Matangazo haya - jiji wamelala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matangazo haya - jiji wamelala

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Yona F. Maro, Aug 27, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 27, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  MATANGAZO HAYA VIPI JIJINI

  Ndugu wananchi

  Kama kuna mtu leo amepita barabara ya bagamoyo leo , kuna kitu cha ajabu pale Kituo cha Mafuta bamaga nacho ni Lile Tangazo la kisasa kwenye gari , toka kampuni ya Mile Stone , ule mwanga wa tangazo lile ni mkali sana nilipofika pale nilishtuka sana macho yangu yaliumia , nikafikiria je wazee ambao macho yao sio mazuri sana inakuwaje haswa wanaoendesha magari ? usalama wa waendesha magari pale unalindwaje ? Hivi jiji limekubaliana na watu hawa kuweka matangazo yao popote bila kufanya utafiti wa kutosha kuhusu athari zake mbali mbali ?

  Lile tangazo liko karibu na TBC1 , ITV nimeshangaa hata katika taarifa zao za leo usiku hawajagusia jambo hili , hata kwenye vipindi mbali mbali vya usalama barabarani watangazaji hawaongelei suala hili la matangazo ya mwanga .

  Naamini wahusika watafanyia kazi tatizo hili ili huko mbeleni lisije kupoteza maisha ya watu kwa ajali zinazosababishwa na mwanga ule .

  Ila kama wakiendelea na tabia hizi basi usishangae siku moja kukuta tangazo juu ya taa za kuongozea magari , kama lile lilopo Benjamin mkapa towers linalotazamana na Kituo cha Mabasi , Mimi naona ni kosa Ile sio sehemu ya Tangazo , matangazo yawekwe angalau sehemu tulivu

  Tusiweke matangazo kwa kuiga miundombinu yetu haijaandaliwa kwa ujio wa aina hii ya matangazo bado , hata jamii inapaswa kuelezwa , kufundishwa na kuelewa kisha wakubali wenyewe
   
 2. K

  Konaball JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Lingekuwa Tangazo linahusiana na UFISADI wangekuwa washatangaza kwenye Taarifa ya Habari zao
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Sijaona tatizo na hilo Tangazo,

  Shy,

  When did you last visit the "eye-clinic"? If not very recently you may need to see the optician ASAP.

  Matangazo (Billboards) lazima ziwe zinalazimisha wananchi kulitazama na sio "eyesore"!
   
Loading...