Matangazo ya TBC jana (Sherehe za Uhuru) utumbo mtupu, yachemmsha vilivyo!

kkarumekenge

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,708
1,026
Jana (Desemba 9,2013) televisheni yenu, TBC ilitoa mpya.

1. Kwanza kama watangazaji hawakujiandaa basi hawajui lolote kuhusu historia ya Uhuru wa Tanganyika. Kulikuwa na makosa yaliyotokana na kutokujua walichokuwa wakisema mengi na ya ajabu. Bila haka watangazaji hao ni matunda ya elimu ya Mungai.

2. Itakumbukwa kwamba TBC hiyo hiyo iliwai kuzusha janga la kutangaza ati Wakristo ni wengi kuliko Waislamu. Ikaomba radhi. Jana, katika kile kicahoonekana ni kutaka kuwafurahisha Waislamu ilikuja na mpya. Kwa mara ya kwanza TBC iliwatambua ndugu wawili, Abdul Wahid Sykes na Ally Sykes katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Ati hapo walikuwa wanataka kuwafurahisha Waisamu. Ovyo kabisa na aibu kwao.

3. Kama kwamba haikutosha ikatangazwa kwamba wamissionari wa Kikatoliki ndio walimpa tiketi Nyerere kwenda UNO. Ovyo kabisa, yote ikiwa ni kuhangaika kutaka kubalance utumbo wao.

Yote haya ya nini?
 
tbc nikitu gani hicho? bado huwa unaangalia tbc? utakufa na presha mkuu, tafuta tv nyingine za maana au bora uangalie katuni kuliko tbc
 
Na Kikwete akasema" kama chama chako umekianzisha juzi unapaswa kuikubali historia uliyoikuta"(sijui alikuwa na maana na mantiki gani)......kwenye historia hiyo akina Sykes hawamo!
 
Ndio kwanza tunaanza kuyasikia majina haya.
TBC sasa naanza kuweka rekodi ya historia sawa pia watu walikuwa hawambiiwi kuwa Kanisa katoliki lilimlipia Mwalimu Nyerere safari ya UNO sijui ilikuwa inaogopwa kitu gani? badala yake ilikuwa inasema wafadhili walikuwa akina Mzee Rupia na wengineo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom