MATAGA wadhibitiwe, wanamkwamisha Rais Samia Suluhu

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,799
18,224
Naingia kwenye mada moja kwa moja nisiwachoshe. Baada ya mwendazake kufanikiwa kuiharibu hii nchi kwa kubaka Uchaguzi Mkuu wa 2020, sasa CCM inaongoza nchi nzima kuanzia Balozi hadi Rais. Mwendazake aliwahi kusema kwamba CHADEMA ndio wanamkwamisha kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo akaamua hata mCHADEMA mmoja asirudi uongozini baada ya 2020. Na kweli mbinu yake ilifanikiwa kwa 101%. Sasa nchi nzima imefunikwa na kijani kibichi tu!

Nilitarajia wanaCCM wote sasa wangeridhika na kuunga mkono juhudi za Rais aliyepo madarakani. Lakini baada ya kifo cha mwendazake, limejitokeza kundi wa MATAGA (waliokuwa wakimuunga mkono mwendazake kindakiki) kumkwamisha Rais Samia kwenye harakati zake za kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli. Hiki kikundi cha MATAGA hakitofautiani na vikundi vingine vya kigaidi kama vile Mungiki, Janjaweed, Al-Qaeda, Boko Haram, Al-Shaabab au genge la kihalifu alilokuwa akilitumia Sabaya kupora mali za raia na kuhujumu uchumi wa taifa. Genge hili ni zaidi ya pimbi anayekurupuka kutoka kichaka A kwenda kichaka B lakini baada ya sekunde chache anakurupuka tena kurudi kichaka A. Kwa ujumla, MATAGA hawajui ni nini wanachokitaka!

MATAGA ni genge la hatari sana na endapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa kuwadhibiti, watayumbisha mno maendeleo ya taifa hili. Na kibaya zaidi, baadhi ya wafuasi wa genge hili wameanza kujikomba kwa mama kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili wakae karibu naye wamharibie. Wanachama wa genge hilo wanajionyesha hadharani kwa vicheko vyao vya kinafiki huku mioyoni mwao wamejawa na husda na unafiki wa kupindukia.

MATAGA wapo kila kona ya nchi hii. Wengi wao wanatumia mitandao ya kijamii kuzusha mambo ya ajabuajabu kuhusu kifo cha mwendazake ili kumtoa mama kwenye reli. Nashukuru mama ameanza kuwashutukia baadhi yao na kuwachomoa mazima kutoka kwenye ulingo wa serikali yake. Kilichotokea majuzi ni ushahidi tosha kwamba janja yao ya nyani imeng’amuliwa mapema kupitia intelijensia ya uhakika.

Ingawa hivyo, namuomba mama Samia atumie mbinu kali kidogo kuwadhibiti CHAWA hawa kabla sumu yao haijasambaa sana kiasi cha kushindwa kudhibitika baadaye. Inasikitisha kuwa genge hili linatoka ndani ya CCM; badala ya kumsaidia mama kujenga nchi, wao wanasaidia kuibomoa. Hawa ni watu wabaya sana, sio wa kuwalazia damu hata kidogo. Hata ikibidi, basi wadhibitiwe kwa mbinu zozote mbaya na za hatari kabla mambo hayajaenda kombo.
 
Hicho Kikundi kisakwe kwa Udi na Uvumba
ufdup.png
 
Yaani kama kuna kitu kinawaumiza MATAGA, ni kuona nyuso za Watanzania zimeanza kung'aa baada ya mama kushika nchi. Angalau tuna uhuru kidogo wa kuandika na kuongea bila kuhofia sana kupotezwa.
Mataga walitaka wafaidi keki peke yao. Sasa wameona mama sio mchoyo, viroho vinawauma....

Kwa taarifa yao mama kapunguza mpaka kodi ya bia....
 
Sikuizi umehamia kwenye siasa umeachana na betting?
Naingia kwenye mada moja kwa moja nisiwachoshe. Baada ya mwendazake kufanikiwa kuiharibu hii nchi kwa kubaka Uchaguzi Mkuu wa 2020, sasa CCM inaongoza nchi nzima kuanzia Balozi hadi Rais. Mwendazake aliwahi kusema kwamba CHADEMA ndio wanamkwamisha kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo akaamua hata mCHADEMA mmoja asirudi uongozini baada ya 2020. Na kweli mbinu yake ilifanikiwa kwa 101%. Sasa nchi nzima imefunikwa na kijani kibichi tu!

Nilitarajia wanaCCM wote sasa wangeridhika na kuunga mkono juhudi za Rais aliyepo madarakani. Lakini baada ya kifo cha mwendazake, limejitokeza kundi wa MATAGA (waliokuwa wakimuunga mkono mwendazake kindakiki) kumkwamisha Rais Samia kwenye harakati zake za kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli. Hiki kikundi cha MATAGA hakitofautiani na vikundi vingine vya kigaidi kama vile Mungiki, Janjaweed, Al-Qaeda, Boko Haram au genge la kihalifu alilokuwa akilitumia Sabaya kupora mali za raia na kuhujumu uchumi wa taifa. Genge hili ni zaidi ya pimbi anayekurupuka kutoka kichaka A kwenda kichaka B lakini baada ya sekunde chache anakurupuka tena kurudi kichaka A. Kwa ujumla, MATAGA hawajui ni nini wanachokitaka!

MATAGA ni genge la hatari sana na endapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa kuwadhibiti, watayumbisha mno maendeleo ya taifa hili. Na kibaya zaidi, baadhi ya wafuasi wa genge hili wameanza kujikomba kwa mama kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili wakae karibu naye wamharibie. Wanachama wa genge hilo wanajionyesha hadharani kwa vicheko vyao vya kinafiki huku mioyoni mwao wamejawa na husda na unafiki wa kupindukia.

MATAGA wapo kila kona ya nchi hii. Wengi wao wanatumia mitandao ya kijamii kuzusha mambo ya ajabuajabu kuhusu kifo cha mwendazake ili kumtoa mama kwenye reli. Nashukuru mama ameanza kuwashutukia baadhi yao na kuwachomoa mazima kutoka kwenye ulingo wa serikali yake. Kilichotokea majuzi ni ushahidi tosha kwamba janja yao ya nyani imeng’amuliwa mapema kupitia intelijensia ya uhakika.

Ingawa hivyo, namuomba mama Samia atumie mbinu kali kidogo kuwadhibiti CHAWA hawa kabla sumu yao haijasambaa sana kiasi cha kushindwa kudhibitika baadaye. Inasikitisha kuwa genge hili linatoka ndani ya CCM; badala ya kumsaidia mama kujenga nchi, wao wanasaidia kuibomoa. Hawa ni watu wabaya sana, sio wa kuwalazia damu hata kidogo. Hata ikibidi, basi wadhibitiwe kwa mbinu zozote mbaya na za hatari kabla mambo hayajaenda kombo.​
 
Naunga mkono hoja.
 
Alichokifanya baada ya kuingia Madarakani cha kwanza ilikuwa kuirudisha #CCM kwenye mstari sahihi.
Kuirudisha kwenye mikono ya majambazi akina Sabaya na Bashite ndio mikono salama? Je, kuwapoteza raia akina Ben Saanane, Azory Gwanda na raia wengine waliopotezwa kule Kibiti ndio mikono salama mkuu au unamaanisha nini? Hebu funguka vizuri ueleweke....usitetee dhambi usiyoijua.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom