BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,144
Na Waandishi Wetu
Mwananchi
KITENDO cha Spika wa Bunge Samwel Sitta kumkataza Naibu Spika wake Anna Makinda kusimamia mijadala mizito inayohusu ubadhirifu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na ule wa utata kuhusu tenda iliyotolewa kwa kampuni ya kufua umeme ya Richmond Development Limited kimeibua maswali kadhaa kutoka kwa baadhi ya wananchi, huku kukiwa na hoja kuwa Spika Sitta huenda ana jambo analolificha.
Sitta jana aliliambia gazeti hili kuwa, hakuna kifungu chochote kinachombana Naibu Spika kusimamia mijadala mizito lakini ni busara tu za ofisi yake kuona mambo makubwa yanabaki kusimamiwa na yeye kwa kuwa ndiye atakayehusishwa na mabaya au mazuri kuhusu mambo yote yanayofanyika Bungeni.
"Mimi ndiye ninayetukanwa kwa kila jambo linalotokea ndani ya Bunge. Hata Rais anapokuwa nje ya nchi Makamu wake hawezi kuamua mtu kunyongwa! Kuna mambo ambayo lazima yanisubiri na sio kama mnavyodhani kuwa kuna mgongano kati yetu," alisema Sitta na kuongeza kuwa;
"Hata muda nitakaokuwa nje bado hauwezi kuathiri hoja hizo kujadiliwa nikiwepo. Kwa taratibu zetu huwa tunaanza na miswada kwanza na bado ipo mingi. Hili jambo naona liko wazi tu na hakuna lolote linalofichwa," alisema.
Mhadhiri kutoka katika kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu Dar es Salaam Dk Sengondo Mvungi aliliambia gazeti hili kuwa, kilichofichika ndani ya maamuzi hayo ya Sitta huenda ikawa ni maangamizi kwa chama chake kufuatia kuwepo kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiteto.
Dk Mvungi alisema, wakati spika Sitta anarejea kutoka hiyo ziara yake ya Marekani kwanza ndio kampeni zitakuwa zimeshika kasi katika jimbo la Kiteto, hivyo kwa yeye kuruhusu agenda hizo mbili kujadiliwa kipindi hicho ni wazi anakifunga goli chama chake bila kwa kujua ama kutokujua.
"Suala hilo kujadiliwa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Kiteto litatoa mwanya mkubwa wa wapinzani kukimaliza Chama cha Mapinduzi, maana zitatumika takwimu hizo hizo anazozilinda spika kuimaliza CCM kwa wananchi," alisema Dk. Mvungi.