Mataa njia panda ya Barakuda - Segerea yamekuwa kero

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Habarini wakuu,

Hii barabara ilikuwa haina mataa ila hivi karibuni kuna mataa yamewekwa kwenye hii njia panda ya barakuda ambayo inahusisha barabara ya kutoka na kweda Tabata Segerea (Segerea - Bima) pamoja na barabara ya kutoka na kwenda tabata chang'ombe (Chang'ombe - Vingunguti).

Kiukweli toka yawekwe haya mataa, yameongeza foleni. Ni usmbufu wa hali ya juu, sio usiku wala mchana. Wananchi tunapoteza muda mwingi sana hapo.

Tatizo kubwa nililogundua pale ni kuwa ile ni One way road hivyo mataa hayaleti ufanisi kama ambavyo yanaleta kwenye njia nyingi.

Mlio jirani na wahusika waambieni waliangalie hili swala. Tunapoteza muda mwingi sana barabarani pale kwenda na kurudi majukumuni.

Wasalaam.
 
Sijui nani aliwaambia waweke pale mataa ni tatizo hasa foleni itakuwa kubwa sana pale ila tutazoea tu ndiyo yashawekwa tena
 
Wasiyatoe ila wafanye marekebisho ya upendeleo wa muda wa taa ya kijani izidishwe muda kidogo wa kubadirika kwenye hii barabara ya kwenda segerea maana ndio inamagari mengi kuliko hii ya chang'ombe na vingungutu
 
Sasa hivi nipo tabata shule foleni ipo hadi tabata baracuda. Mataa yamekuwa kero kwa kweli tarura na tanroad waliangalie ili swala, barabra ni nyembamba sana
 
Back
Top Bottom