Uchaguzi 2020 Mataga nielewesheni nini maana ya Tanzania Mpya, Zanzibar Mpya?

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,870
2,000
Wakuu amani iwe kwenu,

Bila shaka wengi wetu wameona kauli mbiu hizi kwenye mabango ya wagombea mbali mbali hasa wa chama cha mapinduzi (CCM). Mgombea wa Urais Zanzibar kwenye bango lake kuna maneno "Zanzibar mpya", Mgombea wa Ubunge kigamboni kuna neno "Kigamboni Mpya" kwingine kuna Tanzania mpya" kwa ufupi wagombea wengi wa chama tawala wana hii kaulimbiu.

Wagombea ubunge wengi wanaosema sijui kigamboni mpya au ...mpya wamekuwa kwenye nafasi zao za ubunge kwa muda wa miaka 5, wengine kwa miaka10 na wengine kwa zaidi ya hiyo miaka. Hivi inaingia akilini kwamba hii kaulimbiu ni muafaka kwao kutumia? miaka 5 au 10 umekuwa mbunge au Rais halafu unatuambia tukuchague ili kigambani au serengeti iwe mpya? Kwanza mpya kiaje? nadhani wangekuwa waungwana wangetuambia kwanini kwa muda tuliowapa walishindwa kufanya hayo maeneo kuwa mapya, bila kupepesa wangesema wazi safa za hiyo inayoitwa mpya na zamani (mfano ndugu Ndugulile ungesema sifa ya kigamboni ya zamani uliyokuwa mbunge wake huko nyuma na kigamboni mpya unayotaka kwasasa?. Hili suali liko kwenye nafasi zote za udiwani, ubunge na urais bila kujali jimbo au chama.

Kwa chama cha mapinduzi nini maana ya kauli mbiu hii kwenye mabango yenu ya urais maana toka uhuru nyie ndiyo mnatuongoza na kututawala? Zipi zilikuwa sifa ya Tanzania ya zamani chini ya ccm na zipi zitakuwa sifa ya Tanzania mpya chini ya ccm baada ya uchaguzi?

Kuuliza si ujinga ni kutaka kujua

CCM Mpya!
Tanzania Mpya
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
7,624
2,000
Ni namna yao mpya ya kuwapumbaza wanyonge na waliokata tamaa wadhani kwamba yako mabadilikon yanayokuja kupitia chama hicho!!
 

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
1,170
2,000
Kuna wakati huwa natamani Mungu angefungua akili za Watanzania angalau kwa saa moja tu.!
 

issa yurry

JF-Expert Member
Apr 20, 2014
628
1,000
Yani Zanzibar mpya maana yake nikuifanya wilaya ya unguja na wila ya Pemba kwahiyo mamlaka yote yatakuwepo bara kwahiyo Zanzibar itaingia ktk serekali moja

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 

gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,695
2,000
Hao jamaa ni wataalam sana wakutengeneza kauli mbiu zakuadaa watu.ukiwa na akili fupi utadhani nchi inaenda kua bonge la nchi kumbe mbwembwe tu.Hakuna jipya lolote litakalifanywa na icho chama.Pamoja na kauli nzuri nzuri zakitapeli kila kipindi cha uchaguzi ila wale maadui aliowataja Mwl Nyerere bado wako vile vile tena nawengine wameongeza.
 

gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,695
2,000
Hao jamaa ni wataalam sana wakutengeneza kauli mbiu zakuadaa watu.ukiwa na akili fupi utadhani nchi inaenda kua bonge la nchi kumbe mbwembwe tu.Hakuna jipya lolote litakalifanywa na icho chama.Pamoja na kauli nzuri nzuri zakitapeli kila kipindi cha uchaguzi ila wale maadui aliowataja Mwl Nyerere bado wako vile vile tena nawengine wameongeza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom