Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 57,728
- 92,144
- Alipoulizwa kuhusu pesa ya kodi akasema Waulizwe TRA, kwa maneno mengine hajui kilichofanyika, tuliache hilo kwanza.
- Hotel ya Morogoro ikapewa siku 14 iwe imebomolewa, hadi leo hii holaaaa
- Wakulima wa korosho wakatakiwa walipwe ndani ya saa 48 hadi leo hii holaaa
- Akasema atatoa hatma ya Dr. Mwaka hadi leo hiii peupeeeeeee
Nashauri wafanye kazi bila media, wawe wa pole na wawe na mpangokazi, tukishajitangaza kwenye media nanma hii halafu hakuna kinachofanyika tunajishushia hadhi, heshima na utu kwenye jamii.
Hali hii inanikumbusha story ya Snake Girls niliyowahi kuisoma miaka mingi iliyopita, kwa ufupi iko hivi; Mama mmoja hakujaaliwa watoto na hivyo katika hangaika yake akatokea kwa mganga na mganga akampa dawa ambayo alitakiwa kuweka kwenye chungu na baada ya siku saba afungue chungu.
Ilipotimu siku ya saba alifanya kama alivyoambiwa na akawaona wasichana wazuri mno na akamshukuru sana Mganga ila akapewa masharti kuwa hatakiwi kabisa kuwafokea na siku akifanya hivyo ndio itakua mwisho wa watoto hao, siku moja yule Mama akakuta binti yake amevunja mtungi wake, akawafokea sana na kusema "WHAT CAN YOU EXPECT FROM THE HEAD OF THE SNAKE?" na hapo wale watoto waligeuka kuwa nyoka na kurudi porini.
Na mimi nikajikuta najiuliza swali kama hilo hilo kabisa, kwa wingi wa matamko haya yasiyo na tija "WHAT CAN YOU EXPECT FROM THE HEAD OF THE SNAKE?"