Matangazo ya TV kutoka analogue kwenda digital

Mu-Israeli

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
2,454
975
Wana - JF,
Tunajua kuwa kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Tanzania itabadilisha mfumo wa urushaji wa matangazo ya TV toka analogue kwenda digital kuanzia 31st December 2012.
Sasa, mimi naona kuwa muda umeisha, na TCRA haitoi elimu na matangazo ya kutosha kuhusu swala hili.
Wakati fulani TCRA walisema kuwa watu wanatakiwa kununua ving'amuzi ili wapate matangazo ya digital TV.
Nimezunguka madukani kuulizia ving'amuzi vya TV, mpaka sasa nimekutana na ving'amuzi vya StarTimes na Easy TV tu.
Ving'amuzi hivi vyote ni vya TV za kulipia matangazo ya TV kwa mwezi (usipolipia huoni matangazo).
Sasa hii ina maana kuwa watanzania wanalazimika kulipia matangazo ya TV kwa sababu ya kubadilika kwa mfumo wa TV kwenda digital !!
Kwenye maduka niliyotembelea sijaona ving'amuzi ambavyo havitahitaji kulipia matangazo ya TV, yaani ving'amuzi vitakavyoshika matangazo ya digital TV bila ya kulazimika kulipa malipo ya kila mwezi.
Wana-JF, naomba tuelimishane kuhusu swala hili ili tusije kujikuta tunakwama kupata matangazo ya digital TV ifikapo tarehe 31st December 2012.
Nawasilisha, na naomba maoni na michango yenu.
 
Ngoja waje kutujuza hApa, je na sisi wa mbali na mijini tunaotumia madishi makubwa itakuwaje?
 
Mkuu uliulizia bei hivyo ving'amuzi kwanza..?

Bei ya ving'amuzi vya StarTimes ni sh. 39,000 tu. Kinachokera hapa ni yale malipo ya kila mwezi !!
Mimi ninachouliza ni kama sasa tunalazimika kulipia matangazo ya TV kupitia Startimes na Easy TV ??
Yaani, hamna tena matangazo ya TV ya bure kwa station kama ITV, DTV, TBC, n.k. ????
 
Ngoja waje kutujuza hApa, je na sisi wa mbali na mijini tunaotumia madishi makubwa itakuwaje?

Kwa wanaotumia madish ( aka 'ungo'), hamtakuwa na mabadiliko yoyote.
Dish Tv ni digital, hivyo kwenu ninyi mtaendelea na kupata matangazo kama kawaida.
 
Pamoja sana mkuu....

Kazi kwetu sisi ambao hatuna 'ungo' !!
Mpaka sasa sijaona decoder ambazo hazitahitaji kulipa malipo ya kila mwezi (monthly fees).
Kila duka ukiuliza unaambiwa kuna decoder za Startimes na Easy TV tu.
Naona swla la kuhamia digital limekuwa gumu kwa Tanzania.
 
Bei ya ving'amuzi vya StarTimes ni sh. 39,000 tu. Kinachokera hapa ni yale malipo ya kila mwezi !!
Mimi ninachouliza ni kama sasa tunalazimika kulipia matangazo ya TV kupitia Startimes na Easy TV ??
Yaani, hamna tena matangazo ya TV ya bure kwa station kama ITV, DTV, TBC, n.k. ????

Wanachosema wenyewe ni kwamba ukiwa na ving'amuzi zile local channels zitaonyeshwa bure hata kama salio limeisha kwenye king'amuzi.. Ila kwa nyingine za nje na zile za kibiashara hapa nchini ndo za tutalipia.. Swali uzuri na quality za hizo channels zinafidia thamani halisi..? Kwa mfano Star Times wana channels za ajabu ajabu ambazo kuziona zote ni Shs. 36,000/=.. Zina thamani hizo..? channels za kifaransa.. kichina.. yaani...!
 
Hata mimi nilimsikia ofisa wao mmoja (Mr. Mungi kama sikosei) alisema hivyo.
Ila mimi nina king'amuzi cha Easy TV, usipolipa huoni chanell zote !! Hata ITV houni !!
Hapo ndipo nilipokwama mimi. Sijui kwa Startimes wanakuwaje pale sasio linapokwisha kwenye king'amizi.
 
Bei ya ving'amuzi vya StarTimes ni sh. 39,000 tu. Kinachokera hapa ni yale malipo ya kila mwezi !!
Mimi ninachouliza ni kama sasa tunalazimika kulipia matangazo ya TV kupitia Startimes na Easy TV ??
Yaani, hamna tena matangazo ya TV ya bure kwa station kama ITV, DTV, TBC, n.k. ????
Kwa ninavyoelewa mimi ukiwa na hizo decoder, zile 'public TV channels' (kama hizo ulizoziorodhesha) itakuwa ni bure. Hata kama haulipii ile fee ya kila mwezi utaendelea kuziona hizo channel
 
Channel za bongo ni bure,.hutatakiwa kulipia.Ila nadhani kukwepa ukiritimba jipigepige upate ungo!.

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 
Kwa ninavyoelewa mimi ukiwa na hizo decoder, zile 'public TV channels' (kama hizo ulizoziorodhesha) itakuwa ni bure. Hata kama haulipii ile fee ya kila mwezi utaendelea kuziona hizo channel

Hata mimi nilimsikia ofisa wao mmoja (Mr. Mungi kama sikosei) alisema hivyo.
Ila mimi nina king'amuzi cha Easy TV, usipolipa huoni chanell zote !! Hata ITV houni !!
Hapo ndipo nilipokwama mimi. Sijui kwa Startimes wanakuwaje pale sasio linapokwisha kwenye king'amizi.
 
change ya kwenda digitali maana yake stesheni zote ni kulipia bila king`amuzi hata taarifa ya habari local huoni. kwishnee
 
ifikapo dec 31 mitambo yote ya analogue itazimwa, tutaanza kutumia digital,bei ya decorder Inatofautiana toka 48000 Startime mpaka 132000 zuku, pia kuna decorder za ting,easy tv, dstv, coconut(zenji), na mpya kabisa ya btl ambavyo haijaingia sokoni, hawa wote watatakiwa kuonyesha local channels bure ili hata asiye na uwezo aweze kupata habari ila kununua king'amuzi ni lazima, maendeleo pia yana gharama zake, wale wajasiliamali wa antenna za tube lights wafikirie ishu nyingine sasa maana antenna hizo zitakuwa hazina kazi tena
 
Ngoja ni wasiliane na ndugu zetu WACHINA, bilashaka tutapata shuluhisho mapema iwezekanavyo!
 
change ya kwenda digitali maana yake stesheni zote ni kulipia bila king`amuzi hata taarifa ya habari local huoni. kwishnee

Naona muelekeo ndio huo. Labda jamaa wa TCRA watufafanulie zaidi, au mtaalam yoyote anayefahamu swala hili atujulishe.
Mimi hayo yamenikuta kwenye EasyTV. Jamaa wanakata matangazo yote pale salio linapokwisha kwenye king'amuzi.
 
Hata mimi nilimsikia ofisa wao mmoja (Mr. Mungi kama sikosei) alisema hivyo.
Ila mimi nina king'amuzi cha Easy TV, usipolipa huoni chanell zote !! Hata ITV houni !!
Hapo ndipo nilipokwama mimi. Sijui kwa Startimes wanakuwaje pale sasio linapokwisha kwenye king'amizi.

Mkuu kwa sasa ucipolipa huoni zote kasoro TBC.. Wanamaanisha ifikapo January mosi mwakani ndio utaratibu wa kuona bure local stations utaanza..
 
Kama kuna mtu yoyote anayefahamu vinapo patikana ving'amuzi ambavyo havitahitaji malipo ya kila mwezi atujulishe.
 
Mkuu kwa sasa ucipolipa huoni zote kasoro TBC.. Wanamaanisha ifikapo January mosi mwakani ndio utaratibu wa kuona bure local stations utaanza..

Okay, kama ni hivyo itakuwa sawa.
Ila nakumbuka ofisa wa TCRA alisema wakati fulani kuwa hata sasa inatakiwa waruhusu chanel za bure bila malipo.
 
Mimi sikatai kuwa tusihamie kwenye mfumo wa digitali kama nchi wanachama walivyokubaliana.Ila kwa Tanzania suala hili limekuja kibiashara zaidi na viongozi wa mamlaka husika wamekuwa kama kipofu kaona mwezi juu ya suala hili kila mmoja anataka amaliziepo matatizo yake sitashangaa kuona kampuni zinaanzishwa zinarusha chaneli nne tu na zenyewe zinatakiwa zilipiwe.Wanakwenda kututoa kwenye mfumo wa geuzia mjini sasa wanatupeleka kwenye geuzia Kisarawe.
 
Back
Top Bottom