Maswali yanayoniumiza Kichwa Ajali ya MV SKAGIT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali yanayoniumiza Kichwa Ajali ya MV SKAGIT

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by silent lion, Jul 22, 2012.

 1. s

  silent lion JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  wananchi wenzangu tusikubali kufanywa wajinga na hawa wanasiasa njaa. kuna maswali mengi ya kujiuliza

  1. kama suala ni upepo na hali ya bahari kuwa mbaya, kwa nini iathirike meli ya skagit peke yake? ikumbukwe kua wakati ajali inatokezea, kulikua na meli nyingi katika bahari kama flying horse, kilimanjaro 3, majahazi ya tanga achilia mbali vidau vya uvuvi. sasa hivi vyote kwa nini havikuathirika

  2.Pili jee mamlaka za hali ya hewa na bandari zilikua wapi hazikuona dalili ya upepo. Mbona watu wa hali ya hewa wanasema walishatoa taarifa ya upepo lakini ikawa delayed kupokewa na watu wengine?

  3.Hizi meli tokea ziko marekani zilikua zinalalamikiwa kutokana na kutokuwa salama hususan umbo lake ambalo liliongezwa. pia wananchi wa huko walilalamika kuwa hizi meli (skagit na dada yake Kalama) zinayumba mno baharini, (angalia mtandao), hata hapa JF zilishajidiliwa. Jee wataaalamu wetu hawakulijua hilo?

  4.Meli inasemekana ilizama saa saba na nusu, lakini chombo cha mwanzo kufika kilikua ni kilimanjaro nacho kiliwasili saa tisa na nusu, jee muda wote huu maofisa wa serikali walikuwa wapi?

  5.Kwa nini nahodha na baharia wake walishindwa kuact accordingly? inasemekana boti ilikuwa katika mwendo wa kasi mno, huku inayumba na huku hali ya bahari ikiwa chafu. Lakini nahodha akatoa tangazo kwamba abiria wasiwe na wasiwasi. Ghafla meli ikazama. Jee huyu nahodha na hawa mabaharia walikua na sifa? na jee nani aliwaruhusu kuwa katika chombo hicho.
   
 2. s

  silent lion JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Wadau karibuni tujadili
   
 3. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,866
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Haya mambo hata mimi yananishangaza kwani kuna madau yalikuwa yantumiwa kutafuta wahanga wa ajali baharini. Kama hali ya hewa ingekuwa mbaya kiasi hicho, basi madau kibao yangezama na / au mabaharia wa madau wangekataa kushiriki uokozi. Mambo yote ni aidha chombo kilikuwa kibovu, kilijaza kupita uwezo wake au nahodha hana ujuzi.
   
 4. s

  silent lion JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Kweli kabisa ni lazima viongozi wawajibike kwa hili badala ya kukurupuka kua ni Act of God
   
 5. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Bahati mbaya tukio lenyewe limechukuliwa kisiasa zaidi.
   
 6. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,866
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Katika habari zilizotangazwa usiku huu,serikali ya Zanzibarimebainisha kuwa hii ajali ni "act of God"; nimeshituka kiasi na kujiuliza labda ni act of satan, Mosi design ya hii meli ni kutembea kwenye mito, Zanzibat ikaiandikikshga iteembee baharini, pili uwezo wake by design ni watu 230, wao wanabeba hadi 300 na tani 26 juu, iliwahi kuzimika baharini haukuchukua hatua ya kuzuiliwa kubeba binadamu. Sasa hapa ni act of GOD or act of People or act of Satan?
   
Loading...