Maswali ya sensa haijagusa kabisa takwimu za kisiasa

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Kuna umuhimu mkubwa kupata takwimu za kisiasa zitakazosaidia kuweka utaratibu na muundo bora wa utekelezaji wa demokrasia. Takwimu muhimu za kisiasa zinazohitajika;
1.Idadi ya wananchi ambao ni wanachama wa chama cha siasa tawala au upinzani....

Tutambue ukubwa wa watu wasio wanachama wa chama chochote ili watambulike na kutumiwa katika mustakabali wa nchi.Kama watu wengi hawana vyama je ipo haja ya kuendelea kutoa ruzuku kwa vyama vilivyopo? Pia wasio na vyama wakiwa wengi maana yake ni lazima sasa kuruhusu wagombea huru katika chaguzi za nchi..

Je kama wasio na vyama ni wengi tuendelee kufanya uchaguzi wa rais kwa uwakilishi wa vyama pekee au inabidi turuhusu uwakilishi wa muungano wa watu na vyama alliances kama ilivyo Kenya?

2.Suala lingine muhimu la kisiasa ni kujua idadi na ukubwa wa kundi la watanzania wazanzibari wanaoshi na kumiliki makazi/ardhi na kufanya biashara au kazi tanzania bara..hii itatoa picha halisi ya maendeleo ya muungano wetu lakini pia kuthibitisha umuhimu wake na kupelekea baadaye kuwa na muungano wa serikali moja.
 
Back
Top Bottom