Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni: Akerwa na maandamano ya CHADEMA

Bundajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
244
47
Ameanza kuelezea jinsi Lema alivyojifungisha gerezani
Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) aliyesema kuwa mgogoro wa vyama vya CCM na Chadema wa umeya wa Arusha umevuka mipaka na kusambaa nchi nzima na kuwa wa kitaifa. "Hivi sasa (mgogoro huo) umevuka mipaka ya kivyama na umekuwa wa kitaifa na kusambaa maeneo mbalimbali ya nchi na kwa kuwa (Pinda) ulilitambua hilo na ukaandika barua kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na baada ya kupokea majibu ya CCM je, upo tayari kutoa maelekezo mengine ama ushauri mwingine ili upande wa pili ujue hatima ya suala hili na ijue hatua za kuchukua?" Alihoji Mnyika.

Pinda alijibu;
"Ndugu Mnyika usilikuze jambo hili kama limesambaa nchi nzima, si kweli, lakini kikubwa ninachokiona katika mazingira ninayoyaona, wenzangu wa Chadema mnayoyafanya kinachohitajika ni dhamira ya kweli kwa pande zote mbili, kwa namna mambo yenu mnavyoyafanya huoni dhamira ya kweli. "Kila siku maandamano kila mahali sisi tulioko serikalini tunapata tabu sana, tunataka kufanya kazi nyingine ambazo zinahitajika, lakini muda wote unakaa unafikiria maandamano. "Mteremke chini kidogo, tuanze kuona maslahi mapana ya nchi, tuone ni mambo gani ya msingi yanahitajika, kwa pamoja twende mbele," alisema.

Peoples Power inamtisha Pinda
Alisema tabia ya uanaharakati ya Chadema inanipa taabu sana, lakini kama umakini utakuwapo, haoni tatizo watu kukaa na kuzungumza suala hilo, "katika hali ninayoiona mimi ‘peoples power' kila kukicha si nzuri, haiwezekani."

Kuhusu mgogoro wa umeya wa Arusha
Pinda alisema kama Chadema inaona haja ya kukaa kwa mazungumzo iandike na kuelezea maeneo inayoyaona yanahitaji kujadiliwa. Awali Pinda alieleza kuwa aliingilia mgogoro huo kwa kumwelekeza Msajili akutane na vyama hivyo, kuona maeneo ya kuzungumza akiamini tatizo litapatiwa ufumbuzi lakini CCM ilijibu kwa barua kwamba haioni cha kuzungumza.

Kuhusu Lema:
Akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (CCM), aliyetaka kufahamu kwa nini Serikali imemzuia Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutoka rumande na kuathiri utalii, alisema Mbunge huyo hakuzuiwa bali mwenyewe alikataa dhamana. Alisema wanatarajia Novemba 14 kesi hiyo itakapotajwa, Mbunge huyo anaweza kuachiwa na kuongeza kuwa utalii haujaathirika kutokana na vurugu hizo, lakini akawataka wananchi kuzingatia amani ili utalii huo usiathirike
 
Naona Waziri Mkuu amekwepa kujibu swali ambalo limeulizwa juu tanzania kukubali ndoa ya jinsia moja likimtaka atoe kauli ya serikali, badala yake amesema kauli tayari imeishatolewa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje, kwahiyo yeye binafsi anaungana na kauli za watanzania; .
 
Nimesikia hali ni tete huko mjengoni,tujuzeni jamani ngeleja hayupo kwetu leo
 
Pinda ilikuwa ni lazima ajibu kipumba pumba kwa kulinda kibarua chake
 
Naona Waziri Mkuu amekwepa kujibu swali ambalo limeulizwa juu tanzania kukubali ndoa ya jinsia moja likimtaka atoe kauli ya serikali, badala yake amesema kauli tayari imeishatolewa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje, kwahiyo yeye binafsi anaungana na kauli za watanzania; .

Kuna dalili kuwa hawa jamaa hawana dhamira ya dhati kukataa ushoga...Pinda kama Kiranja wa mawaziri na mkuu wa kazi za serikali bungeni alipaswa atoe matamko makali kama Dr Shein na raisi wa Ghana....Hapa kwetu mkuu wa kaya kafyata mkia,kiranja wa mawaziri kafyata mkia then unategemea nini?
 
Kwa walioangalia maswali ya papo kwa papo Bungeni leo Shujaa kijana Mnyika..kambana waziri mkuu kama anaona tatizo lililopo kwa sasa dhidi ya kunyimwa haki na kuingiliwa na dola katika mambo ya kisiasa..

Kama anaona wakati umefika wa Waziri mkuu kukaa pamoja na kutaka kuweka njia sana ya amani nchini..Kweli waziri mkuu hakuingia moja kwa moja kwenye kujibu hoja ila kwa upande fulani anaonekana kuwa anajua linaloendelea..

Ila kasema kama Serikali neno PEOPLES POWER PEOPLES POWER kila kukicha linawasumbua akili...

Nawakilisha
 
Pinda anajiaibisha kwa kujibu suala la mgogoro wa Arusha juu juu.
Suala la Arusha tutalitatua bila kauli ya pinda wala nani. Nguvu ya umma itaamua.
 
Nimesikia hali ni tete huko mjengoni,tujuzeni jamani ngeleja hayupo kwetu leo

Mkuu nimefurahi na huo msamiati mpya....ngeleja!!!! ha ha ha ha ha ha!!! On the other side,Pinda kapigwa swali na Regia Mtema kuhusu Ushoga akaanza kujichekesha kama mkuu wa kaya sijui kamuambukiza?

Na amekwepa kujibu hilo kwa umakini.....akaulizwa ishu ya Meya wa Arusha na Kamanda Mnyika kama kawaida tena anaonyesha kuna uhuni tu unaoendelea na tusitegemee utulivu Arusha siku za karibuni...
 
hili limesemwa na yeye mh Pinda wakati akijibu swali la mh Mnyika Bungeni juu ya hali ya Arusha inavyoendele.
 
Naona Waziri Mkuu amekwepa kujibu swali ambalo limeulizwa juu tanzania kukubali ndoa ya jinsia moja likimtaka atoe kauli ya serikali, badala yake amesema kauli tayari imeishatolewa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje, kwahiyo yeye binafsi anaungana na kauli za watanzania; .

Yeye binafsi anaungana na kauli za watanzania??? Huyu vipi, kauli za watanzania ni zipi................ Hajuii akina aunt Moody nao wana kauli zao. Bongo havtuna viongozi ila waganga njaa tu!!!
 
Lazima wakose usingizi, maana wanajua Nchi zote zilizofanya mabadiliko ni kwa njia ya Nguvu ya watu!
 
CDM ina wabunge vichwa siyo masuburi wa magamba mlitamani wasiwepo ili mpate kupotosha kuwa wako Arusha na hawawakilishi wananchi wao, mbona mbunge mmoja tu wa CDM anawatosha, angalia magazeti kesho ya ni Pinda na Mnyika.
 
CHADEMA walianza kusema 'Peoples Power' kabla ya Tunusia na wakati wote huo serikali na hasa ccm walikuwa wanakebehi huo usemi. Ila baada ya Misri ghafla tukaanza kusikia malalamiko toka kwa hawa wakubwa hasa Chiligati alikuwa analalamika kama mtoto mdogo! Walifikia mahali wakasema 'vyama vya msimu'. Sasa kama kweli kama wao ni ngangari wasimame wenyewe bila msaada wa mitutu ya polisi.
 
Back
Top Bottom