Matamshi haya Pinda ni ya kukwepa wajibu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matamshi haya Pinda ni ya kukwepa wajibu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 19, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Serikali kwa ujumla wake inastahili kulaumiwa kwa mimba za watoto wetu mashuleni.Miaka nenda miaka rudi serikali za awamu mbalimbali zimmeshindwa kabisa kusimamia uchumi wa nchi yetu inavyo pasa.Hivi mwanachi anapo kuwa maskini unategemea afanye nini?Si atafanya lolote ili angalau aweze kujikimu?Kama kweli serikali ina nia ya dhati ya kukomesha mimba za mashuleni,basi isimamie uchumi sawasawa, ili maisha ya wananchi yaboreke.Pili tumeshasema tena na tena, kwamba matangazo ya television,vijiwe vya kuonyeshea kanda za video, matangazo ya biashara,matangazo mbalimbali ya redio yanahamasisha ngono,lakini serikali yetu katika hali ya kushangaza iko kimya kabisa, haitaki kuchukua hatua zozete.Binafsi sijui inafanya hivyo kwa maslahi ya nani.Hivi unategemea tangazo la kipindi cha usiku wa maraha cha RFA kinachorushwa usiku, nadhani kuanzia saa 6 usiku,chenye maneno 'Weka basi mpenzi' kiwe na athari gani kama sio kuhamasisha ngono?Au matangazo ya Fataki yaliyowekwa hata mashuleni,unategemea yafanye nini, kama sio kuhamasisha ngono?Tumeshaishauri serikali mara nyingi kwamba ichunguze kwa undani madai kwamba madawa ya chanjo mbalimbali yana athari kwa watoto wetu katika sula zima la kuhamasisha ngono, lakini mpaka leo haijachukua hatua zozote.Hatujui ukimya huo ni kwa maslahi ya nani.Habari za kuaminika zinasema kwamba ndani ya chanjo hizo wameweka kwa siri 'sex hormones.' Hizi 'sex hormones' ndizo zinazofanya watoto wetu wawe na hamu ya kupindukia ya ngono.Na hizi sindano watoto wetu wanazochomwa mashuleni bila sisi wazazi kujua, zina ajenda gani?Kwakweli serikali inastahili kulaumiwa kwa mimba za mashuleni,na matamshi haya ya Pinda kwamba wazazi wa watoto watakaopata mimba wakamatwe na wawekwe ndani ni ya uonevu na hayastahili kuungwa mkono.Serikali itimize wajibu wake kwanza.Baada ya hapo ndio iwe na ubavu wa kukamata wazazi.Kinyume cha hapo ni uonevu.
   
Loading...