Mataifa yaanza kuwaondoa raia wake Nchini Afghanistan

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Kampeni kubwa ya kimataifa inaendelea kuwahamisha raia wa kigeni na wa Afghanistan waliofanya nao kazi, wakati maelfu ya watu waliojawa na hofu ya utawala wa Taliban wakizidi kufurika katika uwanja wa ndege wa Kabul.

Baada ya mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO hapo jana, katibu mkuu wa Jumuiya hiyo, Jens Stoltenberg alisema kuwa ndege zaidi zitapelekwa Kabul kusaidia shughuli hiyo, ambayo ilikwamishwa na mtafaruku uliotokea Jumatatu.

Pamoja na ndege hizo Marekani pia imepeleka wanajeshi 1000 wa ziada na kufikisha maafisa 4000 wanaosimamia kazi hiyo ya kuwahamisha watu. Msemaji wa Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Steffen Seibert amesema kuwa Kansela huyo amefikia makubaliano na viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Italia, kushirikiana katika operesheni hiyo ya kuwaondoa raia wao kutoka Afghanistan.

Wizara ya ulinzi ya Ujerumani imesema tayari ndege za nchi hiyo zimewahamisha watu 260 kutoka Afghanistan.

Ulaya kushirikiana katika kuwaweka salama raia wao walioko Afghanistan
Suala hilo la kuwaondoa raia wa kigeni kutoka Afghanistan lilikuwa agenda kuu kwenye mkutano kati ya mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell na mawaziri wa nchi za nje wa Umoja wa Ulaya, ambao ulifanyika jana jioni kwa njia ya video.
 
Haya Taliban tunasubiri kuona uongozi wao au ndio watarudi kule kule ya 90's.

Haki ya mtoto wa kike kwenda shule
 
Marekani sio watu wa kuwaamini hata kidogo
 
Back
Top Bottom