Matangazo ya TV kutoka analogue kwenda digital

Hata mimi nilimsikia ofisa wao mmoja (Mr. Mungi kama sikosei) alisema hivyo.
Ila mimi nina king'amuzi cha Easy TV, usipolipa huoni chanell zote !! Hata ITV houni !!
Hapo ndipo nilipokwama mimi. Sijui kwa Startimes wanakuwaje pale sasio linapokwisha kwenye king'amizi.

mie ninacho cha star times, salio likiisha TBC inabaki lakini zingine zote hakuna kabisa, na cha ajabu wanatuambia local channel kama ITV,CHANNEL TEN,STAR TV,EA TV zitaonekana mbona hadi sasa hakuna au muda bado?
 
tunataka kwenda na wakati lakini hatutaki gharama za kwenda hivyo- jamani tukubali ukweli bure sasa haipo
hivi vituo vyetu vya tv havitengenezi faida kama tunavyofikiria kwa sababu matangazo ya biashara siyo mengi sana kuweza kuhimili gharama za uendeshaji.
Wa TZ ni watu wa ajabu sana hasa wa mijini kwani wanalia maisha magumu lakini ofa za bia watoa, michango ya harusi wanatoa, kuhonga warembo wanatoa lakini inapofika vitu kama tv tunaona taabu tunataka vya bure.
cha msingi zaidi aidha nunua dish au king'amuzi au kwa vile wengi jioni wako sitting room za nje basi kuko kuna tv pia.
 
Wana - JF,
Tunajua kuwa kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Tanzania itabadilisha mfumo wa urushaji wa matangazo ya TV toka analogue kwenda digital kuanzia 31st December 2012.
Sasa, mimi naona kuwa muda umeisha, na TCRA haitoi elimu na matangazo ya kutosha kuhusu swala hili.
Wakati fulani TCRA walisema kuwa watu wanatakiwa kununua ving'amuzi ili wapate matangazo ya digital TV.
Nimezunguka madukani kuulizia ving'amuzi vya TV, mpaka sasa nimekutana na ving'amuzi vya StarTimes na Easy TV tu.
Ving'amuzi hivi vyote ni vya TV za kulipia matangazo ya TV kwa mwezi (usipolipia huoni matangazo).
Sasa hii ina maana kuwa watanzania wanalazimika kulipia matangazo ya TV kwa sababu ya kubadilika kwa mfumo wa TV kwenda digital !!
Kwenye maduka niliyotembelea sijaona ving'amuzi ambavyo havitahitaji kulipia matangazo ya TV, yaani ving'amuzi vitakavyoshika matangazo ya digital TV bila ya kulazimika kulipa malipo ya kila mwezi.
Wana-JF, naomba tuelimishane kuhusu swala hili ili tusije kujikuta tunakwama kupata matangazo ya digital TV ifikapo tarehe 31st December 2012.
Nawasilisha, na naomba maoni na michango yenu.

watanzania wengi watalazimika kuwa na deki kutazama filam watakosa matangazo ya moja kwa moja kwa sabab yamalipo yakila mwezi,viongozi hawawajui watu wao kipato.pengine tunategemea fikra za ng'ambo,
 
Wacha tusubiri, ila mi nadhani ni poa tu kwakuwa local channels zitakuwa bure, isipokuwa zile za nje. Ila ni vema TCRA wakatoa mwongozo kwa makampuni ya ving'amuzi watuwekee au washindane kwa kuwa na channel za nje zenye mvuto, mfano STARTIMES kuna channel za kizushi tu hazina mvuto kwa mazingira ya Kitanzania.
 
Wana - JF,
Tunajua kuwa kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Tanzania itabadilisha mfumo wa urushaji wa matangazo ya TV toka analogue kwenda digital kuanzia 31st December 2012.
Sasa, mimi naona kuwa muda umeisha, na TCRA haitoi elimu na matangazo ya kutosha kuhusu swala hili.
Wakati fulani TCRA walisema kuwa watu wanatakiwa kununua ving'amuzi ili wapate matangazo ya digital TV.
Nimezunguka madukani kuulizia ving'amuzi vya TV, mpaka sasa nimekutana na ving'amuzi vya StarTimes na Easy TV tu.
Ving'amuzi hivi vyote ni vya TV za kulipia matangazo ya TV kwa mwezi (usipolipia huoni matangazo).
Sasa hii ina maana kuwa watanzania wanalazimika kulipia matangazo ya TV kwa sababu ya kubadilika kwa mfumo wa TV kwenda digital !!
Kwenye maduka niliyotembelea sijaona ving'amuzi ambavyo havitahitaji kulipia matangazo ya TV, yaani ving'amuzi vitakavyoshika matangazo ya digital TV bila ya kulazimika kulipa malipo ya kila mwezi.
Wana-JF, naomba tuelimishane kuhusu swala hili ili tusije kujikuta tunakwama kupata matangazo ya digital TV ifikapo tarehe 31st December 2012.
Nawasilisha, na naomba maoni na michango yenu.

Elimu zinatolewa kila siku sasa wewe utawasikia wapi tcra wakati huna muda wa kuangalia star tv,itv na tbc upo unatizama ng'ari ng'ari clouds tv? Zipo local channels 5 ambazo zitapatikana free sio za kulipia, itakua ni itv,star tv,tbc,channel ten na eastafrica tv nyingine zitalipiwa! Mimi natumia star tym sijalipia muda ila naziaacces izo chanels
 
Time will tell! Tarehe 31 sio mbali ni kiasi cha kusubiri na kuona! Sipati picha uswahilini itakuaje, ina maana mapaa ya nyumba yatakua yamejaa nyungo! Huyu zuku,startimes,easy tv,dstv na mengine..
 
Elimu zinatolewa kila siku sasa wewe utawasikia wapi tcra wakati huna muda wa kuangalia star tv,itv na tbc upo unatizama ng'ari ng'ari clouds tv? Zipo local channels 5 ambazo zitapatikana free sio za kulipia, itakua ni itv,star tv,tbc,channel ten na eastafrica tv nyingine zitalipiwa! Mimi natumia star tym sijalipia muda ila naziaacces izo chanels

Asante sana Sixgates,
Kama Startimes wameshaweka hizo channels, basi safi kabisa, Maana kabla ya hapo waliweka TBC1 pekee.
 
Back
Top Bottom