Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu yana mambo mengi ya kujiuliza

Teleza1

Senior Member
May 16, 2020
190
198
Vijana kama vijana tunasakamwa kila kona.Ukianzia nyumbani hapasomeki, wazazi wakati mwingine wanakuona kama mzigo, ukija kwa watengeneza sera wa nchi ndo balaaa! Viongozi wetu balaaa kubwa.Mara hatuwezi kuweka hata mbolea!

Kazi kushinda mitandaoni ohh!? Mara kazi kuvuta shisha.wakati tunakua tuliambiwa vijana ndio taifa la leo lakini kwa yanayotokea ina furahisha nadhani vijana wanaozungumziwa kama taifa la kesho nimekuja kugundua ni watoto kama wa akina pinda, ndungai, jakaya, pombe, na viongozi wengine hao ndo taifa la kesho.

Katika hotuba ya waziri mkuu nimemsikia kwamba anasema wamekwisha ajiri waalimu 8000, na wengine 5000 majina wamesha yatoa wanaendelea kuripoti vituoni. Sijajua kauli nitumie kauli gani rasmi, waziri alidanganya bunge au yeye alidangwanya na jaffo. Maanake majina hayajatoka majina yanayotoka ni kwamba ni wanapigiwa simu kwa maelekezo maalum waende kuripoti vituo vipya vya kazi.Kwa maana hiyo waziri mkuu alidanganya bunge kwa kuwa hakuna cha ajira zaidi ya watu wachache kupangiwa kazi kwa mtonyo.

Hii inawafikirisha sana vijana waalimu wasio na kazi wako mtaani kama serikali ya wanyonge inayojinasibu kwa kutetea wanyonge itoe ajira kwa waalimu hawa. Nasio kuwapiga dana dana. Siku hizi hata ukienda private unatakiwa ujitolee kwa miezi mi3 kisha unaweza kufikiriwa kazi vijana tunanyanyasika hakuna wakutusemea. Serikali ifanye mambo yake chonde chonde isituzalau vijana kwani sisi ndio wazee wa kesho.
 
Wataajiri hao walimu elfu 5 kwa hela ipi? Wamejianzishia mamiradi lukuki ili tu kupata umaarufu wa kisiasa! Na sasa wanachechemea. Maana inakomba hela zote kwenye kile chungu chao! Hali mtaani ni tete!

Hela zote wanachukua Wachina, Waturuki, Wajapani na Wakorea! Wafanyakazi hawajapandishwa madaraja kwa miaka sita sasa! Wakulima hali ni mbaya! Wafanyabiashara nao wako kwenye vita na mamlaka za serikali!

Tutaelewana tu.
 
Mandeleo ya vitu lazima yaende na maendeleo ya watu mkuu, sasa kama tutaipa miradi kipaumbele watu tutaisha halafu miradi hiyo ataitumia nani!?
 
Umeongea kwa uchungu sana kijana.

Nyinyi vijana ndio kitu pekee cha kuleta mabadiliko. Mkiamua mnaweza. Kama waliwaambia nyinyi ndio Taifa la leo basi kamateni usukani. Msisubiri mtu aje awape madaraka yenu. Tatizo wazee tumekuwa na imani kuwa sisi ndio tunatakiwa kuwaamulia vijana kila kitu!.

Amkeni!
 
Daaah kuna vijana wengi mambo hayako vizuri lkn basi tunamwachia alie juu hili ni bomu kubwa
 
Majina ya hao walimu 5000 wame display wapi?
Siyaoni kwenye Ukurasa wa TAMISEMI
Kama wanaweza kuficha ajali ya Mbunge wanashindwaje kidanganya kuhusu ajira hewa 5000? Wanakwambia nenda mashuleni ukawahesabu kama hawafiki 5000? Awali walipotoa majina walisema ni 13,000 watu waliposhituka wakaja na ngonjera kwamba ajira ziko awamu 2.

Majina ya awali yakajirudiarudia, walipoulizwa wakafuta haraka haraka. Walimu walioripoti vituoni baadhi yao wakagundulika hawajawahi kusomea ualimu. Wakurugenzi walipowakataa wakaitwa Dodoma. Nchi ya mazlingaombwe hii, Rais Mwanamalundi Waziri Kalumanzira.
 
Kama wanaweza kuficha ajali ya Mbunge wanashindwaje kidanganya kuhusu ajira hewa 5000? Wanakwambia nenda mashuleni ukawahesabu kama hawafiki 5000? Awali walipotoa majina walisema ni 13,000 watu waliposhituka wakaja na ngonjera kwamba ajira ziko awamu 2. Majina ya awali yakajirudiarudia, walipoulizwa wakafuta haraka haraka. Walimu walioripoti vituoni baadhi yao wakagundulika hawajawahi kusomea ualimu. Wakurugenzi walipowakataa wakaitwa Dodoma. Nchi ya mazlingaombwe hii, Rais Mwanamalundi Waziri Kalumanzira.
Wakurugenzi wakaitwa Dodoma
 
Umeonaeee!!tunatawaliwa na wahuni,Wales walio faulu kwa kuingia na vibuti kwenye mitihani
 
Kama wanaweza kuficha ajali ya Mbunge wanashindwaje kidanganya kuhusu ajira hewa 5000? Wanakwambia nenda mashuleni ukawahesabu kama hawafiki 5000? Awali walipotoa majina walisema ni 13,000 watu waliposhituka wakaja na ngonjera kwamba ajira ziko awamu 2.

Majina ya awali yakajirudiarudia, walipoulizwa wakafuta haraka haraka. Walimu walioripoti vituoni baadhi yao wakagundulika hawajawahi kusomea ualimu. Wakurugenzi walipowakataa wakaitwa Dodoma. Nchi ya mazlingaombwe hii, Rais Mwanamalundi Waziri Kalumanzira.
Hatari
 
Nchi yetu nzuri imepata watawala wa ajabu sanaaaa, mm ck nne kabla ya kauli ya maziri mkuu niliwauliza Tamisemi kuhusu hizo ajira za kupigiana simu, wakakanusha na kunihakikishia ajira zikitoka lazima ziwekwe kwenye tuvuti yao ya tamisemi. Lakini baada ya ya yule jamaa kuongea juzi ilibidi niamini kuwa jamaa hawajaajiri na kama wameajiri hao 5000 bc hawafiki ata 500 ili kutupoteza. Nimeamini serikali hii wote ni waongooo. Usishangae ukaenda kupima malaria lkn kwa sabb huenda dawa za malaria hazipo, wakakwambia hawajaona ugonjwa ili wakupe panado ambazo ndo zipo😁😁 usiiamini hii serikal kamweeeee. Labda tusubiri utawala mwingine🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom