Maswali ya papo kwa pao kwa waziri Mkuu

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
836
48
Ndg waheshimiwa wakuu mnaoendesha na kuuwezesha mtandao huu kuwa live nina ombi:

Naomba ianzishwe nafasi ya kuweza na sisi kurusha maswali kwa wizara husika au kwa waziri mkuu yanayohusu maendeleo ya nchi yetu.

Nina hakika humu wapo viongozi na wanasiasa wanaosoma mijadala yetu na inaweza kuwa nafasi ya kufikisha ujumbe kwa wahusika na pengine kuchukuliwa hatua za kutatua kero mbalimbali.

Hili nimeliona baada ya kuchunguza na kubaini kuwa mijadala mingi inayowekwa ktk JF ni ile ya matukio yaliyotokea tayari au matukio yanayotarajiwa (tetesi nk) ambayo pia siyo mbaya ktk kupashana habari.

Hivyo nimeona ipo haja ya kuwa na special page ya maswali muhimu (bila kukashfu wala kutukana) kwa wahusika serikalini na hasa wabunge wetu kama wawakilishi wetu watayaona na kuwashtua ili watafute ufumbuzi.

naomba km utaanzishwa ukumbi huu watu wasitumie kurusha makombora ya matusi au mambo ambayo hayataleta tija wala suluhisho kwa hoja zilizoulizwa, hivyo tutumie nafasi hiyo kistaarabu.

Najua zipo threads nyingi, lakini wakati mwingine inakuwa vigumu kwa kuwa masuala ni mengi sana.

Inaweza kuwa simple tu ikisema "Maswali kwa wizara husika au kwa Mh. Waziri Mkuu"

lakini yawe ni maswali ya msingi na yaliyofanyiwa uchunguzi.

Hata kama hayatawafikia mawaziri naimani wapo wabunge na watu wa karibu na wizara husika wanaosoma mijadala yetu ya Great Thinkers na wanaweza kuyafuatilia kupata uhakika zaidi na kuyafikisha sehemu husika.

Nawasilisha kwenu wakuu wa JF kulitafakari au kuona njia muafaka.
 
wazo zuri naomba ifanikiwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom