Mataifa kadhaa yalaani mabadiliko ya uchaguzi Hong Kong yanayolenga kuipa nguvu zaidi Serikali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mataifa kadhaa duniani yakiongozwa na Marekani leo yamelaani mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi wa mji wa Hong Kong yaliyoidhinishwa jana Alhamisi na Baraza la Wajumbe wa Chama cha Kikomunisti cha China.

Marekani, Australia, Canada na Uingereza zimetoa matamshi ya kukosoa uamuzi huo utakaoipa nguvu kamati inayounga mkono serikali mjini Beijing kuteua wabunge wengi zaidi wa Hong Kong kuliko idadi ya wanaopigiwa kura na umma.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amesema kile kilichoidhinishwa ni mwendelezo wa ukandamizaji unaofanywa na China kwa taasisi za mji wa Hong Kong wenye mamlaka yake ya ndani.

Matamshi kama hayo yametolewa pia na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Australia, Canada na Uingereza ambao wameutaja uamuzi huo wa China kuwa njia ya kuminya demokrasia na uhuru wa kisiasa mjini Hong Kong.
 
Back
Top Bottom