Matakwa ya Spika Ndugai kuhusu Kamati za Bunge kufuatilia mchakato wa ajira za walimu. Je, Serikali inafanya udanganyifu?

zebedayo musibha

Senior Member
Oct 26, 2019
111
86
Mapema leo 24/05/2021, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amezitaka kamati kufatilia mchakato wa ajira za walimu zilizotangazwa kwa uwazi na ukweli.

Pia ameonyesha kutoridhika na ajira zilizotolewa mwaka jana huku ikionyesha kanakwamba hakuna uwazi katika kuajiri. Nimekuwa na maswali kuhusu hili.

Je, hapa Spika anamanisha kuwa katika kuajiri walimu serikali haiko wazi?

Je, Spika anamaanisha kuwa katika kuajiri serikali inaegemea ukanda na ukabila?

Je, Spika anamaanisha hapa Tanzania kuna aina ya watu fulani ndio wanafaa kuwa walimu?

Huyo ukiona hivyo kuna watu wake alitaka kuwachomeka sasa imebuma,,sakata la kuwashambulia Tarura ilikuwa haelewani na meneja wa Tarura kule kongwa na Mke wake pia alikuwa na shida pale chamwino.

Afu huyu jamaa ni mbinafsi Sana aisee
 
Mapema leo 24/05/2021, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amezitaka kamati kufatilia mchakato wa ajira za walimu zilizotangazwa kwa uwazi na ukweli.

Pia ameonyesha kutoridhika na ajira zilizotolewa mwaka jana huku ikionyesha kanakwamba hakuna uwazi katika kuajiri. Nimekuwa na maswali kuhusu hili.

Je, hapa Spika anamanisha kuwa katika kuajiri walimu serikali haiko wazi?

Je, Spika anamaanisha kuwa katika kuajiri serikali inaegemea ukanda na ukabila?

Je, Spika anamaanisha hapa Tanzania kuna aina ya watu fulani ndio wanafaa kuwa walimu?

View attachment 1796302
Ikiwa ufuatiliaji huo ni kwania njema ya dhati ya moyo wake na ikiwa lengo ni kuiunga mkono awamu ya sita,itakuwa ni jambo jema sana.
 
Mapema leo 24/05/2021, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amezitaka kamati kufatilia mchakato wa ajira za walimu zilizotangazwa kwa uwazi na ukweli.

Pia ameonyesha kutoridhika na ajira zilizotolewa mwaka jana huku ikionyesha kanakwamba hakuna uwazi katika kuajiri. Nimekuwa na maswali kuhusu hili.

Je, hapa Spika anamanisha kuwa katika kuajiri walimu serikali haiko wazi?

Je, Spika anamaanisha kuwa katika kuajiri serikali inaegemea ukanda na ukabila?

Je, Spika anamaanisha hapa Tanzania kuna aina ya watu fulani ndio wanafaa kuwa walimu?

View attachment 1796302
8000 wapi wakati waliopata hata 500 hawakufika
 
hakika suala la keki ya taifa linatakiwa kutazamwa upya kwa jicho la kipekee, najua mheshimiwa spika kagusia ajira za ualimu wataanza kufuatilia na kuwe na utaratibu maalumu wa kueleweka, ila hili suala ni pana zaidi kwenye ajira zitolewazo na mamlaka za uteuzi, nadhani hakuna kipindi kigumu kama mamlaka inafanya uteuzi wewe unaitwa tu kwenye hafla kushangilia na kutoa speech nzuri ya kusifia huku watu wako hawana ajira na hawapewi fursa serikalini, ni wakati sasa uteuzi wa viongozi wa kitaifa kuanzia wakuu wa wilaya, majaji, wakuu wa taasisi, idara nyeti, bot, wakurugenzi, ras, das, makatibu wakuu wakatokana na utaratibu maalumu ambao upo wazi yeyote anaweza kupata kulingana na utumishi wake ndani na nje ya serikali na watu waombe nafasi hizo za uteuzi kulingana na uwezo wao na kuwe na sifa zinazotambulika kwa viongozi wa nafasi hizo, mbali na hizo kuna ajira za idara nyeti za serikali kuanzia Tiss, bot ziwe zinatangazwa kwa vigezo maalumu, sio unakuta miaka nenda rudi ni wale wale inasikitisha sana kuona jamii ile ile iliyopo kwenye vyombo vyetu ndo hiyo hiyo inaongoza kwa kuendelea kupachika watu bila kufuata utaratibu maalum
 
Leo mhe. Spika alipata Nafasi ya kuwakumbusha Wabunge Majukumu yao.

Ndugai amehoji Kwamba Mbunge upo Bungeni zinatoka Nafasi za Ualimu ama Udaktari wewe upo tu wala ujui Jimboni watu wangapi Wamesoma ualimu hawana Ajira .

Anashauri Kuwa Ni Jukumu la Mbunge Kujua Vijana wangapi wakimaliza Form 4 ama Form six na Chuo.

Mbunge Kuwa Bungeni ni Rahisi yeye kuongea na Kuomba kwa Mawaziri Husika vijana wake wasadiwe wale wenye vigezo wakwenda Jeshini waende wakupata Kazi wapate.

Akaenda Mbali zaidi Na Kusema Kwamba tuwe na Utumishi ambao unatoa Sura ya Nchi kwa kuangalia Vigezo.

Akasema Unajua wanaosimamia Ajira nao ni binadamu wanaweza angalia wanapotokea tu. Spika kashauri Wabunge wafatilie angalau kila Jimbo wapate nafasi kwa Vijana ambao wana vigezo. Video inanishinda kuipandisha Hapa Wakuu
 
Akasema Unajua wanaosimamia Ajira nao ni binadamu wanaweza angalia wanapotokea tu. Spika kashauri Wabunge wafatilie angalau kila Jimbo wapate nafasi kwa Vijana ambao wana vigezo ..... Video inanishinda kuipandisha Hapa Wakuu
1621886466174.png
 
Wimbo wa "Vijana tujiajiri" bora upumzishwe na tukabiliane na hii changamoto ya ukosefu ajira.
 
Back
Top Bottom