Maswali Yangu Kwa Dr. Wilbrod Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali Yangu Kwa Dr. Wilbrod Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mchambuzi, Aug 25, 2010.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Nina tumai kwamba Jamiiforums inatekeleza dhana yake ya – WE DARE TO TALK OPENLY, kwa vitendio, na kwahiyo basi waratibu wake hawatafuta maswali yangu kwa wagombea Urais wa Chadema, CUF, na CCM. Mimi kama raia na mpiga kura katika nchi yangu nina haki ya kujibiwa maswali na wagombea moja kwa moja au kupitia wasaidizi wao ilimradi hayavunji sheria, kanuni na heshima. Ntaanzia na mgombea wa Chadema, Mheshimiwa Dr. Slaa.

  Dr. Slaa, nafasi ya uongozi ngazi ya Uraisi ni nafasi nyeti, yenye maamuzi mazito ambayo wakati mwingine yanakinzana na suala la dini. Kwa mfano dini ya kikristo hairuhusu kulipiza visasi – haitakiwi ulipize ubaya kwa ubaya. Kama tukikupa Urais wan chi yetu, ikitokea nchi yetu ya Tanzania ikavamiwa na maaadui, tukikuchagua Dr Slaa kuwa Rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, je kama amiri jeshi mkuu wetu, utaweza kutoa ruhusa nchi yetu iende vitani kutetea maslahi, mipaka na haki zetu watanzania?

  Pili, hakuna shaka kabisa kwamba serikali ya Jakaya Kikwete imesimamia kwa mafanikio makubwa sana suala la mauaji ya walemavu wa ngozi yani ALBINO. Dr. Slaa, je, tukikuchagua uwe Rais wetu wa Tanzania, ikija fikia suala la kufanya maamuzi ya kuizinisha wauaji wanyongwe, utakuwa tayari kusimamia death penalty, mfano kuizinisha wauaji wa albino wanyongwe? Utaziteteaje Haki za ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi yani Albino? utazisimamiaje?

  Mwisho tunafahamu fika ni jinsi gani Jakaya Kikwete alivyoweza kuwa kiongozi mvumilivu na asiye hamaki. JK ni mvumilivu sana, kwa mfano likija suala la vyombo vya Habari ambapo tumeona jinsi gani magazeti mbali mbali yanavyomchafua, ameyapa uhuru sana licha ya kuwa na uwezo wa kuyabana kikatiba. Je, Dr. Slaa wewe ni mvumilivu na usie na hamaki? Kuna mifano dhairi kutoka kwa wajumbe wa kamati yako ya Bunge jinsi gani ulivyokuwa mtu wa kuhamaki, hasira, kuzira na kung’ang’ania mawazo yako ndiyo yasikilizwe na yawe ya mwisho. Je, unatuelezea nini juu ya suala hili? Kuna ukweli kuhusu suala hili?

  Haya ni baadhi tu ya maswali ambayo mimi na watanzania wengine nadhani katika kipindi hiki tutakuwa tunakuuliza wewe na wagombea wa vyama vingine mara kwa mara ili tujiridhie kabla hatujafanya maamuzi mgumu ya kumpigia mgombea katika nafasi ya Urais Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania. Nina matumaini makubwa sana kwamba waratibu wa Jamiiforums hawatafuta maswali haya. Naomba kutoa hoja.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi bana....yaani tokea ubalaswe na Mwafrika Wa Kike ukapotea kabisa na sasa umeibuka baada ya kampeni za uchaguzi mkuu kuanza. You are a trip!!!

  But let not your heart be troubled because CHADEMA stands no chance to pull off the upset of all upsets.
   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,848
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Wewe umeshasema ni amiri jeshi mkuu na kazi za amiri jeshi ziko wazi atazifuata
  Ataangalia katiba na sheria za nchi zinasemaje rule of law, sheria ziko kwa watu wote na si kwa wauaji wa albino tu.
  Toa mfano hata mmoja JK amechafuliwaje na magazeti inawezekana kuambiwa ukweli wewe unachukulia ni kuchafuliwa.
  Hili si swali umeshamhukumu kuwa yeye ni mtu wa kuhamaki sasa unategemea jibu gani No au Yes.
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mchambuzi,

  Kwanza kabisa, KARIBU sana tena ndugu. Tulikosa upande wa mawaidha yako kwa muda mrefu. Naona umegusia kuwepo wasiwasi kuwa maoni yako yaliyoandikwa kwa ustaarabu BADO yanaweza kufutwa na waratibu wa JF. Kwa kweli sidhani kama waratibu wanaweza kufanya kitu kama hicho. Maoni na maswali yaliyo anti-Slaa, anti-Kikwete au anti-Seif mengi tu yana exist. Maoni mengi niliyoona yamepotea ni ya jamaa mmoja ambaye amepewa ban kwa sasa, Malaria Sugu. Kama ulikuwa unafungua JF kwa kipindi alichokuwa active, bila shaka yalikutibua pia. Jamaa anaudhi bana, hili halina ubishi!!

  Pili, naona kutoweka kwako kumekufanya upoteze ule u-sharpness nilio utegemea kutoka kwako. Nasema hivyo kwani naona maswali yako yako very basic, na yanaweza kujibika kwa majibu ambayo ungependa wewe mwenyewe kuyasikia. They are such leading questions, even Mh. Kikwete would answer them without a tele-prompter, au kwenye mdahalo live!

  Tatu, swali lako la mwisho nimelipenda, na ningefurahi kuona majibu ya Mh. Slaa. Lakini kwa kuwa Slaa ni member hapa, na kwa vile baadhi ya Wanachadema wenzake ni member kwa majina yao halisi, sitoshangaa kuona Mh. Slaa anakuwa na msimamo ulio na uvumilivu kuliko hata Mh. Kikwete kuhusiana na vyombo vya habari. Kwani, kushiriki kwake tu hapa JF na hata kuweza kujibizana na akina Malaria Sugu kunaonesha ni jinsi gani ambavyo anapenda kutoa maoni yake kwa wanajamii wote na kuongea kwa maoni bila kusita kujibu hoja.

  Kimoja chakujiuliza ni kwamba, pamoja na JF kukaribisha wanajamii wote kushiriki mijadala hapa jamvini, naona ni Chadema pekee waliojitokeza kujiandikisha kwa majina yao halisi, na hata kukubali mdahalo (CCM bila shaka imenywea!!). Kwa maoni yangu, hoja yako uliyoipaisha kupitia hapa JF kuhusiana na uvumilivu kwa vyombo vya habari na uhuru wa habari; hiki ni kielelezo tosha cha viongozi wanaopenda dhama ya uwazi na uwajibikaji. Basi, hapo juu kwenye kijani umesema utawauliza maswali CUF na CCM, najiuliza - je kweli utapata majibu ya CCM au CUF kama ambavyo unaweza kupata majibu kutoka kwa Zitto, Mnyika, Kitila au Slaa??!!

  Kuhusiana na swala la kuzira na kuhamaki, yumkini Slaa ni mgombea urais; ningelifurahi sana kama ungelitoa hadharani hiyo "mifano dhahiri" unayotaka kusema kuwa ni kiashiria cha mtu mwenye hasira na asiyekubali kupingwa na wajumbe wenzake.
  Shukrani.
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ukiona watu kama mchambuzi wanafikia kuandika utumbo kama huu basi ujue ccm wameshikwa pabaya. Yaani kama mkatoliki na mkristo Julius Nyerere (the real JK) aliamrisha watu kupigana ndio itakuwa vigumu kwa wakristo wengine kufanya hivyo?

  Bange tu hizo mchambuzi and you know it
   
 6. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HTML:
   
  Nina tumai kwamba Jamiiforums inatekeleza dhana yake ya – WE DARE TO TALK OPENLY, kwa vitendio, na kwahiyo basi waratibu wake hawatafuta maswali yangu kwa wagombea Urais wa Chadema, CUF, na CCM. Mimi kama raia na mpiga kura katika nchi yangu nina haki ya kujibiwa maswali na wagombea moja kwa moja au kupitia wasaidizi wao ilimradi hayavunji sheria, kanuni na heshima. Ntaanzia na mgombea wa Chadema, Mheshimiwa Dr. Slaa.
  
  Dr. Slaa, nafasi ya uongozi ngazi ya Uraisi ni nafasi nyeti, yenye maamuzi mazito ambayo wakati mwingine yanakinzana na suala la dini. Kwa mfano dini ya kikristo hairuhusu kulipiza visasi – haitakiwi ulipize ubaya kwa ubaya. Kama tukikupa Urais wan chi yetu, ikitokea nchi yetu ya Tanzania ikavamiwa na maaadui, tukikuchagua Dr Slaa kuwa Rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, je kama amiri jeshi mkuu wetu, utaweza kutoa ruhusa nchi yetu iende vitani kutetea maslahi, mipaka na haki zetu watanzania? 
  
  Pili, hakuna shaka kabisa kwamba serikali ya Jakaya Kikwete imesimamia kwa mafanikio makubwa sana suala la mauaji ya walemavu wa ngozi yani ALBINO. Dr. Slaa, je, tukikuchagua uwe Rais wetu wa Tanzania, ikija fikia suala la kufanya maamuzi ya kuizinisha wauaji wanyongwe, utakuwa tayari kusimamia death penalty, mfano kuizinisha wauaji wa albino wanyongwe? Utaziteteaje Haki za ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi yani Albino? utazisimamiaje? 
  
  Mwisho tunafahamu fika ni jinsi gani Jakaya Kikwete alivyoweza kuwa kiongozi mvumilivu na asiye hamaki. JK ni mvumilivu sana, kwa mfano likija suala la vyombo vya Habari ambapo tumeona jinsi gani magazeti mbali mbali yanavyomchafua, ameyapa uhuru sana licha ya kuwa na uwezo wa kuyabana kikatiba. Je, Dr. Slaa wewe ni mvumilivu na usie na hamaki? Kuna mifano dhairi kutoka kwa wajumbe wa kamati yako ya Bunge jinsi gani ulivyokuwa mtu wa kuhamaki, hasira, kuzira na kung'ang'ania mawazo yako ndiyo yasikilizwe na yawe ya mwisho. Je, unatuelezea nini juu ya suala hili? Kuna ukweli kuhusu suala hili?
  
  Haya ni baadhi tu ya maswali ambayo mimi na watanzania wengine nadhani katika kipindi hiki tutakuwa tunakuuliza wewe na wagombea wa vyama vingine mara kwa mara ili tujiridhie kabla hatujafanya maamuzi mgumu ya kumpigia mgombea katika nafasi ya Urais Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania. Nina matumaini makubwa sana kwamba waratibu wa Jamiiforums hawatafuta maswali haya. Naomba kutoa hoja. 
  

  ~Our house is in a mess;there's nothing substantial in this.By the way,is this a party thing??This's a country's thing.If you are sure the person who has written this amesukumwa kufanya hivyo by someone for a certain amount,what do u expect hata mpinzani akimpa dau kubwa zaidi ili aandike utumbo kama huu?Ataandika.Simple:such people stand for nothing and they fall on anything,and that's the nation we have.~
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pia kwa kumkumbusha tu Mheshimiwa Mchambuzi, wiki hii niliona news kwenye magazeti JK akijinadi kwamba HAJAWAHI KUIDHINISHA KUNYONGA tangu aingie madarakani. Lakini Mchambuzi kwa spin zake naona amesema JK na serikali yake wamesimamia mauaji ya albino kikamilifu, ni lini walifanya hivyo? Hivi kuna mtuhumiwa hata mmoja ambaye amenyongwa mpaka sasa? Alinyongwa lini na ilihali JK kasema hajanyonga binadam yeyote?

  Naomba Mchambuzi umerudi kuendeleza hoja za LOWASSA FOR 2015, maana unajua kwamba JK akishinda itakuwa rahisi sana kwa Lowassa ku-bounce back ili anyooshe mapito ya kwenda Ikulu.
   
 8. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Si sahihi kwamba Wakristu hawaruhusiwi kupigana vita. There is what is called the doctrine of just war. Mchambuzi inabidi awe anasoma zaidi. Hajampiga vita adui ujinga kiasi cha kuridhisha.

  Kwenye swala la capital punishment niseme hivi: Si lazima kuwa Mkristu ili kuona kukosekana logic kwenye uamuzi wa kuua wauaji. Why murder murderers? We don't rob robbers or rape rapists! Sitegemei mtu kama Dr Slaa aidhinishe kuuawa wauaji, hata kama ni wauaji wa Maalbino
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Whats the frack is this?
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Naona siasa za Tanzania zinachukua muonekano mpya. Wananchi sasa wanataka kujua kuhusu

  Death penalty

  Karibuni watataka misimamo ya wagombea urais juu ya

  Abortion

  Gay rights


  :))
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Aug 26, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Oh yes, those are the hot button issues that I want to know where the candidates stand.....don't you?
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0

  nataka tena sana tu...............wacha akijibiwa mchambuzi suala lake la hukumu ya kifo labda na hayo mengine mawili yatatizamwa

  :))
   
 13. T

  Taso JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  they are not even in the conversation within the TZ social-political scene, how can they be "hot button" issues?

  preposterous dreams of a diaspora generation out of touch
   
 14. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Hivi waungwana sheria inasemaje katika hali hii "Itokee Dr.Slaa anashinda Uchaguzi wa Rais,Lakini kwa bahati mbaya ana Idadi ndogo mno ya wabunge walioshinda ktk Bunge la Jamhuri...Sheria bado inamruhusu kuunda serikali kutoka miongoni mwa Wabunge wachache wa chama chake?"
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Whether they are in the conversation or not, they are 'hot button issues' because they are controversial and are bound to trigger intense and emotional reaction from people.
   
 16. T

  Taso JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  if the issues are not in the conversation how can they be controversial?

  importing irrelevant foreign issues reflects total lack of ingenuity in framing the real issues
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Gaijin ka-speculate kutokana na Mchambuzi kuleta issue hii hapa ili iwe discussed as if Watanzania kwa wingi wanaongelea hili swala. Ndiyo maana kasema "naona." Lakini kama kawaida yako, ume comment kwa lengo la kubeza watu walio ughaibuni kuwa wako out of touch... [I do not wish kuongelea urefu wa uwepo wako hapa Bongo!]. Taso you do not represent the Tz social-political scene kiasi kwamba unaweza kusema hayo authoritatively hayaongelewi popote pale katika jamii na nyanja za siasa.

   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Aug 26, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Abortion is not an 'irrelevant foreign' issue!! Homosexuality is not an 'irrelevant foreign' issue. Capital punishment is not an 'irrelevant foreign' issue.

  Just because those issues are not in the conversation (per you, of course) it doesn't mean that they are irrelevant or foreign. Failure to even see that speaks volumes about your nescience.
   
 19. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kitu kuwa controversial si lazima kiwe kinaongelewa kila pahala.

  Anzisha basi thread zenye hizo real issues badala ya ku-diverge attention za members kwenye thread za watu na topics walizochagua wao kuongelea.
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkulu Mwawado, nijuacho likitokea hilo ni kuwa hawezi kuunda serikali inayoongozwa na chama kimoja. Nadhani itakayo tokea ni kuunganisha vyama, au mmoja wa walioshinda wabunge wengi kuwa PM. Serikali ya mseto ni uwezekano mkubwa zaidi iwapo hilo linatokea.
   
Loading...