Matajiri 10 hawa hapa na 80% wamewekeza kwenye technology

mujulu

Member
Dec 25, 2017
61
37
Post iliyo pita nilikuelezea kuwa utajiri mkubwa upo kwa wawekezaji walio wekeza kwenye teknolojia , sikatai kwamba wawekezaji wa kwenye mafuta na Madini na wengine wapo ila tunaona kwenye teknolojia ya mawasiliano wamezidi kuwa juu
HII NI ORODHA YA MATAJIRI 10 WAKUBWA DUNIANI

karibia asilimia 80% wote wamewekeza kwenye teknolojia ya mawasiliano angalia
hawa hapa

1. Jeff Bezos, dola bilioni 145

Jeff Bezos, mbali na kuwa mmiliki wa Makampuni ya Amazon, lakini pia amewekeza zaidi kwenye teknolojia za anga za juu (Space technology) na pia anamiliki gazeti kubwa la The Washington Post

2. Bill Gates, dola bilioni 106.6

Kwa miaka 20 iliyopita, Bill Gates, Mwanzilishi wa Microsoft amekuwa juu kwenye orodha ya Forbes ya watu matajiri zaidi duniani. Bill ametoa kiasi kikubwa cha umiliki wake kwenye Microsoft na sasa anamiliki 1% pekee na amejikita zaidi kwenye shughuli zake za kutoa misaada chini ya Taasisi yake ya Bill and Melinda Gates Foundation.

3. Bernard Arnault, dola bilioni 91.6

Arnault, Mfaransa ni Tajiri namba moja barani Ulaya anayepatikana kwenye orodha hii. Bernard anamiliki zaidi ya makampuni 60 ikiwemo Louis Vuitton na Sephora. Hivi karibuni alishika nafasi ya pili katika orodha ya matajiri duniani mbele ya Bill Gates, ingawa alirudishwa nyuma baada ya utajiri wa Bill kuongezeka

4. Mark Zuckerberg, dola bilioni 78.6

Mark Zuckerberg ni maarufu zaidi kwa kuanzisha kampuni la Facebook Inc. ambalo linamiliki makampuni mengine kadhaa ikiwamo Facebook yenyewe, Instagram, WhatsApp na kadhalika. Zuck alianzisha Facebook mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 19 pekee.

5. Warren Buffett, dola bilioni 68.8

Kwa zaidi ya miongo tisa sasa, Warren Buffet, Mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya Berkshire Hathaway, ni moja kati ya watu matajiri zaidi duniani na moja kati ya wawekezaji wenye mafanikio zaidi duniani na pia ameahidi kutoa 99% ya utajiri wake kwaajili ya misaada.

6. Larry Ellison, dola bilioni 67.3

Larry ni Mwanzilishi mwenza wa Kampuni la kutengeneza programu mbalimbali ya Oracle. Aling’atuka kama Mkurugenzi Mkuu mwaka 2014 lakini bado ni mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Afisa Mkuu wa Teknolojia.

7. Steve Ballmer, dola bilioni 66.4

Steve Ballmer ni Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Microsoft akihudumu kati yam waka 2000 hadi 2014 huku akiwa mwajiriwa wa kampuni hiyo tangu mwaka 1980. Steve aliacha Chuo Kikuu cha Stanford wakati akifanya Shahada ya Uzamili. Baada ya kustaafu kutoka Microsoft, alinunua Klabu ya Mpira wa Kikapu ya Los Angeles Clippers inayoshiriki Ligi ya NBA.

8. Larry Page, dola bilioni 63.3

Mwaka 1998, Page alianzisha kampuni ya Google pamoja na mwenzake Sergey Brin. Mwaka 2019, aliamua kung’atuka madarakani kama Mkurugenzi Mkuu wa Alphabet, kampuni mama wa Google ingawa bado ni mmoja kati ya wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo.

9. Amancio Ortega, dola bilioni 61.9
Mwaka 2011, Ortega aling’atuka kama Mwenyekiti wa Inditex, kampuni inayomiliki chapa ya Zara ingawa bado anamiliki 60% ya hisa za kampuni hiyo.

10. Sergey Brin, dola bilioni 61

Brin ni Mwanzilishi mwenza wa Google ambaye aling’atuka kama Rais wa Alphabet 2019 December, ingawa bado ni mjumbe wa bodi. Kwasasa anatumia muda wake mwingi kwenye mradi wa utafiti wa Alphabet unaufahamika kama Lab X

POST ITAKAYO FUATA NDIO NTAELEZEA JINSI YA KULINDA WAZO LAKO LA KITEKNOLOJIA ILI LIZAE MATUNDA NIMEKWAMBIA TENA ISSUE SIKUWA NA WAZO LA KITEKNOLOJIA ISSUE KUBWA NI KULINDA WAZO NA KULIBADILI LIZAE PESA UITUMIE
 
Naomba nikurekebishe kidogo boss latest data hizi apa bezos ana $B200
Screenshot_20200828-220740_Chrome.jpg
 
Dah haya mambo ni hatari,juzi juzi tu mukeshi ambani alikuwa ndiyo habari baada ya kuingia top 5 ya matajiri duniani,sasa Hivi watu washachukua position.
Mukeshi nashangaa aliingiaje top 5 wakati kisa kampuni ya mafuta. Achana na Jio, kampuni mpya ya simu itakayokuja kwa kasi. Sioni nafasi tena ya oil billionaires kama hadi BP wameanza kusitisha baadhi ya miradi ya utafiti wa mafuta.

Ila mdogo wake Mukeshi, Amil Ambani ni jinga sana. Mtu alikuwa anahesabu zaidi ya $42B miaka ya 2010s leo anahesabu negative. Yani mali alizonazo hata akilipa madeni bado anabakia anadaiwa.
 
Huyo Jeff hafai, mpunga wote huo na bado anakomaa...
Jeff hakomai chochote tena. Ni upepo wa mahitaji unamfanya ale. Yani hakuna breakthrough ya maana amefanya, huyu ndo billionaire kwenye list ambaye hana pressure sana.
Hawa kina wamiliki wa Tesla lazima wakomae sana kutoa product innovative kila mwaka. Imagine mtu kama Page au Sergei Brin, lazima watoe matoleo kibao ya Google wahangaike. Ila Amazon inafanya changes na ofa ambazo si za kuumiza kichwa kabisa.
 
Channel ya pesa ukiijenga kwenye value chain hupati shida🤣🤣🤣 ni sawa na mchuuzi na mzalishaji.

Anayezalisha bidhaa ndio anateseka iwe shamba au kiwandani ila dalali ndio anamenya, kila manunuzi online anaokota senti zake tu!

Sawa na mtu aingie ubia na Tanroads wajenge highway speed track (autobhan) kisha waweke road tolls kwa kila mtumiaji wa hio track ambayo itakaa pembeni zaidi ya lami ya kawaida kushoto na kulia ikiwa ni kwenda na kurudi with protection cages.

Una relax unakamua hela tu kila anayetaka kukimbiza gari anaingia humo na kulipa 30k gari za chini ya tani 3, chini ya tani 8 wao 50k zaidi ya tani 8 wao 100k mtu anawahi mkoa anakoenda. Hapo ndani ya 10 years we ushakuwa Mo Dewji hela inaingia vizazi na vizazi. Unasubiria kuandikwa forbes tu!

Imagine kwa kila siku mnakusanya kati ya 150M-300M on moving cars. Mkitoa kodi ya mapato ukala gawio lako hata kama ni 30M per day, kwa mwezi una bei gani katika account!? Thats on minimum halafu serikali inakosa kodi kizembe kwa kukosa ubunifu na matochi yao ya kijinga wanakomalia fines kama source ya kodi.
 
Mukeshi nashangaa aliingiaje top 5 wakati kisa kampuni ya mafuta. Achana na Jio, kampuni mpya ya simu itakayokuja kwa kasi. Sioni nafasi tena ya oil billionaires kama hadi BP wameanza kusitisha baadhi ya miradi ya utafiti wa mafuta.

Ila mdogo wake Mukeshi, Amil Ambani ni jinga sana. Mtu alikuwa anahesabu zaidi ya $42B miaka ya 2010s leo anahesabu negative. Yani mali alizonazo hata akilipa madeni bado anabakia anadaiwa.
Huyu mdogo wake kazingua sana
 
Back
Top Bottom