Maswanya kusimikwa Kamanda wa Uvccm Jimboni kwa Sitta!

Feb 3, 2010
19
0
Umoja wa vijana wilayani urambo jumapili ya wiki watafanya shughuli nzito ya kumsimika bwana Ally Maswanya kuwa kamanda wa vijana wa ccm wa wilaya kwa kipindi cha miaka 5 ijayo, bwana Maswanya ni mkurugenzi wa Zain kanda ya Ziwa na habari zisizo rasmi zinasema kuwa Bwana Maswanya ni mmoja kati ya watu ambao wameanza kumnyima usingizi bwana spika. Mgeni rasmi toka makao makuu ya Uvccm atawasili Tabora kesho mchana akitokea Dar na ataelekea Sikonge ambapo pia jioni ya kesho atamsimika bwana George Kakunda kuwa kamanda wa wilaya ya Sikonge!
 
Back
Top Bottom