Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,808
- 6,500
​​​​Mwalimu nyerere katika kitabu chake cha Uongozi wetu na hatima ya Tanzania aliwahi kuandika, Chama legelege huzaa serikali regelege. Nami nasema, kama hiyo ikitokea hata vikao na maamuzi mbalimbali serikalini yatakuwa pia ni legelege.Tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia matukio mbalimbali yanayotokea ya watu fulani kujaribu kuigawa jamii katika misingi ya Utaifa, Udini na tofauti za kiitikadi lakini Serikali yetu iko kimya bila hata kukemea wale wanaoendekeza hulka kama hizi. Na ukimya ni kiashilia cha kuwa labda serikali inakubaliana na haya yanayotokea au haijui nini cha kufanya.
Serikali yetu inakuwa kama MAJIVUNO kwenye riwaya ya Shaaban Robert. Shaaban Robert anamuelezea Majivuno kama Waziri mkuu mwenye haiba kubwa na uhodari mwingi lakini anakosa utashi katika utekelezaji wa majukumu katika serikali yake mpaka inafikia katika hali tete.
Serikali yetu kwa kiyafumbia macho matatizo madogo madogo ambayo Mwalimu Nyerere aliyaita nyufa ndiyo imepelekea kufikia hapa tulipo ambapo inakuwa ni vigumu sana kukabiliana na hili tetemeko la ubaguzi wa kitaifa, kidini na tofauti za kiitikadi.
Itakuwa vizuri tukijikumbusha nini Mwalimu Nyerere alisema katika maswala haya ya Ubaguzi kwa misingi ya taifa, Kidini na kiitikadi za kisiasa na athali zake katika jamii.
Unaweza pia ukakataa kukubaliana na mawazo ya "Baba wa Taifa".

Last edited by a moderator: