Matamko Hewa Serikali Ya Magufuli

Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
1,115
2,771
Itajulikana kama serikali isipokuwa na meno kwani wametoa matamko mengi sana ambayo hayajatekelezwa.
1. Ombaomba walipewa siku Chache kuhama jiji la Dar, cha ajabu wakaja kumkejeli Paul Makonda
2. Hakuna kusimama kwenye daladala. Yaani ndio daladala zinazidi kushona
3. Wenye mahoteli ufukweni walipigwa marufuku kutoza kiingilio kwa wale wanaotaka kuingia ufukweni. Leo nenda South Beach, mbalamwezi Pamoja na Ramada wanakotoza 40,000
4. Sukari serikali ilipanga bei yake, leo, Sukari ni 7000 mtaani.
5. Elimu bure kwa kila mwanafunzi. Hili nalo jipu la Magufuli, maana shule nyingine ilipokea 50,000 kuwezesha shule zenye wanafunzi 700

Serikali yetu mbona matamshi hewa?
 
Mtatubu mwak huu na hii speed.....hongera kwa kuielewa vzr...tunzeni data vzr... Hii ndo bahari mKapi yatakaa nje kila SKU.
 
Mtatubu mwak huu na hii speed.....hongera kwa kuielewa vzr...tunzeni data vzr... Hii ndo bahari mKapi yatakaa nje kila SKU.

Kweli aisee watuache na wamuache mkulu atimilize sera zake za viwanda. Hii ndo serikali ya viwanda jamani tupeane muda, ndo tuna miezi 6 madarakani yote yataisha tuu. Tuwe wavumilivu tafadhari.

Hayo matamko yote tunayafanyia upembuzi yakinifu soon utekelezaji unaanza na mkandarasi yupo njiani kuanza kazi tukimaliza upembuzi wetu. Narudia tuvumiliane. Serikali ya viwanda itatimiliza yote iliyoahidi.
 
Mtoa mada umenifurahisha sana. Walichora alama ya x kwa mbwembwe sana kwenye jumba la mama Rwakatare kisa kajenga pasipostahili na ndio ukweli lakini mpaka sasa jengo lipo na habari ya matajiri ndo ishaisha ivo
 
Tatizo kubwa Makufuli anapigana vita ambavyo wenzie hawamuungi mkono,viongozi wote wa ccm hawako tayari kupiga vita Ufisadi maana wao ndio mafisadi na hawakujua kwamba makufuli alikuwa na nia ya kupinga ufisadi wao,wao walitegemea Makufuli atawashughulikia mafisadi wa vyama pinzani,sasa imekuja kuonekana kwamba kwenye vyama vya upinzani hakuna mafisadi,mafisadi wote ni viongozi wa ccm maana wao ndio wenye madaraka serikalini, kwa hali hiyo vita hii ni ngumu kupigana nayo ndani ya ccm maana ni sawa na kupigana na watoto wako. mwenye masikio atanielewa
 
Back
Top Bottom