SoC01 Maswali yanayoulizwa sana kuhusu lishe na mtindo bora wa maisha

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 13, 2021
6
6
JE, NINA WEZA KUTUMIA JUISI BADALA YA MATUNDA?

Inashauriwa kula tunda halisi badala ya kunywa juisi ya matunda halisi,kwani matunda yana nyuzinyuzi kwa wingi na hivyo husaidia kuongeza makapi mlo mwilini.makapi mlo husaidia mfumo wa chakula kufanya kazi kwa ufanisi na husaidia MTU kupata haja kubwa kwa urahisi.

JE, NI MAFUTA YAPI YALIYO BORA KUPIKIA?

Mafuta ni muhimu mwilini lakini yanahitajika kwa kiwango kidogo,hivyo kuacha kabisa kutumia mafuta huweza kuleta athari katika mwili ikiwemo ubongo kutofanya kazi vizuri.Vilevile mafuta yakitumika kwa wingi huleta athari katika mwili.
Mafuta yanayoshauriwa ni yatokanayo na mimea ,mafuta haya huwa katika hali ya kimimnika katika joto la kawaida ,mafuta haya ni kama ya soya ,ufuta, mawese ,alizet,pamba.ikumbukwe kwamba ni muhimu kuweka mafuta kwa kuasi kidogo kwenye mboga mboga zenye rangi ya kijani ili kurahisisha upatikanaji wa vitamin A.

JE, MATUMIZI YA CHUMVI NYINGI YANA MADHARA GANI?

Chumvi inapotumika kwa kiasi kidogo haina madhara,kwa wastani tunahitaji chumvi chini ya gram 5(kijiko kidogo cha chai).Hii husaidia mwili kupata madini ya sodium yanayohitajika kwa siku.lakini matumizi ya chumvi kupita kiasi yanaongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa LA damu kwani chumvi hukusanya maji mwilini,na maji yaliyokusanyika huongeza shinikizo kwenye moyo na mishipa ya damu hivyo kufanya moyo ufanye kazi kwa nguvu zaidi na shinikizo LA damu husababisha magonjwa mengine sugu kama ya figo na uzito uliopituiiza ambao baadae huleta athari katika mifupa ya miguu(osteoporosis).

JE, NIFANYE NINI ILI NIWEZE KUPUNGUZA MATUMIZI YA CHUMVI?

Kupunguza matumizi ya chumvi kutasaidia kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa sugu.Yafuatayo yatasaidia kufikia lengi hilo;
Punguza chumvi inayowekwa kwenye chakula wakati wa kupika
Usiongeze chumvi katika katika chakula wakati wa kula pia usiweke chumvi mezani
Epuka vyakula vilivyosindikwa kwa kutumia au kuongezwa chumvi kama nguru aliyekaushwa kwa chumvi, baadhi ya vyakula vya makopo au paketi.
Tumia zaidi vyakula vya fresh unavyopika mwenyewe
Tumia zaidi viungo kuongeza ladha kwenye chakula mfano vitunguu saumu na tangaeizi

JE, NYAMA NYEKUDU ZINA MADHARA GANI MWILINI?

Tafiti zinaonyeaha kuwa nyama nyekundu zinapotumika kwa wingi husababisha srartani ya kunywa koo utumbo moana na kongosho.Vievile nyama nyekundu INA lehemu (cholesterol) nyingi ambayo husababisha magonjwa ya moyo ,shinikizo kubwa LA damu, kisukari na kiharusi.Kama unatumia nyama nyekundu inashauriwa isizidi nisu kilo kwa wiki .Ni vyema kutumia nyama nyeupe zaidi ambayo inatokana na samaki ,kuku bata pamoja na bata mzinga.Nyama nyekundu hutokana na ng'ombe mbuzi kondoo nguruwe na sungura.

JE, MGONJWA WA KISUKARI ANAWEZA KUTUMIA ASALI BADALA YA SUKARI?

Mgonjwa wa kisukari hashauriwi kutumia asali katika chakula au kinywaji chake kwani asali ina sukari nyingi hivyo husababisha kuongeza kiwango cha sukari kwenye damu kama ilivyo matumizi ya sukari. Matumizi ya asali yanaweza husababisha madhara kwa mgonjwa wa kisukari.

JE, NIFANYAJE ILI KUPUNGUZA UZITO ULIOKITHIRI NA UNENEE?

Uzito na unene uliokithiri ni hatari kwa afya yako na unaeza husababisha magonjwa yasiyoamvuliza kama saratani magonjwa ya figo kisukari na moyo.mbinu za kupunguza uzito ni kuzingatia ulaji unaofaa,kupunguza matumizi ya vyakula vyenye nishati lishe kwa wingi, kupunguza matumizi ya vyakula vyenye mafuta na sukari kwa wingi na kufanya mazoezi angalau kwa dakika 30 tu kwa Sikh au dakika 60 angalau msra tatu kwa wiki.

#story of change
 
Back
Top Bottom