Matamshi ya viongozi wetu....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matamshi ya viongozi wetu.......

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kidudu Mtu, Dec 4, 2009.

 1. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwa najiuliza...hivi kauli za baadhi ya viongozi wetu zina ukweli ndani yake au ni kauli za kulewa madaraka?

  Matamshi ya Waziri Ghasia yasababisha miguno  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, jana aliibua hisia na kujikuta akizongwa na miguno na minong’ono kutoka kwa washiriki wa kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), jijini Dar es Salaam, iliyoashiria kupinga kauli yake iliyotafsiriwa kuwa ni dharau kwa wananchi maskini.


  Hali hiyo ilimkuta Waziri Ghasia alipokuwa akizungumza kuchangia mjadala wa mada ya “Hoja kuhusu watu” na kujikuta sauti yake ikimezwa na miguno na minong’ono, iliyozizima karibu ukumbi mzima wa Karimjee na kusababisha washiriki kutotilia maanani mchango wake. Mada hiyo iliwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MNF, Joseph Butiku, katika kongamano hilo.
  Waziri Ghasia, ambaye aliomba kuchangia kama mwananchi na si kama mbunge wala waziri, alianza kwa kuwashangaa watu, ambao kwa zaidi ya miaka 48 ya uhuru hawajajipatia nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  “Kama Watanzania ilitakuwa kila mtu aipate Katiba. Ni kwa vipi mpaka leo mtu bado hajaipata Katiba wakati mikanda ya ki-Nigeria na magazeti ya udaku ananunua,” alisema Waziri Ghasia.
  Baada ya kukosoa hilo, Waziri Ghasia alizungumzia nukta nyingine kumjibu mmoja wa washiriki, ambaye katika mchango wake alihoji kuhusu maendeleo duni yaliyopo nchini.


  Waziri Ghasia alisema hivi sasa kuna maendeleo makubwa kulinganisha na hali iliyokuwa zamani. Alisema anakumbuka wakati alivyofaulu mtihani ilikuwa shida sana kwa baba yake kuweza kumnunulia viatu aina ya ‘raba’ na kandambili walikosa Mtwara yote na kwa hiyo, ikabidi avae viatu vya katambuga.


  “Lakini leo kama unatembea barabarani, kama umevaa kandambili, ikakatika, unaweza kumtuma mtu akakununulie popote,” alisema Waziri Ghasia.
  Aliongeza wakati huo walikuwa wakisafiri kwa meli, huku wakigombea usafiri wa ndege kama daladala, lakini hivi sasa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam wanasafiri kwa saa chache.


  Waziri Ghasia alikwenda mbali zaidi na kusema kwamba, kutokana na maendeleo yaliyopo: “Sasa hivi hata watoto wangu hawajui chawa.”
  Kauli hiyo ilisababisha ukumbi mzima kuzua miguno kupinga kauli yake hiyo, huku baadhi yao wakisikika wakisema, watoto wake hawajui chawa kwa vile yeye ni waziri, lakini watoto wa maskini hadi leo wanawajua chawa.
  Hali hiyo ilidumu kwa dakika zaidi ya moja, huku Waziri Ghasia akiendelea kuzungumza bila washiriki kumsikiliza.


  Hali hiyo ilimfanya Kaimu Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Hashim Mbita, kuingilia kati na kuwatuliza bila mafanikio na kumfanya Waziri Ghasia kushindwa kuendelea na kutamka: “Naona watu wamechoka, wanahitaji chakula.”


  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...