui hili limekaaje?

Utasikia Ndugu Deshideshi wa Sehemu fulani, anasikitika kutangaza kifo cha Pangalashaba kilichotokea kwenye Hospitali Kali, mipango ya mazishi inafanywa.

(Mwanzo wa Mbwembwe Hapo):

Habari zimfikie rafiki wa marehemu aliyeko Canada,
Mtoto mkubwa wa marehemu aliyeko Uingereza,
Sijui nani yule aliyeko Ulaya nyingine, na kadhalika.

Je una uhakika hiyo redio unayotangazia msiba wako inafika kote huko?

Kwanini tunapiga sana mikwala wasikilizaji wa matangazo ya vifo?

Tubadilike kidogo tu na tuishi maisha yetu halisi.
 
hapo buji umenena...hasa wale ndugu zangu na mie...sijui huko ulaya nako lazima wasikilize radio one au ni mbwembwe tu tujue marehemu yuko matawi....ila buji KIFI ndo nini?
 
hapo buji umenena...hasa wale ndugu zangu na mie...sijui huko ulaya nako lazima wasikilize radio one au ni mbwembwe tu tujue marehemu yuko matawi....ila buji kifi ndo nini?


ni typing error ndugu yangu.
Nilikuwa namaanisha kifo.
 
Hariri kichwa cha habari mkuu;

Mie mpaka nimeyasusia kabisaa! Najua ndugu yangu akifariki nitafahamishwa kwa njia nyingine! Isitoshe unakuta kiredio chenyewe ni Mbwembwe FM haisikiki hata mikoa miwili! Wanawaacha watu wa jirani ambao wangefika msibani haraka na kutoa msaada (ujuavyo misiba yetu mingi ya kiafrika) wanakurupuka kumwaga mbwembwe kuwakoga wasikilizaji!

Tutajuaje kama ukoo fulani una watoto wengi ughaibuni?
 
Hiyo tisa...........kumi kwenye historia ya marehemu........... we acha..............
 
Si unajua tena "mtajuaje kuwa kuna ndg,UGHAIBUNI" akina siye tunajumuishwa nanukuu ile sauti ya yule mdada... "pamoja na ndugu na jamaa popote pale walipooooo"
 
kweliii mbwembwe zimezidi..yule kule ulaya atasikiajeee???...........wakati kuna ndugu wengi tu hapa tz hawajatumiwa....twajua kuwa watapewa taarifa kwa email au simu walio nje nchi...sio fm radio....za mbwembwe'
 
Familia ya Mama mchungaji Mrs. Dr. Nanihii....
Marehemu alikuwa akifanya kazi ya utendaji mkuu na shirika la UN kitengo cha chakula na kazi kwa miaka zaidi ya ishirini....
Mipango ya mazishi inafanyika hoteli ya Kunduchi beach hotel karibu na nyumbani kwa marehemu!
Kazi ni hapo kwa wafikiwa habari...
lol!
 
Kuna mambo mengi ya kuweza kuwatumia salamu watu wa nje. Mojawapo ni marafiki zake walio ndani ya nchu kuweza kujua jamaa yao amefiwa. Hivyo tusilaumu moja kwa moja bila kujua sababu ya kutuma kwa jamaa wa nje. Pia unajua msiba una mambo mengi, kuchanganyikiwa nako kwaweza sababisha kuandika jina la mtu wa nje, wakati unajua hatosikia. Lakini kuna Radio siku hizi ziko online, hakuna ubaya.
 
Hata kama redio hizi hazisikiki huko ughaibuni, inawezekana mtu yeyote aliyepo nchini akawa na mawasiliano na hao wa ughaibuni baada ya kusikia redioni jamaa wa ughaibuni akitajwa kuwa kafiwa anaweza akamtaarifu kwa njia yoyote ile. Licha ya kuwa kuna mbwembwe katika matangazo haya lakini sometimes kuna ukweli...... mtu kama kweli yupo Marekani asitangazwe?????
 
Very good observation mkuu... sijui ni masifa au ignorance??
 
Bujibuji fahamu kuwa dunia imekuwa kijiji kwa sasa given the globalisation and its contents including ICT!

Sasa unapotangaza kifo na kama ninamfahamu marehemu au huyo ndugu yake na vizuri kama nina mawasiliano naye naweza hata mimi mtu wa pembeni nikamjulisha through Communication (phone, internet and the like). Kwa hiyo wanaotangaza matangazo yote na wakiweka pia walio nje ya nchi hawakosei. Si lazima asikilize Radio One, Tumaini, Maria Upendo au TBC Taifa na nyinginezo ndipo apate taarifa!!! Lo!!!
 
I dont mean to segregate,lakini Wachaga wanataja hadi vyeti vya mahudhurio (certificates of attendance) za semina, kozi, kongamano na workshop katika historia fupi ya marehemu..huh!
 
I dont mean to segregate,lakini Wachaga wanataja hadi vyeti vya mahudhurio (certificates of attendance) za semina, kozi, kongamano na workshop katika historia fupi ya marehemu..huh!

Ni kweli kabisa,

sasa kuna ya "mipango ya mazishi inafanyika chapombe bar" ---yani hata majumbani sasa hamna, watu wakutane kwenye pombe tu!!
 
I dont mean to segregate,lakini Wachaga wanataja hadi vyeti vya mahudhurio (certificates of attendance) za semina, kozi, kongamano na workshop katika historia fupi ya marehemu..huh!
Umeshawahi kusikia historia ya marehemu wa kihaya................ utajibeba........... HISTORIA imejaaa vyuo vikuu vya primary school............... historia yote NSHOMILE tupu............mweeeeeeeh
 
Si unajua tena "mtajuaje kuwa kuna ndg,UGHAIBUNI" akina siye tunajumuishwa nanukuu ile sauti ya yule mdada... "pamoja na ndugu na jamaa popote pale walipooooo"

We acha tu; ukibahatika kuingia kwenye hiyo listi lazima uwe na title flani

Dr......wa.....ambapo ni mji ama sehemu hiyohiyo ulipo msiba!:D
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom