Matangazo ya makampuni ya simu kwenye simu ya mteja ni kero

53930

Member
Jan 20, 2011
65
21
Makampuni ya simu za mkononi yanatabia ya kutuma matangazo yao kwenye simu za wateja. Sio watu wote wenye simu wanapenda miito ya simu au hudumafulani wanazotangaza kupitia sms na kuingia kwenye simu za wateja. Binafsi zinanikera sana hizi sms kwani hawanilipi chochote kwa promo zao nikujaza nafasi kwenye simu tu. Matangazo yao wapeleke kwenye radio, tv, magazeti, mitandao ya kijamii, mbao za matangazo nk. Ni kero kwani hapiti siku bila kutumia sms promo ambazo zihitaji.
 
duh huwezi kuamini mpaka huku jf yapo kama unatumia simu some times yanakuzuia hata kuchangia
 
Mie sipendi kama nini wakati fulani mtu uko njiani na chombo cha usafiri unafuatilia mpango wa fedha ukiwa speed 100 unasikia mlio wa sms unapaki pembeni ukidhani ni ujumbe toka kwa mtu unae mfuata. Unapofungua ujumbe tu unaona promo za mitandao unatamani ubamize simu barabarani baadae unagundua kuwa hasara itarudi kwako unaishia kusonya tu.
 
Sms ndo zinakeraa,na smtym hadi wanapiga kabisa ,ukijiunga kifurushi ndo uwiii ...usiombe sasa uwe mikao ya kusubiri msg muhimu unaweza tupa kisimu kwa hasira
 
Ni kweli kabisa mkuu sms inaingia usku wa manane unaamka kuangalia unakuta ni promo zao..inaboa sana
 
Back
Top Bottom