Matangazo ya sigara

Jewel

Senior Member
May 1, 2008
176
62
[MPOOOOOOOOO!!!!

TANZANIA: Baada ya kupitishwa sheria ya kuzuia uvutaji sigara migahawani na hotelini, Serikali iliamuru kila wenye migahawa au hoteli kuweka tangazo la sheria hiyo, mambo yalikwenda kama ufuatavyo:

MATANGAZO:

Mgahawa wa Msomali: Habana kufuta dumbago habah,
kama nafuta dumbago haba serkali atashkuwa hatwa mkali
kabeisa.

Mwarabu: Habana kufuta mtumbatu ndani ya myumba hii, mtu ukufuta mtumbatu haba tabigwa kwa kishwa yake halafu tabelekwa kwa bolis!

Jaluo....... Ni makufuru kuvuta singara kipande ii. Kama we nakamatwa inavuta singara kipande iii tapelekwa direct kwa prison.


Mhindi....Serkali sema pana buta sigara apa. basi watu ote pana buta sigara apa!


Makonde; Hailuuchiwi kubuta chigala apa otelini. Ukibuta chigala apa utapigwa nchale na kupelekwa chelikalini!

Msukuma: Inakatazwagwa kuvutaga masigala apa. mtu akivunja hili lishelia atapelekwa kwa mwanagwa jitabu.

Mpemba. Sigara zeshakatazwa kuvutiwa humu ngahawani hivo, na msifanye nchezo, Bwan Juma ni nkali atawatia jela wabishao na atawatoa kwenye CUF!

Hoteli ya mwana CCM:
Kufatana na sababu zisizoweza kuzuilika, serikali imechukuwa hatua nyeti ya kupinga uvutaji wa sigara kidamnasi ya watu, migahawani na mahotelini. Pia imeelezwa kinagaubwaga kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka sheria hii. Wahudumiwa wote wanapaswa kuzingatia amri hii ili kuepukana na kile kinachojulikana kama mkono wa sheria.
 
hapo kwa mwana CCM hakuna action ni bla bla tuu maneno mengi bila vitendo
 
CCM si unajua zao....

Serikali ipo makini kuangalia mchakato wa kupunguza kama sio kumaliza kabisa matumizi ya sigara hadharani...ni muhimu kwa watu kujua kuwa mchakato huu unafanywa na watu wenye weledi mkubwa sana katika nyanja ya afya na utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi...hivyo basi katika kutekeleza hili tunaomba watu wote wafatilia angalizo hili muhimu!!....tunajua watanzania ni wavumilivu na wanaelewa dhamira ya serikali ni kuona kila kitu kinaenda sawa.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom