Ngorika Nangomwa
New Member
- May 28, 2020
- 2
- 0
Nimemsikiliza ndugu Polepole mara kadhaa kuhusu watia nia kuanza kampeni maapema pamoja na kutoa rushwa. Niseme hili ni zuri sana ila linawahusu hawa watia nia wasiokuwa na fedha. Kwa mfano juzi nilikuwa mkoa wa Ruvuma watia nia matajiri wanazunguka kuhonga bila woga Ruvuma na wale wenye vyeo vya ukurugenzi na udc nk. Hawaogopi na nilipouliza wenyeji wanasema jamaa wanatoa saana na hakuna anayeshughulika nao hili tayari changamoto kwa chama
Pia nilivyoenda Tunduru nimekutana na hali hiyo wenye pesa wanazunguka hakuna chombo chochote kinachochukua hatua yaani kimsingi kama huna fedha au madaraka basi vyombo utakutana navyo tu.
Mtwara ndio usiseme wanazurula hovyo watia nia wale matajiri yaani huko ndio utasema serikali jamaa wameitia mfukoni, niliuliza sehemu moja mtia nia anagawa sukari hapo Mtwara wengine wanagawa sementi wengine fedha yaani mkoa wa Mtwara vurugu ndio zimekuwa nyingi sasa.
Jana asbh nimeingia mjini kwangu hapa Dar waungwana hapa ni zaidi ya sehemu zote nimebaki kujiuliza hivi haya matamko ya Polepole hawayasikii au viburi vimewajaa tena huku wanatishiwa kabisa vijana waliotia nia na wenye fedha.
Wiki kadha zilizopita kule Tanga nako ilikuwa hatari mno wanagawa sana fedha kwa ufupi mchakato wa kura za maoni washindi watakuwa wenye fedha na umaarufu na wale wenye vyeo sasa hivi ma-RC,ma-DC na ma-DED wachache saana hawa wasio na kitu watakaotoboa kutokana na uhalisia wa siasa za Tanzania.
Nimwombe ndugu Polepole watumieni vizuri watu wa vyombo hali ni mbaya sana Rais ana nia nzuri na chama ila mikoani huko balaa tupu hata hivyo vyombo vinanunulika huko ni marafiki zao matajiri na wenye vyeo.