Maswali ya wazi kwa Hapiness katabazi- Ni mgomo wa Madaktari kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali ya wazi kwa Hapiness katabazi- Ni mgomo wa Madaktari kweli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kizimkazimkuu, Jan 31, 2012.

 1. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Hapiness katabazi, mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima; siku ya jumatatu aliandika makala yeye kichwa cha habari Ni Mgomo wa madaktari kweli. Nimeinakili makala hiyo hapa na nimeweka maswali (rangi nyekundu)yangu kadhaa nikimpa changamoto ayajibu. Lengo langu ni kumtaka aisome tena kwa makini makala yake kishe apime dhamira yake kama mwandishi wakati anaandika makala hiyo. Nasubiri majibu yako Happiness K

  Ni mgomo wa Madaktari kweli-Happiness Katabazi Tanzania Daima Jumatatu 30, 2012
  Kwa takriban wiki moja sasa vyombo vya habari vimekuwa vikipambwa na habari za mvutano baina ya serikali na madaktari kuwawamegoma kufanya kazi kwa kile wanachodai kupandishiwa mishahara, kujengewanyumba za kuishi na kuongezewa masurufi yao. Taarifa za mvutano huo binafsi zimekuwa zikinikosesha raha na kunikeramno na kuanza kutamani kuwa na viongozi madikteta
  .

  Swali: Tamaa yako ya kuona udikteta Tanzania inatokana na nini? Sio nyie waandishi wa habari mliokuwa mnapinga mabadiliko ya sheria ya habari mkiita yaki kandamizaji (na kidikteta).. halafu hao viongozi madikteta wafanye nini?

  Baadhi ya madaktariwalinukuliwa wakisema wamevuka hadhi ya kiwango cha kuongea na Waziri wa Afyana Ustawi wa Jamii, Dk. Juma Mponda, kwani ameshindwa kutatua mgogorowao na mwenye uwezo wa kuongea naye hivi sasa ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda nakushinikiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Brandina Nyoni, hii ni dharau ya aina yake.
  Swali: Labda utukumbushe nani aliyewanukuu hao madaktari; kwa sababuw anachoeleza sababu ya kukataa kuonana na wizara ni kukosa imani nao (B.Nyoni, D.Mtasiwa na H.Mponda) kwa kuwa walipofuatwa kwa mazungumzo hawakutoa ushirikiano. Pengine hao walio wananukuu madaktari ambao umewatumia kama source yako ya taarifa waombe pia wakuambia kauli iliyonikuliwa kutoka kwa B.Nyoni alipofuatwa na viongozi wa madaktari ofisini kwake.

  Wakati madaktari hao wakitoa maneno hayo, Waziri waAfya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, Alhamisi ya wiki iliyopita alifanyamkutano na waandishi wa habari na kutoa tamko la serikali na ufafanuzi kuhusumadai ya madaktari hao na bila kumung'unya maneno alisema serikali haiwezikuwaongezea mishahara na kufikia shilingi milioni 3.5 kwa kuwa kada hiyo inalipwa vizuri tu.

  Swali: Mwandishi makini alipaswa achambue kauli ya waziri anaposema madaktari ni kada inayolipwa vizuri anawalinganisha na nani (kwa muundo wa utumishi). Kwa jinsi unavyoondika unaonesha una chuki au umetumwa. Ulichofanya hapa ni kuchukua press release ya waziri na kuongezea maneno/mawazo yako binafsi na kuyamwaga gazetini. Nakuomba unijibu ; waziri aliposema " ni kada inayolipwa vizuri tu " ulielewa nini, na unatarajia wasomaji wako waelewe nini?

  Dk. Mponda alisema mishara ya watumishi wa serikalihufuata miundombinu ya watumishi iliyopo ambayo iliboreshwa kwa sekta ya afyana hivi sasa watumishi wa afya wanapatamishahara mikubwa kuliko watumishi wengine serikalini. Ieleweke kwambabaadhi ya madai ya madaktari ni ya msingi na tayari serikali imesemainayafanyia kazi.

  Hapo nilipo Bold; utanijibu hapo juu; Sasa nikuulize tena waziri anapotaka ieleweke kuwa baadhi ya madai ya madaktari ni ya msingi wewe kama mwandishi ungependa kujua ni yapi yaliyo ya msingi? Au kwako hilo sio la muhimu; you just copied the press release sio?
  .

  Ila sikubaliani na hatua ya madaktari hao kukiukaviapo vyao walivyoapa kuwa watahakikisha wanahudumia wagonjwakatika mazingira yoyote yalelakini hivi sasa wameamua kuwatoroka wagonjwa na kwenda kufanya migomo na‘deiwaka' katika mahospitali binafsi ili waweze kujiongezea kipato. Na kitendohicho hakina tofauti na jambazi ambaye anamwelekezea bunduki kichwani mwananchiakimtaka ampatie fedha ama sivyo anamuua au hakina tofauti na daktari ambayeanamtibu mgonjwa halafu anamwambia hawezi kumpatia dawa hadi ampatie hongo.
  Kwanza nakubaliana na maelezo ya Waziri Mponda kuwasuala la kupandishiwa mishahara na masurufu mengine kwa watumishi wa umma kunautaratibu wake. Wafanyakazi wa serikali wanaodai kuongezewa mishahara namasurufi mengine wanapaswa kufuata utaratibu mahususi ulioanishwa ndani ya‘Civil Service Negotiation Machinery Act' na kama serikali itashindwakutekeleza madai yao yaliyofuata utaratibu wa sheria hiyo wanaruhusiwa kugoma. Sasatuwaulize hawa madaktari walifuata utaratibu ulioainishwa katika sheria hiyohadi wafikie uamuzi wa kugoma ? Na kama hawakufuata utaratibu, sheria za nchiziko wazi ambazo zinawabana wale wote wanaofanya kazi au kutoa ushahidi chiniya kiapo na pindi wanapokiuka viapo vyao wanatakiwa waadhibiwe mara moja.
  Maana ni wenyewe walieleza kuwa madai yaowaliyafikisha wizarani na WaziriMponda akasema aliupokea ujumbe wa chama cha madaktari na wakajadiliana naserikali ikaueleza ujumbe huo kuwa baadhi ya madai yao, serikali inayafanyiakazi.

  Swali: Waziri hajaeleza ni lini aliyapokea madai ya madaktari kwa mara ya kwanza na (narudia tena) ni madai gani aliyaona ya msingi na yapi aliyapuuza. Ndugu mwandishi ulijiuliza hili swali? Hivi kama waziri aliyapokea madai hayo siku saba zilizopita ama miezi sita iliyopita wewe unadhani kuna tofauti yeyote? Je ungependa kujua ni yapi serikali inayafanyia kazi na imefikia wapi?

  Na baada ya Dk. Mponda kutoa ufafanuzi huo,hatujakisikia chama hicho cha madaktari kikipinga maelezo ya waziri huyo kwakutoa ushahidi mbadala, matokeo yake tunakisikia chama hicho kikisema kuwahadhi yao kwa sasa si ya kuongea na waziri huyo, hadhi yao hivi sasa ni yakuzungumza na Waziri Mkuu. Haya, Pindawaliyekuwa wakimtaka alikwenda Karimjee kuzungumza nao, lakini wao walishindwakutokea kwa sababu zisizokuwa na kichwa ambazo sasa zimenilazimu nianze kuaminikuwa huu siyo mgomo wa madaktari bali una ajenda mbaya iliyofichika nyuma yake.

  Swali: Pengine ndugu mwandishi ungerejea sababu walizotoa madaktari kukataa kuonana na Pinda (wasomaji wako ndio watapima kama zina kichwa au miguu). Halafu,utuambie ni ajenda gani inayoweza kujificha nyuma ya mgomo wa madaktari;unataka kuwaaminisha wasomaji wako kuwa hawa wanaokutana kwa mgomo sio madaktari?Je ni kina nani hawa basi ambao kwa wao kugoma huduma mahospitalini zinazorota?

  Hivi nani kairoga nchi hii? Madaktari ndiyo wenyeshida na Waziri Mponda ndiye waziri wao, lakinicha kushangaza madaktari hao ambao ndiyo wenye shida wamegeuka kuwa manyaparawa kutoa amri ya kutaka nini na nani wazungemze naye na cha ajabu hadisasa serikali inaendelea kuwakumbatia?

  Swali: Kabla ya kushangaa na kutushirikisha mshangao wako, (nimekuulizahuko juu) Mponda aliyapokea matatizo ya madaktari kwa mara ya kwanza lini?

  Nyie madaktari kwa akili zenu waziri alichokizungumza mnafikiri kabla yakukizungumza huyo Waziri Mkuu Pinda alikuwa hakijui? Waziri wenu kasemaserikali inayafanyia kazi madai yenu hamsikii sasa mnataka nini? Niulize uleujumbe wa madaktari uliokwenda kuzungumza na Dk. Mponda kuhusu madai yao naakawasikiliza, walikuwa hawajui waziri huyo siyo saizi yao na kwamba hana uwezowa kuwatatulia kero zao? Mlimfuatia nini ?. Ni lini wamegundua Waziri Mpondasiyo saizi yao? Je ni baada ya waziri huyo kuwaambia ukweli kuwa haitawezakuwapandishia mishahara?

  Swali: Katika hili unajichangya mno, lakini ukijibu baadhi ya maswali yangu yaliyotangulia naweza kukuelewa.

  Kwa mtazamo wangu, kwa upande wako Waziri MkuuPinda, aibu uliyoipata jana ulijitakia kwani haiwezekani wewe Waziri Mkuu namawaziri wote wapo chini yako na wanakusaidia katika utendaji kazi wako wa kilasiku, madaktari wanamtolea maneno yashombo Waziri wa Afya Dk. Mponda na maofisa wake ambao ndiyo wenyedhamana ya sekta hiyo, halafu na wewe unakubaliana na dharau hiyo ya madaktarikwa kuamua kwenda kuwaona na matokeo yake na wewe wamekudhalilisha umejikutaukumbini peke yako.

  Sidhani kama ulihitaji maneno ya taarab na mipasho kujenga hoja zako.

  Nchi hii hivi sasa heshima ni bidhaa adimu katikangazi zote kuanzia ya familia. Hatuheshimiani, tunadharauliana bila sababu zamsingi. Hajulikani baba ni nani, mama ni nani, mkubwa ni nani, mtoto ni nani nakiongozi ni nani. Kila mtu anaongea na kufanya analotaka. Na hali hii isipotokomezwaipo siku taifa hili litajikuta limetumbukia matatizoni. Hivi mnadhani hayomadai yenu ya kupandishwa mshahara ndiyo mtapandishiwa leo leo? Je, hizo nyumbamnazodai mjengewe ndiyo ujenzi wake utakuwa umekamilika ndani ya siku mbili?Lakini wafanyakazi wengine kwa uhalisia wa fani zao walioajiriwa serikalihawawezi kufanyakazi kazi serikali na sekta binafsi kwa wakati mmoja, lakiniwafanyakazi wa aina hiyo hatujawasikia wakigoma. Sasa kama hivyo ndivyo nikwanini madaktari mnaofanya kazi sehemu mbili na mwisho wa mwezi mnapatamishahara miwili mfikie hatua hiyo ya kutisha? Mbona kule kwenye hospitali zasekta binafsi mnakofanyia kazi hamuwagomeagi mnakuja kuigomea serikali?

  Hivi kweli, ulikuwa unamaanisha hayo maswali yako hapo juu?; katika madai ya madaktari (kama unayafahamu kwa kuyasoma na sio kusimuliwa) walitamka popote kuwa wanataka nyumba kesho? Na mishahara keshokutwa? (namaanisha walitoa timeframe). Halafu mbona hutaki kuyataja madai mengine ya madaktari? Au katika haya uliyoyataja yako katika kundi lipi la madai anayoyajua Mponda (ya msingi anayoyafanyia kazi au baadhi aliyoamua kuyaapuuza?) Kuuliza kwanini madaktari hawagomi ktk sekta binafsi ni kujichanganya na inaonesha hujui madai yao yamsingi. Kwa kifupi makala yako ilikuwa na lengo la kuuonyesha umma kuwa madaktari ni watu wabaya sana lakini kwa kuwa hukutulia na kujipa muda kulielewa tatizo, na kujieleimsha kabla ya kuandika makala yako umeishia kuchangaya mambo mengi na kuifanya dhamira yako mbaya iwe wazi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Nakushauri uyatume Tanzania Daima au mtumie kwenye e-mail yake kwa vile yeye sii mwanachama humu jf. Mwana jf ni bosi wake Kibanda!.
   
 3. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  maswali haya nimeyaweka katika comment box katika blog yake FJ lakini naona ameamua kutokuziweka. naamini atasoma hapa au ameshasoma kwenye blog yake.
   
 4. kitonsa

  kitonsa JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Labla tuwaulize walimu wake Mugabe primary, sinza wakina zungiza, masenga na naobena labla na nyagawa na kaka yake riston wanaweza wakajibu!! Kama wakishindwa labla tumuulize baba yake japo waliachana na mama yake kule ukuta wa posta sinza!!
   
 5. L

  Lsk Senior Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...msiomfahamu Katabazi mtahangaika sana. Ana bahati ya mtende ya kuwa karibu kimahusiano na bosi wake,vinginevyo kashfa ya kupewa kitita kikubwa na wenye RICHMOND ingemuondoa Tz-Daima. Inasadika maandiko yake ya utetezi wa Richmond yalisababebwa na bonge la mlungula alopewa na Rostam
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Umejuaje si memba wa jf?
   
Loading...