Matajiri ambao ni Maadui wa Magufuli ni wengi kiasi hiki?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,226
116,839
Nimesikia leo Rais Magufuli anasema kuna 'matajiri' wanahonga magazeti
ili yaandike habari za njaa wakati hakuna njaa..

Najiuliza maadui wa Magufuli wako wengi kiasi hiki?

Kwenye sukari tuliambiwa kuna matajiri wanaficha
karibu kila tatizo utaambiwa kuna 'watu fulani' wako nyuma ya hilo tatizo
kumkwamisha Rais.....

Je, wakishamkwamisha wanapata faida gani?

Je, ni kweli hawa watu wapo kweli?
what if ni 'imaginary enemies'?

Rais hana nguvu ya kuwashughulikia kama wapo?
 
Kwani mkuu ulikuwa hujui jinsi nchi ilivyogeuzwa ya wapigadili? Wauza unga, wakwepa kodi, vibaka, majambazi wote hao unadhani wanafurahia hizi drastic measures anazochukua mkuu??
Zipi hizo drastically measures?Za kufunga Wapinzani kwa kesi uchwara au zakuwafutia kesi wabunge wa CCM walioomba Rushwa??Nchi ya Vi-wonder,mbaazi zikikosa jua zinasingizia jua
 
yeye ndiye anataka kuweka uwadui .

"SERIKALI YANGU HAITATOA CHAKULA,NINAPOSEMA SILETI CHAKULA SILETI KWELI,WALA SIMUNG'UNYI MANENO NA SITALETA KWELI,MLIZOEA MANENO MATAMU SASA MIMI SINA MANENO MATAMU"alisisitiza RaisMagufuli.

swissme
 
Hakuna kitu kama hicho ....

Wewe ushindwe kununua mahindi kuweka kwenye magala ya Serikali uje usingizie wafanyabiashara........

Hivi mfanyabiashara maana yake ni nini? Si ni kupata faida?.....

Au siku hizi wanawalipa mishahara wafanya biashara mpaka wawatishe kiasi hiki?.....

Na sukari alikurupuka hivi hivi mpaka ikapanda......

Sasa hivi hii kauli naona inaenda kupaisha Sembe na Mchele......

Wanaumia sio Magufuli au wafanya biashara ......

Wanaoenda kuumia ni wananchi tena hao hao waliokuwa wakimshangilia hapo Bariadi.....

Hivi Serikali inataka kupata kodi
wapi kama haiwataki wafanyabiasha na wawekezaji?....

Nchi ya kipumbavu sana hii.....
 
Zipi hizo drastically measures?Za kufunga Wapinzani kwa kesi uchwara au zakuwafutia kesi wabunge wa CCM walioomba Rushwa??Nchi ya Vi-wonder,mbaazi zikikosa jua zinasingizia jua
Mmezoeleka mpaka mmeanza kuboa...wakishinda upinzani utasikia "mahakama inatenda haki"....mkishindwa mtasikia comments kama hiyo yako...guys, grow up
 
Kwani mkuu ulikuwa hujui jinsi nchi ilivyogeuzwa ya wapigadili? Wauza unga, wakwepa kodi, vibaka, majambazi, wazee wa 10%, wote hao unadhani wanafurahia hizi drastic measures anazochukua mkuu??
Kwa hiyo hata wale wananchi waliomsimamisha mkuu wa mkoa na mimea ya mahindi iliyonyauka kama ishara ya njaa nao walitumwa na matajiri?
Hapa hatuna mtu watanzania tulikosea njia
 
Sema ulikosea wewe mwizi au mkwepakodi uliyedhani mtamrubuni pindi akiingia ikulu...pole(ni)
 
Matajiri wanachukiwa kweli, kila siku wao ndio wanasababisha matatizo kwenye urais. Mara wanaficha hela, mara wanaficha sukari,mara milioni 7 kila dakika , mara wanaeneza njaa duh. Hao matajiri hawana cha kufanya au? Kuna ukweli au visingizio baada ya kuchemka?
 
Nimesikia leo Rais Magufuli anasema kuna 'matajiri' wanahonga magazeti
ili yaandike habari za njaa wakati hakuna njaa..

Najiuliza maadui wa Magufuli wako wengi kiasi hiki?

Kwenye sukari tuliambiwa kuna matajiri wanaficha
karibu kila tatizo utaambiwa kuna 'watu fulani' wako nyuma ya hilo tatizo
kumkwamisha Rais.....

Je wakishamkwamisha wanapata faida gani?
je ni kweli hawa watu wapo kweli?
what if ni 'imaginary enemies'?

Rais hana nguvu ya kuwashughulikia kama wapo?
Awashughulikie mara ngapi?
 
Hivi kusema tu bila data kunatusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo husika?
Kusema tu kuwa kuna matajiri wanafanya hivi na vile ili kuleta sintofahamu kwenye jamii ambayo kwayo wewe ni kila kitu Kama polisi, mahakama na magereza na Dola yote unaimiliki, sisi hadhira tutarajie kutoa suluhu au?
Ni matajiri gani wasiotajika wala kukamatika? Ni wa nje au hawa wa hapa wasiozidi 10 tunaowajua?
Hiki kizungumkuti kinatutia kizunguzungu!
 
Matajiri wanachukiwa kweli, kila siku wao ndio wanasababisha matatizo kwenye urais. Mara wanaficha hela, mara wanaficha sukari,mara milioni 7 kila dakika , mara wanaeneza njaa duh. Hao matajiri hawana cha kufanya au? Kuna ukweli au visingizio baada ya kuchemka?

Wafanye hivyo kwa faida ipi?
 
yeye ndiye anataka kuweka uwadui .

"SERIKALI YANGU HAITATOA CHAKULA,NINAPOSEMA SILETI CHAKULA SILETI KWELI,WALA SIMUNG'UNYI MANENO NA SITALETA KWELI,MLIZOEA MANENO MATAMU SASA MIMI SINA MANENO MATAMU"alisisitiza RaisMagufuli.

swissme
With time,utamuelewa tu
 
Hivi kusema tu bila data kunatusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo husika?
Kusema tu kuwa kuna matajiri wanafanya hivi na vile ili kuleta sintofahamu kwenye jamii ambayo kwayo wewe ni kila kitu Kama polisi, mahakama na magereza na Dola yote unaimiliki, sisi hadhira tutarajie kutoa suluhu au?
Ni matajiri gani wasiotajika wala kukamatika? Ni wa nje au hawa wa hapa wasiozidi 10 tunaowajua?
Hiki kizungumkuti kinatutia kizunguzungu!

kizunguzungu kikubwa
 
Back
Top Bottom